Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nakupenda KWA HARUFU YAKO ya KIKWAPA, pamoja na HARUFU ya PILAU kunizingu Wakati wa EID HII!

>> Friday, October 12, 2007

NAWATAKIA HERI YA EID WAISLAMU WOTE na Wadau wote wa BLOGU HII!


Ngoja nikuzingue kwa nyepesi nyepesi basi.........

Wakati huu wa EID , ni rahisi pua kunusa harufu nzuri za mapochopocho.
Kile chakula kizuri kizuri, ndio hutawala majumbani na kikichelewa kuiva, unaweza kushiba kwa harufu tu!

Lakini ningependa kukukumbusha harufu binadamu azitoazo , ambazo ni vigumu kuzinusa wakati huu wa EID , ingawa zipo.

Kazi ya Proffesor Winston, ichambuayo machale ya binadamu(HUMAN INSTINCT) inagusia mpaka jinsi hata umpendaye wakati huu wa EID ,upendo wako unaweza ukawa umesababishwa na anavyo nukia kiasili(Bila Perfumes).Unaweza ukawa unamzimia baada ya kunusa harufu ya kikwapa chake.


Napenda kukukumbusha kuwa kikwapa hutoa aina mbili za harufu zinukiazo kama chakula. Kama unabisha , soma hapa usikie jamaa aliyefanya kauchambuzi.

Kumbuka pia , wanawake wapendao wanaume na wanaume wasenge ,huvutiwa na harufu sawa za homani za ngono. Ila wataalamu hawa bado hawajagundua wanawake wasagaji wanavutiwa na harufu gani.

Si basi ujisomee hapa mwenyewe wakati unasubiri pilau la EID?

Ningependa kugusia mpaka maswala ya jinsi ya kugeuza harufu ya kikwapa iwe harufu nzuri, harufu za uvundo za sehemu za faragha au zile harufu zipatikanazo katika sehemu za faragha mara nyingine zinukiazo kama samaki, lakini najua tunasherehekea EID, kwa hiyo nafikiri niache hilo kwa sasa:-(

Lakini usitishike, harufu asilimia kubwa zitokazo kwa binadamu , zinanukia vizuri puani mwa binadamu na zinamaana nzuri kwa binadamu. Tunazistukia harufu tuziitazo mbaya kwa sababu ni chache na ni rahisi kuzistukia.

DUH!

TURUDI kwenye EID basi.............!

NAWATAKIENI wote msherehekeao EID, harufu NZURI za MAPOCHOPOCHO hapo mlipo!

DONDOO:

  • Tukumbuke tu na kutowasahau wengi ambao watalala njaa katika EID hii, kutokana na kukosa chakula. :-(


Duh!

Naacha kukuzingua basi!:-)


Ngoja nirudi anga fulani za miziki. Kwa bahati bado MAXI PRIEST yuko kichwani.....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP