Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SWALA LA MUAFRIKA KUOA MZUNGU!

>> Sunday, October 28, 2007

Swali:

  • Kuoa au kuolewa maana yake ni nini?
  • Ushastukia kuwa mtu umlengaye nitofauti na wewe?(Ukiwa wewe ni mwanamke, unaweza ukawa unamlenga mwanaume.)
  • Muafrika ni tofauti na Mchina au haya ni maneno tu?

Kuoa au kuolewa ni jambo la ajabu sana binadamu mwenye akili alifanikiwa kugundua.

Katika kuheshimu ndoa na kufanya yote jamii ikubaliyo kuwa yanaruhusiwa ndani ya ndoa, binadamu akagundua kuachana na kuachika hata kama wengine nje ya chumba hatustukii swala.

Staili ya kuacha au kuachika,(hapa na maanisha ifikiapo mpenzi kageuka mshea chumba kama unaaibu ya kukikimbia chumba) ni noma. Kwa sababu maana yake ni kutukana ile fikira uliyokuwa nayo wakati unataka kuoa au kuolewa kwa kisingizio umempenda kweli nanihino na unataka uishinaye milele.

Nakubali kuwa unaweza ukawa umeoa au kuolewa kwa sababu nyingine na sio kuwa unapenda harufu ya kikwapa ya mpenzi.


Ndoa kitu kizuri, inatunzika tu vizuri kama kikojozi awezavyo kutuza siri ya godoro alilokojolea.
Ndoa inatamanika sana tu kama walioko ndani ya ndoa wamtamanivyo kisiri hausigeli/hausiboi bomba wa nyumba ya jirani(ikiwa wa ndani havutii)

DUH!
Ngojea niache utani!(hivi unafikiri natania?)

Naamini ndoa nyingi na jamiii nyingi zihusishazo jamaa waliofunga ndoa, huendeshwa kwa janja ya mwanaume iliyo jificha ndani ya dini, mila desturi, ndani ya suruali na.......

DUH!

Hebu msikilize tena Harry Enfield akitania kuhusu baadhi ya mitazamo ya wanauume juu ya wasionauume....


DUH!

Napenda hadithi za ndoa kwasababu nyingi zimekaa kinamna ya kwamba aliyeoa au kuolewa na Mchina anajifanya hakustukia kuwa inabidi ajifunze kula kwa vijiti mara nyingine kama sio zote.

Halafu hadithi nyingine za ndoa, ni zile jamaa ajifanyapo hakustukia kuwa kwa kuoa au kuolewa hakujiingiza tu kwa mtu mmoja bila familia au jamii yake ambayo daima hukumbuka kuwa yeye ni wakuja tu hapo chobosi ya mjanja aliyemdaka.( ingawa kisiri anajua kuwa ni yeye kadakwa)

DUH!

Swali:
  • Unaposema unaheshimu ndoa yako, inamana unajinyima nini vile?
DUH!

Samahani naacha basi!
Siunajua niko mawazoni tu?
Nisamehe basi!
AU?

Lakini...

.......Naamini wewe kama Muafrika au Mgagagigikoko, umeoa au kuolewa na Mzungu, Mtanzania, Kibaka, Zeruzeru, Mweusi tiii, Muarabu fulani au yule ambaye uzuri wake unaonekana vizuri mpaka mkisogeleana umbali sifuri, ujue tu umeoa au kuolewa na haka kamchezo ni kaubunifu ka kidunia tu.

Naamini kama mbinguni ni kuzuri kama baadhi ya vitabu (biblia na...) vya ujanja uwakilishwavyo utundu uitwao dini vituambiavyo, sidhani kama kutakuwa na msamiati uitwao ndoa hapo HEVENI.
AU?

Swali:
  • Hivi si unakumbuka hisia za binadamu hutengenezwa na mchanganyiko wa kemikali tu mwilini mwa binadamu?

  • Halafu si unakumbuka ni mjanja fulani tu aliyetuambia TELEVISHENI kwa kiswahili inaitwa LUNINGA?

DUH!

Ngoja niache basi,Nisije kukosa mke bure!

Nawatakia maisha ya kutafuta au kuwa ndani ya ndoa mema!

Tulia na Samim akija na Heater

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Egidio Ndabagoye 8:05 am  

Sio Muhindi?

Pamoja.

Simon Kitururu 6:43 pm  

@Egdio:Wahindi ni baabu kubwa! Si unaona mpaka Miss Tanzania ni Muhindi?
Vipi , umejipatia mmoja hapo India?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP