Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ratiba YA kujifunza KUMJUA Mpenzi!

>> Wednesday, October 31, 2007

Tokea kuzaliwa binadamu yuko katika ratiba ya kujua vitu fulani.
Kwa bahati mbaya binadamu atakufa bila kujua vitu vyote.

Lakini ukimuuliza mtu kajifunza nini tokea azaliwe, atakuwa na majibu mengi sana ya mambo aliyomaliza kujifunza, mpaka ataweza kukusimulia jinsi alivyoanguka wakati anamalizia ratiba ya kujifunza kuijua baiskeli.

Kama ni mdau wa kushushua , atakustua ; acha cha hizo wewe!
Swali gani hilo?

Lakini....

Swali:

  • Hakuna jipya unalojifunza kuhusu mama yako mzazi mpaka leo?
Sasaaaa....

...inaaminika kuwa mtu akijua kuendesha baiskeli , ndio imetoka hiyo. Yaani, hana cha zaidi cha kujifunza kuhusu baiskeli. Kitu hiki kinaweza kukushangaza sana ukistukia waendeshaji baiskeli maarufu, huwa wanafanya mazoezi kila siku yakuendesha baiskeli kabla hawajaingia Tour de France.Unaweza kubisha lakini kuwa hawa jamaa wafanyacho hakiko katika ratiba ya kujifunza kuijua baiskeli na miili yao waliyozaliwanayo!

AU?

Lakini...

...mimi naamini unaweza ukajifunza kitu kipya katika mikono yako mwenyewe kama utaiangalia kila siku kwa makini wakati mawazo yako yamekaa mkao wa kujifunza kuijua.


Kama ulianzia tumboni kwa mama, na inawezekana mpaka leo unaendelea kugundua mambo mapya kuhusu mama huyo huyo mpenzi aliyekuzaa, inawezekana mjumbe wa nyumba kumi kumi humjui kabisa.

Swali:
  • Unafikiri unamjua nani vile?
Ni rahisi kwa baba kudhani anamjua mtoto wake au mtoto kudhani amemaliza kumjua mama yake , hivyo kuacha kukaa mkao wa kujifunza.

Kwa wapenzi ndio kabisaa, mkao wa kuacha kujifunza kuhusu mwenzio , unakwisha mpenzi akisha kukubalia!

AU?

DUH!

Swali:
  • Si ulishamaliza kumjua rafiki yako tayari?
Nimtazamo tu mawazoni!
Usitishike!

Siku njema!

Nakuacha na SIMPLY RED wakinibishia katika swala na wimbo IF YOU DONT KNOW ME BY NOW.

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 11:50 pm  

HAkuna cha kumjua mtu yeyote asilimia mia...hata mzazi ambaye hudai kuwa anamjua mwanae..kuna vitu vingi asivyojua na mpaka huu huzidi miaka inapokwenda...wapendanao hivyohivyo...hata akishekupa...usidhani umefika:)

Simon Kitururu 2:18 pm  

@Serina:Nakubali kabisa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP