JINSI WABONGO TURUDIVYO NYUMBANI BAADA YA KUBEBA MABOKSI UGHAIBUNI!
>> Thursday, October 04, 2007
Staili za kurudi bongo, kama uko nchi nyingine ni nyingi.
Na sababu za wabongo kuwepo nje ya Bongo ni nyingi.
Swali:
Hivi ushawahi kuona tangazo la kazi , wakitafuta mbeba maboksi?
DUH!
Sasaa...
Baadhi ya dondoo ya jinsi Wabongo warudivyo bongo:
Mara nyingi ni kimawazo,
...unarudi kimawazo , unajitengenezea ugali na mbilimbi, makande, kisamvu au chakula chochote kikukumbushacho bongo, huku kwa mbali unasikiliza kimasomaso au miziki fulani ikukumbushayo ulivyokuwa pale bongo kwenye kioski fulani.
Duh!
Naacha!:-)
Lakini kabla sijaacha....
- Unaweza ukajiandaa na kurudi na vyeti vyako au kale kamtaji. (si unajua siku hizi si ujanja kurudi na friji?)
- Unaweza usijiandae na ukarudi au kurudishwa tu Bongo(si unajua yote mbele kwa mbele?)
UKWELI ni KWAMBA, wote tunajua BONGO inahitaji MINYOO , samahani, MICHANGO ya Wabongo wote(walio ndani ya nchi na pembeni)
Inahitaji michango ya hata wasio Wabongo pia.
Kitu hiki, wengi tunakikumbuka ingawa tunakumbushwa kila siku na wadau na hata halihalisi ya kuwa pembeni ya mipaka ya Bongo.
Ukiwa nje ya Bongo, kitendo hicho tu cha kutokuwepo Bongo, hukukumbusha bongo. Na kama wewe ni mkereketwa, kila siku utatafuta jinsi ya kubadili jambo bongo.
SWALI:
- USHAWAHI kukutana na Mbongo HATA mmoja, AMBAYE chini na hata JUU ya moyo wake, HAJALI BONGO?
- NI nini maana ya kujali BONGO?
Nakuacha na TALINA akija na Pour te Revoir
Kumbe haimbi Kibongo ,DUH!
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Maulizo yenye changamoto juu yake.Kuna jamaa anasema kuwa suala la kugeuza moja kwa moja bongo huwa linampa fikira nyingi sana.
Hajui akifika aanzie wapi.Hivi ukipata friji kidogo na vyeti unaweza kugeuza au?
thinker sikutaka kuitia maguu yangu kwenye kona hii kwa mida aniwei umeniwin kwa hii mada.
nakujia na kibao cha 'THE GRASS IS ALWAYS GREENER ON THE OTHERSIDE.uwepo bongowatakuambia majuu ukiwa majuu siku hizi miaka ya karibuni utasikia single mpya ati bongo nyu yoki. wajasilimali wanazidi kujinufaishakwa mi slogan aniwei wewe bado hujafikiri kwamba maisha nipopote ulimwenguni? chooni, kitandani, kula, kunywa, kuvaa, makutembea well richman wealth is in the city distruction of the poor is thier proverty.
@Egdio:Kazi kweli kweli!
@Altunes:
Duh! Sikatai ulichosema!
Ukiwa na nia unaweza kuigeuza Bongo well sio yote hata mtaani kwako au kijijini kwako.
Kufanya mabadiliko sio lazima ujengee wananchi shule, unaweza ukasaidia ujenzi wa choo bora ( I mean cha matofali na kilichoezekwa kwa bati badala ya nyasi mlango wa bati/mbao badala ya gunia au kipande cha khanga/kitenge).
Kukiwa na watu Elfu kumi watakao jenga vyoo 2 kila mmoja watu hawajastarehe jamani? (usishangae kunya kwenye choo safi bila hofu ya kuchunguliwa ni starehe).
Ikiwa umerudishwa ghafla basi tumia elimu yako au uzoefu wako kuelimisha wabongo wenzio, Mfano utakuwa unajua jinsi ya kujibana(save) kile kidogo upatacho, ukielimisha watu kwa kujitolea tu, huoni kuwa utakuwa umefanya jambo?
Hivi kwanza tunaongelea nini hapa?
@Dinah!
Kweli kabisa ulichosema. Tatizo, wengi wetu tunasubiri kuanza na jambo kubwa, kitu ambacho mtu unaweza kujikatisha tamaa ,pale utakapo shindwa kufikia malengo .
Post a Comment