Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MARAISI WA AFRIKA WALIPWAVYO MAMILIONI ILI WAFANYEKAZI WATAKIWAZO KUFANYA!

>> Wednesday, October 03, 2007

Inasemekana binadamu hatosheki!

Ndio maana hukusikia Mobutu Seseseko, Abacha na.... wakisema wametosheka na idadi fulani ya pesa walizojilundikia wakiwa ofisini.

Swali:
Hivi Mo Ibrahim Foundation itakapomlipa Raisi mshindi wakufanyakazi atakiwazo kuzifanya dollar milioni tano , halafu kumshikisha mshahara wa dollar laki mbili kwa mwaka;itaondoa hamu ya Maraisi wa Afrika kutopenda kukaa zaidi katika ofisi zao au itaondoa kweli kale kahamu kamaraisi wetu wapendwa kakutofanyakazi watakiwazo kufanya huku wakiingiza mamilioni kwa mwaka?

Tukitoka nje ya Afrika.....

  • Hivi mnafikiria ni nini kimfanyacho Raisi wa Russia , PUTIN, kutaka kuwa waziri mkuu baada ya kumaliza URAISI?
  • Hivi unafikiri , kwanini Fidel Castro ,hajiudhuru hata pamoja na kuwa dhaifu kiafya nk.?

Naamini pesa sio kitu kizima kiwapacho motisha hawa jamaa! Pesa mara nyingine ndio ziwafanyazo kutofanya kazi wapaswazo kufanya.

Waulize akina Obama, Hillary Clinton na .. pale Marekani kuwa, kwanini wanatumia mamilioni kugombea kuingia kwenye kazi iwalipayo mshahara mdogo kuliko watumiazo kwenye kampeni , wakati Raisi wa Mexico ana pensheni kubwa kuliko wao.

DUH!
Naacha basi!

Tulia na Admiral T akiwa na Kassav

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP