Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nakutaka wewe!

>> Saturday, November 03, 2007

Nakutaka, ni starehe kwasababu ipo sikutaki au nimekuchoka weye!
AU?

DUH!

Swali:

  • Ushastukia kuwa baadhi ya binadamu huwa wanawataka wenzao?
Kutaka kitu ni dalili ya kupungukiwa.
Kutaka mara nyingi ni hisia tu !

Ubingwa wa kutaka hauna nukta.
Unaweza ukataka mpaka siku ya kufa.
Unaweza kuanza kwa kutaka gari likusaidie katika usafiri.
Ukilipata gari fulani , unahamia katika kutaka Benzi.

Kisa kikufanyacho uamini kuwa benzi ni tofauti na Corolla, ni kamchezo ka akili za binadamu ambako kajinga mara nyingine.
Ndio maana binadamu huyo huyo, karibu katika lugha zote, ana neno liwakilishalo ujinga.

Swali:
  • Hivi nyumbu na lada si yote ni magari?
Lakini ....

Unaweza kutaka kwa sababu wenzako wanataka hicho kitumbua!
Inamaana unaweza ukafikiri unataka hata kama ukweli ni kwamba hutaki.

DUH!
Endeleza wikiendi njema!
Mimi naacha basi!
Lakini ukiweza kasikilize haka kawimbo ka SIMPLY RED

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Christian Bwaya 6:07 pm  

Maswali yako yananifikirisha sana. Tuko pamoja kamanda.

Simon Kitururu 8:24 pm  

@Bwaya: Mkuu umepotea lakini kwa muda!Tuko Pamoja!

KKMie 2:12 pm  

Kweli kabisa sote tunataka kila siku na kutaka huko hakuishi mpaka siku utakayotoweka Duniani (kufa).

Hii "kutaka" inasababishwa na tamaa au kutoridhika au kiu ya kurahisisha mambo fulani ktk maisha yako.

Ila ikumbukwe tu kuwa kutaka sio lazima upate, hii ni kutokana na uwezo wako mdogo wa kumudu kile unachokitaka au kuwa na mapungufu fulani ambayo yatasababisha wewe kukosa kile unachokitaka.

Imetulia!

Simon Kitururu 2:43 pm  

@Dinah:Nakubali kabisa ulichosema!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP