Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo mawazoni; CAMPUS CEO na Stan O'Neal.

>> Monday, November 05, 2007


Kama ni mwanafunzi na unapenda biashara na ujasirimali, na una nafasi ya kupata kitabu cha Randal Pinkett Campus CEO ningekushauri ukisome.
Ni kitabu kizuri kwa mtu mwenye ndoto na anania ya kuzifuatilia.Mimi binafsi nimekipenda sana.



PICHANI ni Dr Randal Pinkett









Mcheki kidogo Dr Pinkett akiongelea Campus CEO

Mawazoni yuko bado Stan O'Neal aliyekuwa bosi wa Merill Lynch.

Huyu jamaa ni miongoni mwa watu walioko katika fani ninaowaheshimu na kuwafuatilia maswala yao ya kikazi kwa muda. Katika miaka kadhaa yakumfuatilia sikuwahi kusikia akizungumziwa sana kama Mtu mweusi hasa mambo yalipo kuwa yanakwenda vizuri. Matatizo yalipoanza tu kuikumba Merill lynch chini ya uongozi wake ,nikastukia kuwa kila aguswapo lazima na rangi yake ikumbukwe katika seko zangu za mihangaiko.

Nachojaribu kusema ni kwamba, kama wewe ni mtu mweusi kama STAN, unaweza kuchekewa kirahisi na rangi yako kuwa sio tatizo kama maswala yako shwari. Lakini mambo yakiharibika, anga kibao mpaka za watu weusi wenzako huanza kukumbuka weusi wako.

Nisikufiche, kuna anga kibao ambazo ni mweusi anaongoza kwa kumstukia mweusi mwenzie kuwa hawezi dili pamoja na kuwa ni kawaida kulaumu wengine kwa kubagua weusi.




















PICHANI ni Stan O´Neal

Tukumbuke tu kuwa mimi wewe na yule , kama ni mweusi , bado dunia fulani inatulenga kama watu wasioweza.

Kumbuka hilo wakati unaendeleza libeneke !



Sikiliaza kidogo baadhi ya maoni kuhusu kuonekana mweusi


Basi ngoja nikurudishe kwa Mzee wa Nigeria STEREO MAN akikupa kibao E Dey Pain Me.
SIKU NJEMA!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

ombui 8:13 am  

Ni kweli hakuna kizuizi kuwa tajiri ukiwa kwenye chuo. Labda tishio ni jinsi ya kutumia muda and mapato ya kuekeza.

Nakala nzuri hii...nitaanzisha biashara...nitakupa faida....haha

Simon Kitururu 11:06 am  

@Kisiki:Si rahisi sana lakini, ingawa inawezekana:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP