Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MHESHIMIWA unataka AONGEE nini , AKISHA KUDANGANYA?

>> Thursday, November 08, 2007

Uongo wa Mheshimiwa unastarehe zake!

Mheshimiwa akidanganya, ingawa umestukia, ukiropoka ni wewe unaonekana huna heshima.
Mheshimiwa wakati anakudanganya ni rahisi kuwa anafaidika na wewe kudanganyika.

Mtu fulani asiye julikana katika maeneo ya ulaji kama Mheshimiwa, mara nyingi anadanganya akijitetea.

Lakini...

.....mwanamme fulani anaweza kutafsiri mdanganyo afanyao, kuwa ni mtongozo.

.... mwanamke fulani anaweza kutafsiri mdanganyo afanyao kuwa ni.... duh! sijui!

Swali:

  • Hivi ushawahi kuogopa kumuambia ukweli mpenzi mtarajiwa, kuwa unamhitaji kwa faragha ya ngono tu na sio kwa mahusiano ya mke na mme?
Nahisi Mheshimiwa ni neno danganyifu usipoangalia!Unaweza ukawa unamuogopa mtu na sio kumheshimu. Inawezekana hujui tu kitu fulani ambacho unafikiri yule anajua ndio maana unadai unamheshimu.

Swali:
  • Hivi Mheshimiwa ni nani?
  • Unafikiri ni kwanini unadai unamheshimu yule?
DUH!

SIKU Njema!

INCUBUS wanakupa kibao Drive

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Christian Bwaya 2:26 pm  

Maswali mazuri.

Binafsi, pasipo kutafsiri maana ya uheshimiwa wenyewe, nafikiri ni vyema kuwafahamu watu kijuu juu ili kuwapa heshima zao (wanazostahili na wasizostahili).

Tunapomfahamu mtu kwa kina kunatufanya tumpunguzie uheshimiwa wake.

Kwa sababu kumfahamu kunamaanisha kuujua upungufu wake kitu amabcho ni hatari katika dhana ya uheshimiwa katika mipaka ya tafsiri yangu.

Simon Kitururu 5:57 am  

@Bwaya: DUH!Sikupingi katika hilo.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP