Ushamchukia mwalimu mpaka ukaamua ukamuue?
>> Friday, November 09, 2007
Katika nchi ambayo ni rahisi kupata kibali cha bunduki zaidi ya cha gari, nafikiri hili tendo lilikuwa linasubiri tu kutokea.
Baada ya kumchukia mwalimu mkuu wake, mwanafunzi mmoja aliamua kwenda kumpiga risasi mwalimu huyo katika mitaa ya Jokela , Finland .
Baada ya kumpiga risasi mwalimu, akaamua kuwapiga risasi baadhi ya wanafunzi aliokutana nao kiholela kabla ya kujipiga risasi mwenyewe.
Inasikitisha sana jinsi wanadamu tunavyofikia kuua kama suluhisho.
Inatisha , ukifikiria kuwa kuna watu wanaweza kukuua bila sababu wakiwa katikati ya kuhangaika na matatizo yao.
Cha ajabu ni jinsi tuondokapo nyumbani , tunakuwa na aina fulani ya kujiamini kuwa tutarudi nyumbani baada ya shughuli.
Ukisoma jinsi watu wanavyo kwenda kulipua watu bila ya kuwafahamu kwa visingizio vya dini , siasa au hata mambo binafsi siku hizi hapa duniani, unaweza kuogopa kwenda sehemu yoyote.
INATISHA!
Soma zaidi hii habari
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Watu hawa wanahitaji msaada wa matibabu au ushauri. Unajua baadhi yetu hatujui jinsi ya kukabiliana na matatizo na mahangaiko ya maish ayetu yakila siku na hali hiyo hupelekea stress ambayo inaweza kuzaa depression etc.
Vilevile kuna watu wachache ambao huzaliwa na mapungufu fulani akilini/kichwani ambayo baadae hutambuliwa kama aina fulani ya depression...mara nyingi watu hawa huwa hawajijui na hujaribu kutafuta namna ya kuishi kama watu wengine lakini wanashindwa hali ilizidi kuwa mbaya basi suluhisho kwao ni kifo (kuua au kujiua wenyewe).
Alafu kuna wale ambao wanapandikizwa imani fulanina hivyo kudhani njia pekee yakumuona Mungu au kupumzisha matatizo yako ni kuua na kujiua mwenyewe hapo ndio tunapata akina "kujitoa mhanga".
Badala ya kulaumu ni vema kujifunza nakuzuia hilo lisitokee tena. Kufanya kampeni za watu kutoonea aibu matatizo ya akili.....kama unakuwa stressed mara kwa mara sema usaidiwe, kama una-depression weka wazi kwa wazazi, walimu, boss wako ili wajue jinsi ya ku-deal na wewe na hatimae kupata tiba ya kukabiliana na hali hiyo.
Inasikitisha sana.
@Dinah: Ulichosema skipingi hata kiduchu. Inasikitisha. Naombea walio na stress fulani wawe wamekusoma.
Dinah umesema kweli.
Mtu kufikia kuchukua hatua kali kama hizi, maana yake kuna hitilafu mahala fulani, si bure.
Habari hii ni changamoto kwa wenye watoto na jamii kwa ujumla wake. Tuangalie namna ya kuepusha mambo kama haya tangu mtoto anapokuwa tumboni.
Post a Comment