Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HIVI ni NANI anapata MADEMU zaidi?

>> Tuesday, October 09, 2007

Kabla sijasema, ngojea nijikumbushe mahesabu ya kubwa kuliko, ndogo kuliko na.....

DEMU= Mwanamke.

Na inawezekana ikawa matumizi ya jina DEMU <UTU wa mwanamke

DUH!

Samahani!
Haya turudi kwenye hoja .........

  • Dunia kama itawaliwavyo na wanaume kwa asilimia kubwa, mtu anaweza kuingia upofu wakutoweza kutazama nguvu za wanawake.

Dunia ionekanayo kirahisi,utastukia...

....Kwenye dini maarufu kama za Kikristo, Kiislamu,mpaka zile akina Babu Shogholo walikuwa wanafuata, kuna ka-sehemu fulani kakubwa ambako mwanamke amepewa, kasehemu kakuwa msikilizaji na sio mtoa hoja.

Mwanamke wa shoka mtoa hoja, katika kumbukumbu nyingi kuanzia zilizoko kwenye maandishi au hata za masimulizi ya mdomo, ni yule anayetengenezwa kama vile alibahatisha nguvu au anatokea kwenye familia iliyoko na nguvu kiasi cha kupenya mpaka katika kiti cha mtoa hoja kwa njia ya kusaidiwa na mfumo uliomzunguka kutokana na familia kujulikana.

Watu weusi hulalamika kuwa , hadithi nyingi zilizo tawala zionyeshayo mapungufu yao, zimetokana nakuandikwa na watu wa rangi tofauti na nyeusi.

Lakini...


Unaweza kusema pia, kutokana na wanaume kuhusika sana na usambazaji na uhifadhi wa stori za mwanamke, ndio maana kuna mambo mengi yamuhusuyo mwanamke dunia imenyimwa kuyajua. Na kwa bahati mbaya wenye kumbukumbu za stori hizo wanazidi kuondoka na kutuachia kazi ya kubunia, ambayo inasaidia kuendeleza mtazamo tulionao hivi sasa, ambao mmoja wapo, ni huu usemao; mwanamke ni msaidizi tu wa mwanamume.

Dondoo:
Nafikiri unakumbuka hata maswala ya sensa za watu , wanawake walikuwa hawa hesabiwi mpaka miaka isiyo mingi iiyopita.

Swali:
  • Hivi demu(jina sahihi mwanamke) gani anapata wanaume zaidi?

  • KWA nini unafikiri MWANAMKE mwenye kujisifia kutembea na wanaume kadhaa wa kadhaa, anaitwa MALAYA katika jamii nyingi duniani, halafu mwanamume atembeaye na wanawake wengi, huonekana mjanja, dume la mbegu, rijali...nk?

  • AU mwanaume atembeaye na wanawake wengi naye ni malaya?

DUH!

Inasemekana mitazamo ya wanawake na wanaume ni tofauti.
Kwa hiyo, ayaonayo mwanamke katika kipengele , yanatofautiana na jinsi mwanaume ayaonavyo katika kipengele hicho hicho.Ukichanganya na jicho lijengwalo na tamaduni mbalimbali kuongeza maluweluwe, basi unaweza kufikiri kuwa maswala ya wanaume na wanawake kama yalivyo sasa katika jamii mbalimbali ndio jinsi yanavyotakiwa kuwa.


Lakini...

Pamoja na yote ambayo kwa asilimia kubwa naamini kuwa mimi na wewe hatuyajui kwa asilimia za kutosha, tutakubaliana angalau kwa machache kuwa ..
  • Mahusiano kati ya wanawake na wanaume bado siyo murwa
Ingawaa...
  • Wanawake na wanaume wanahitajiana hapa duniani.
Bado kuna vita ya kijinsia , ambayo inaendelea , kutokana na mwanaume anayetawala kung'ang'ania kiti cha utawala ,wakati mwanamke kachoshwa na kutawaliwa,....

.... halafu na yule mwanamke aliyefanikiwa kutawala kutumia nguvu zaidi kushikilia kiti cha utawala, kutokana na mwanamume kukuzwa katika mazingira yamtengenezeayo saikolojia ya kudhani yeye ndio apaswaye kutawala.


Swali:
  • Hivi unafikiri ni kweli wanawake na wanaume wanatakiwa wawe na usawa?
  • Usawa nini?
Ni rahisi kuongelea tofauti,....
..... kutokana na kujua tofauti za kimaumbile, kisaikoloji, kifikira, kikusikia utamu, kinyume cha kuhisi utamu naki ........nk ; kati ya wanawake na wanaume.

Ni rahisi kuruka baadhi ya mambo ambayo yanaleta usawa kati ya wanawake na wanaume, kimaumbile, kisaikoloji, kifikira , kiakili,kikusikia utamu, kinyume cha kusikia utamu naki.......nk.

Swali:
  • Ushawahi kukutana na wanaume wawili walio sawa?
  • Ushawahi kukutana na wanawake wawili walio sawa?
  • Usawa ni nini?

Naamini, kama jamii haina hata tafsiri moja inayokubalika na wote ya usawa, hii jamii mpaka kesho ya kizazi cha mwisho, itakuwa inajadili haki ziambatanazo na usawa kati ya jinsia hizi mbili zenye sehemu za siri zisizofanana.

Ukiingia katika kudai haki za usawa wa wanaume wajisikiao kuwa ni wanawake na wanawake wajisikiao kuwa ni wanaume kutokana na kemikali za mwilini, hapo ndio kasheshe!

DONDOO:
  • Unakumbuka kujisikia kwako kuwa ni mwanamke au mwanaume ni mchezo wa kemikali mwilini mwako zikuzinguazo mpaka siku nyingine unaamini maswala ya ajabu ajabu kama vile kupenda, kuchukia,njaa, uchoyo ...nk?

  • Kamchezo kakemikali kakibadilika , si unakumbuka, dume zima utaota MATITI?
Halafu na haya maswala ya sayansi, ambayo yanaweza kukubadili kidude,....

....... usishangae kujua kuwa yule Demu umzimiaye, juzi alikuwa MWANAUME, na yule Mwanaume uliyempenda baada ya kuona picha yake kwenye gazeti, bado anasehemu za faragha za kike , mpaka akipata mshahara wa kumalizia operesheni yakumwekea kidude mwezi ujao .

DUH!

KUMBUKA MAMA ZETU WAZAZI NI WANAWAKE!

  • Naamini wote tunahusika katika kuhakikisha haki za watu wote zinaheshimika.

  • Naamini kuwa, wanawake bado wako na mapambano zaidi ya wanaume katika kudai haki zao za angalau kutoa hoja na kusikika.
  • Naamini unayesoma hapa , utajaribu kustukia na kusawazisha pale ugunduapo, mimi na wewe tunachangia kuongezea tatizo na sio utatuzi wa tatizo.

Ngojea nijaribu kuacha!

Lakini ngojea tupewe shule kidogo tena na Ahmed Deedat ......



Tuendelee na utani ambao unamgusa Warren Jeff , nabii wa WAMORMONI katika jambo lisilo utani lihusianalo na janja yetu WANAUME ya kupata KALE KAKITU mara kadhaa zaidi ya WANAWAKE.






Naacha basi DUH!

Burudika na Blues(halisi na sio ile ya disco la...) kama ipigwavyo na MUDDY WATERS

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

KKMie 4:02 pm  

Demu sio jina sahihi kwa wanawake, inasikitisha tumeliacha na limezoeleka midomoni mwenu wanaume.

Kutokana na Utamaduni au mila na desturi ktk jamii nyingi Duniani mwanamke kutembea na wanaume wengi ni kutojiheshimu na kujithamni.

Vilevile kutokana na maumbile yetu wanawake na tendo zima la kutembea (ngonoana) ni wazi kuwa utakuwa umemwagiwa "uchafu" na wanaume hao wote hali inayoweza kusababisha mkanganyiko wa viasilia na hivyo kuibuka na gonjwa kama Saratani au mengine ya kike........umewahi kusikia magonjwa ya kike wewe?

Wanaume maumbile yenu hayabadiliki na vilevile sio rahisi kupokea na kutunza "uchafu" kutokana na umbo la nanihii.

Manii ni uchafu ikiwa unapokea kwa mtu ambae sio mpenzi wako a.k.a hit & run.

Usawa unamaani zaidi ya moja, nafikiri inategemea unazungumzia kona gani.

Mf:- Usawa ktk mahusiano ya kima penzi ni kushirikiana ktk maamuzi, Uchumi, kusaidiana ktk shughuli mbalimbali za kuendesha nyumba n.k.

Elimu-Wote kupewa "pass" kutokana na uwezo wetu sio kupewa Grade maalumu (ya chini) kwa vile tu wewe ni mwanamke (kwamba huna uwezo kama mwanaume).

Uongozi-Kupewa cheo kutokana na uwezo au uzoefu wako, sio kubaniwa kwa vile tu ni mwanamke na huwezi kufanya maamuzi makubwa.

Ila inasikitisha kuwa wanawake usawa huu wanauchukulia vingine kabisa. Mwanamke sasa kapoteza thamani yake kama mwanamke na ile haiba haipo tena.

Wanawake wamekuwa na viburi bin visasi. Na-miss when women were women & men were men sio karne hii Doh!

Inasikitisha.

KKMie 4:05 pm  

Kutokana na Utamaduni au mila na desturi ktk jamii nyingi Duniani mwanamke kutembea na wanaume wengi ni kutojiheshimu na kutojithamni.**

Simon Kitururu 4:28 pm  

@Dinah!: Ni kweli kutokana na mila na desturi nyingi , hii sio kujiheshimu.

Lakini huwa najiuliza tu, isije ikawa ni wanaume walioko nyuma za hizi mila na desturi waliosababisha, hili swala lichukuliwe hivi na jamii.

Kuhusu kujua magonjwa ya wanawake, mimi nayajua kijuu juu tu. Unajua mila na desturi zetu wengine zilifanya huwezi kuona hata chupi ya mwanadada imeanikwa sehemu. Nachojua kutokana na uzoefu fulani, ni kwamba wanawake ni rahisi sana kupata magonjwa katika sehemu za faragha kuliko wanaume. Na wanawake karibu wote niliowahi kuwa na uhusiano nao, ni makini sana kwenda kuchunguzwa mara kwa mara kwa daktari , ili kuondoa uwezekano wa kustukia too late kuwa kunakaugonjwa kama saratani kameanza.

Nakubaliana na wewe kuwa , katika swala la usawa kati ya wanaume na wanawake , kunasehemu tumelemea kushoto. Mpaka neno usawa ni vigumu kwa wengi kulielewa siku hizi.


Pia nakubaliana na wewe hili neno Demu (kama lilitumikavyo kiswahili), linashusha thamani ya neno Mwanamke.
Mwanamke si Demu.

Lakini nafikiri hili neno (DEMU)lilitoka kwenye kiingereza DAME . Na dame ya kiingereza inatafsiri nzuri tu.

Hapo ndipo utakapo choka na mchezo wa lugha! Neno hilo hilo likitamkwa kwa lugha nyingine limeweza kubadili uzito wa jambo.

Unajua ninaweza kumuambia mwanamke yeyote kwa kiingereza ``I love U´´kirahisi, kwa sababu, kwa kiingereza sentensi hiyo kwangu haina uzito. Ni kama tu kuomba chai.

Lakini, nikisema kwa kiswahili kuwa, ``NAKUPENDA!´´ jasho litanitoka kutokana na uzito naoipa sentensi hiyo.


Asante Dinah kwa kunipa shavu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP