Nimebanwa kinamna, ingawa ndani ya kubanwa, mida mida nilifanikiwa kukutana na ... na kuliwazwa na ......
DUH!
Kabla sijakutonya ... Twende JAPAN tumsikilize PUSHIM
akikupa THE RACE OF LOVE
Sasaaaaaaaaaaaaa......
Pata ambao wako nami ingawa sija.....
Kutoka CUBA GRUPO SON CON SON na Cuban Ambassador
DUH!
Pumzika basi!
AU!
Ngojea basi SAIDA KAROLI atuleteee...
DUH! Tuendeleee..... ,,,,.... na Wadau ambao pamoja na kushindwa kwangu kuandiaka mawazo wame.....
Ronaldo , Mzee wa London Mkuu wa Kikao aka Raymond Byamungu EEH! DUH! Original WAX Mtimkubwa aka Fidelis na anayejisogeza:-) Erick aka PRODUCER Wax na CHE Edo Mghosi! Avae urewedi!:-) Hi aho!:-) Du ndugu yangu nahitaji shule kidogo kabla sija piga forighoko!:)
Katika nchi ambayo ni rahisi kupata kibali cha bunduki zaidi ya cha gari, nafikiri hili tendo lilikuwa linasubiri tu kutokea.
Baada ya kumchukia mwalimu mkuu wake, mwanafunzi mmoja aliamua kwenda kumpiga risasi mwalimu huyo katika mitaa ya Jokela , Finland .
Baada ya kumpiga risasi mwalimu, akaamua kuwapiga risasi baadhi ya wanafunzi aliokutana nao kiholela kabla ya kujipiga risasi mwenyewe.
Inasikitisha sana jinsi wanadamu tunavyofikia kuua kama suluhisho. Inatisha , ukifikiria kuwa kuna watu wanaweza kukuua bila sababu wakiwa katikati ya kuhangaika na matatizo yao.
Cha ajabu ni jinsi tuondokapo nyumbani , tunakuwa na aina fulani ya kujiamini kuwa tutarudi nyumbani baada ya shughuli.
Ukisoma jinsi watu wanavyo kwenda kulipua watu bila ya kuwafahamu kwa visingizio vya dini , siasa au hata mambo binafsi siku hizi hapa duniani, unaweza kuogopa kwenda sehemu yoyote. INATISHA! Soma zaidi hii habari
Mheshimiwa akidanganya, ingawa umestukia, ukiropoka ni wewe unaonekana huna heshima. Mheshimiwa wakati anakudanganya ni rahisi kuwa anafaidika na wewe kudanganyika.
Mtu fulani asiye julikana katika maeneo ya ulaji kama Mheshimiwa, mara nyingi anadanganya akijitetea.
Lakini...
.....mwanamme fulani anaweza kutafsiri mdanganyo afanyao, kuwa ni mtongozo.
.... mwanamke fulani anaweza kutafsiri mdanganyo afanyao kuwa ni.... duh! sijui!
Swali:
Hivi ushawahi kuogopa kumuambia ukweli mpenzi mtarajiwa, kuwa unamhitaji kwa faragha ya ngono tu na sio kwa mahusiano ya mke na mme?
Nahisi Mheshimiwa ni neno danganyifu usipoangalia!Unaweza ukawa unamuogopa mtu na sio kumheshimu. Inawezekana hujui tu kitu fulani ambacho unafikiri yule anajua ndio maana unadai unamheshimu.
Kuna vitu fulani hata kama una shida nivigumu kujisitiri navyo.
Swali:
Kwanini?
DUH!
Samahani kwa kuandika neno chupi kwenye tako(samahani ! Kichwa) la habari hapo juu .
Naamini ghafla tu, inawezekana umekumbuka kisitiri faragha zaidi ya kitu ninachojaribu kukilazimisha uamini nakiongelea hapa, ambacho ni kitu kile ukisaminicho na kukiamini mpaka kuweza kukiweka karibu nawe ingawa si kipya.
Tukirudi kwenye chupi...
.......Ukisoma biblia utaambiwa kuwa kuna mtundu mmoja alikula tunda fulani ndio akafanikiwa kustukia maeneo.
Lakini ...
.. kuna makabila kadhaa duniani mpaka karne hii bado yalikuwa hayajisitiri kinamna ya kuficha maeneo ya faragha kwasababu yasionekane. Tamaduni kadhaa walistukia kuficha maeneo kwa sababu yasiumie au kuugua kirahisi na sio kwasababu jamaa atachungulia.Hawa jamaa nahisi eva wao hakulila tunda lote , alimega tu.(Ushawahi kucheki baadhi ya makabila ya Papua New Guinea mwaka huu wanavaaje?)
Maeneo fulani naamini ni vizuri tu yafichwe kutokana na yalivyokuwa rahisi kuumia au hata kuugua.
Lakini....
.... tujifanye tu kuwa ni maeneo ya ajabu, ingawa kwa Wafini ,baba na binti hawakawii kwenda sauna pamoja uchi bila kustukia hicho ni kitu cha ajabu kwetu wenye mila zenye heshima.
..tujifanye ni maeneo ya ajabu ndio maana ni noma kuyachungulia.
DUH!
Tukiacha hilo....
...ukiongelea chupi na mtumba, ni rahisi kuoanisha na kitu kikugusacho karibu na sehemu unazo zijali na kikioanishwa na vitu vilivyotumika.
Vitu vilivyotumika si vyote vibaya, ingawa wengi tunapendelea vipya. Lakini vitu vilivyotumika wanalengeshwa masikini zaidi ya wenyenavyo. Kitu ambacho nafikiri ni cha kisaikolojia zaidi ya ukweli wa kwamba kitu kipya kinamnufaisha mtu zaidi ya cha zamani.
Si umecheki...
....wenyenavyo wakinunua mtumba , wanabadili jina na kuita vinteji au majina fulani ili tu chupi hiyo hiyo ya mtumba ionekane kuwa ina thamani zaidi kwa sababu ilikuwa inavaliwa na mtu maarufu.
Saikoloji nyuma ya mtu ajivunaye kwa kuwa ana gari alilo kuwa anaendesha Hitler, ni sawa tu na ile ya ajivuniaye kuwa anauwezo wa kuvaa gwaguro jipya lililo na lebo GUCCI.
Swali:
Chupi ya mtumba isiyo na kiraka iliyooshwa vizuri, inatofauti gani na chupi iitwayo mpya ambayo hata madawa yaliyotumika kuifanya ionekane kama unavyoiona hujui?
Nisikufiche.....
....wengi wetu tunapenda vitu vipya.
Tunavisingizio vingi , kwanini kitu kipya ni bora kuliko cha zamani. Moja ya tupendacho kusema ni kwamba , kitu kipya hakiharibiki mapema.
Lakini....
.... katika dunia ambayo tunajaza matakataka, na ambayo binadamu anajilimbikizia vitu hata asivyo vihitaji, inasikitisha kuwa ujanja ni kuvaa chupi mpya.
DUH!
Naacha!
Pata baadhi ya picha zangu na WADAU kadhaa tena! Hakuna kipya ! Mpaka leo kama wewe ni mdau wa blogu hii ,nafikiri umestukia marafiki zangu nakutananao wapi:-)
Nina matatizo na filmloop, kwa hiyo picha ni kibao kidogo!:-( Msikilize basi Lenny Kravitz akiwa na Jay Z kabla hujajitesa! Wanakupa GUNS N ROSES.
Mtu mmoja pale tu awezapo kufanya idadi ya watu wakutosha wafuate mawazo yake, anaweza akashangaza umati kwa jinsi awezavyo kusababisha umati upendao Bongo Fleva ,upende SINDIMBA.
Swali:
Unakumbuka Ghandi hapo mitaa ya india, alishawahi kusababisha umati wa Wahindi uache kuvaa nguo alizohisi zinafaidisha Waingereza wakati yeye mwenyewe kavaa nepi?(ilikuwa haiitwi nepi lakini:-))
Unaweza kufikiria nini ukienda kwenye mkutano wa kiongozi wako sasa hivi ukamkuta anahutubia huku kavaa nepi?
Idadi ya watu wanaotakiwa kukufuata ili wazo lako lichukuliwe maanani , inategemea na wewe mwenyewe na aina ya wafuasi wako.
Yesu na baadhi ya Masupastaawa baadhi ya dini tuzishabikiazo, walianza na wafuasi wachache.
Akina Fidel Castro , Museveni na .... waliingia msituni na wafuasi wachache.
Yesu , alianza na walalahoi ambao silaha yao ilikuwa imani yao kwake.
Fidel Castro na Museveni , inasemekana ilipobidi walitumia mabavu katika kuhakikisha kuwa wafuasi wao wanabakia wafuasi. Nafikiri unakumbuka stori za jinsi isemekavyo CHE GUEVARA alivyokuwa rahisi kukupiga risasi mtu, akihisi kuwa huaminiki katika jeshi la FIDEL CASTRO.
Swali:
Nyama ya mbwa haina sumu , unahisi kwanini huili au unajivunga kuionja?
Ushastukia watu wanakula nyoka mwenye sumu kwa kujua jinsi ya kuondoa sumu wakati wanaacha nyama ya ng'ombe kwa sababu za maisha ya baada ya kufa?
DUH!
Sasaaa.....
Asili ya mitazamo mingi , ilianzia kwa mtu mmoja. Unaweza kufuatilia mpaka kwa mtu mmoja aliye tamka kwa mara ya kwanza kuwa anahisi dunia ni mduara na sio kama meza.
Mtu atoaye wazo na wafuasi wake katika hilo, wanaweza wakawa na nguvu au wasiwe na nguvu kutokana na wachukuliwavyo katika jamii.
Mtu aaminiwaye katika jamii , ni rahisi ushauri wake kuwa; watu wale nyama za mbwa koko mtaani ili kupunguza mbwa wazururao , ukachukuliwa uzito kuliko mdau jamii impuuzayo akisema kuwa sababu kubwa ya siasa mbovu Africa ni pamoja na uwepo wa tabaka litawalao ambalo limejaa watu waheshimiwao katika jamii lakini hawana dira ya wapi waelekeze nchi zao, kwa hiyo mpaka tabaka hili litakapo pata kuwa na wengi wanye uchungu wa kweli , ndio itakuwa mwisho wa kupiga makitaimu kimaendeleo.
DUH!
Mtu bila watu , mchango wa mtu unakuwa mdogo sana katika jamii. Hata katika kuijanza jamii, mtu huhitaji angalau mtu mwingine wamimbishane ili azaliwe mwingine kuongezea kaidadi ka watu duniani.
Lakini......
Tusisahau mchango wa mtu mmoja, kwani ndio kiini halisi cha swala. Naamini inawezekana ikawa ni wewe mwenye wazo ambalo ndio utatuzi wa matatizo fulani yatuzungukayo.
Naamini hakuna mtu au wazo moja litakalo kuwa jawabu ya yote.
Hata Yesu na watu wengine fulani, bado mpaka leo mawazo yao hayakukubalika na wote. Kumbuka kuwa hawa ni ambao wanahusianishwa na Mungu katika hoja zao na bado watu wanawastukia maeneo maeneo.
Hivyo... ..... Uwezo wa mtu wakawaida na hoja zake binafsi kukubalika unatakiwa kulenga maeneo yaguasayo udhaifu uliopo katika jamiii.
Swali:
Hivi unafikiri ni kwanini masikini wengi hawacharuki kirahisi katika nchi masikini wakati wanashuhudia wachache wakifaidi matunda ya jasho au udhaifu wao?
Naamini mpaka dunia itakapokufa baada ya jua kufa, bado hakutakuwa na mtu au kitu kimoja kilicho kubalika na wote.
Lakini...
... pamoja na kwamba wazo lako nitalikataa, bado ni wazo zuri likiwa lina jenga jamii na kupunguza machungu yaigusayo jamii. Wazo lako linaweza likaoneka na la ajabu kutokana tu na kuwalenga watu walioko na kujengwa kifikra na mifumo ambayo inasababisha mawazo ya ajabu ya wengine yashamiri na kuifanya dunia kuwa ya ajabu kama uionavyo hivi leo.
Mfumo ambao unaruhusu baadhi ya mawazo yasikike na kufuatwa zaidi kuliko mengine ndio unao sababisha mtu kama George Bush , Marekani na hata Kikwete Tanzania, waweze kuwa ni watu tuwasikilizao na watuongozao kuliko wale ambao kwa mtazamo flani wangeweza kuwa ndio viongozi ambao wangekuwa wanatuongoza sasa hivi kama mfumo huu haungekuwepo.
Swali:
Kama mfumo huu uendeshao dunia leo hii ni mbaya sana, unahisi ni kwanini umeshamiri namna hii?
Kama CCM ni mbaya kwa Tanzania, unafikiri ni kwanini bado wajanja hawajitengi nacho?
DUH!
Lakini....
.......naamini kuwa mawazo mengi watu tufikiriayo kuwa ni mapya, ni mawazo ambayo mtu mwingine alishawahi kuyawaza na kutoyafanyia kazi.Tatizo ni kwamba mara nyingine wazo lako wewe ni zuri lakini kunamtu mwingine ndio yuko katika nafasi ya kuweza kulifanyia kazi. Tatizo ni kwamba , ni vigumu kwetu wengi kukubali utoe wao kwa ajili ya wengine kufaidika kama tunahisi sisi hatutafaidika na wazo hilo tuchangialo. Ni vigumu kushauri watu wale mbwa mtaani kwao kama mimi huku minofu haitanifikia.
Cha ajabu ... ...karibu sisi wote naamini tunachangia sana kibinafsi kukwamisha jamii kwa kutochangia kwetu angalau kimawazo katika matatuzi ya magumu yaigusayo jamii.Naamini hata mawazo yetu tukiyaweka wazi, kuna mwingine anaweza kufaidikanayo hapo baadaye kwa kuyafanyia kazi au hata kuyakarabati kama akina Nyererewalivyofanya.
Swali:
Unahisi unawafuasi?
Watoto wako au hata ndugu, wale wadogo uwanunuliao peremende bado hawakufuati na mawazo yako?
DUH!
Naacha! Mawazo mengine hayafai kuandika haraka haraka, nisije nikajipoteza bure na wafuasi wangu!
DUH!
Tulia na Mtu mmoja aitwaye Savion Glover atuonyeshe mchango wake katika sanaa ya TAP DANCE
Nahisi ni muachie tu na SAMMY DAVIES JR ,andeleze kutuonyesha TAP DANCE
Kama ni mwanafunzi na unapenda biashara na ujasirimali, na una nafasi ya kupata kitabu chaRandal PinkettCampus CEO ningekushauri ukisome. Ni kitabu kizuri kwa mtu mwenye ndoto na anania ya kuzifuatilia.Mimi binafsi nimekipenda sana.
PICHANI ni Dr Randal Pinkett
Mcheki kidogo Dr Pinkett akiongelea Campus CEO
Mawazoni yuko bado Stan O'Neal aliyekuwa bosi wa Merill Lynch.
Huyu jamaa ni miongoni mwa watu walioko katika fani ninaowaheshimu na kuwafuatilia maswala yao ya kikazi kwa muda. Katika miaka kadhaa yakumfuatilia sikuwahi kusikia akizungumziwa sana kama Mtu mweusi hasa mambo yalipo kuwa yanakwenda vizuri. Matatizo yalipoanza tu kuikumba Merill lynch chini ya uongozi wake ,nikastukia kuwa kila aguswapo lazima na rangi yake ikumbukwe katika seko zangu za mihangaiko.
Nachojaribu kusema ni kwamba, kama wewe ni mtu mweusi kama STAN, unaweza kuchekewa kirahisi na rangi yako kuwa sio tatizo kama maswala yako shwari. Lakini mambo yakiharibika, anga kibao mpaka za watu weusi wenzako huanza kukumbuka weusi wako.
Nisikufiche, kuna anga kibao ambazo ni mweusi anaongoza kwa kumstukia mweusi mwenzie kuwa hawezi dili pamoja na kuwa ni kawaida kulaumu wengine kwa kubagua weusi.
PICHANI ni Stan O´Neal
Tukumbuke tu kuwa mimi wewe na yule , kama ni mweusi , bado dunia fulani inatulenga kama watu wasioweza.
Kumbuka hilo wakati unaendeleza libeneke !
Sikiliaza kidogo baadhi ya maoni kuhusu kuonekana mweusi
Basi ngoja nikurudishe kwa Mzee wa NigeriaSTEREO MAN akikupa kibao E Dey Pain Me. SIKU NJEMA!
Nakutaka, ni starehe kwasababu ipo sikutaki au nimekuchoka weye! AU?
DUH!
Swali:
Ushastukia kuwa baadhi ya binadamu huwa wanawataka wenzao?
Kutaka kitu ni dalili ya kupungukiwa. Kutaka mara nyingi ni hisia tu !
Ubingwa wa kutaka hauna nukta. Unaweza ukataka mpaka siku ya kufa. Unaweza kuanza kwa kutaka gari likusaidie katika usafiri. Ukilipata gari fulani , unahamia katika kutaka Benzi.
Kisa kikufanyacho uamini kuwa benzi ni tofauti na Corolla, ni kamchezo ka akili za binadamu ambako kajinga mara nyingine. Ndio maana binadamu huyo huyo, karibu katika lugha zote, ana neno liwakilishalo ujinga.
Swali:
Hivi nyumbu na lada si yote ni magari?
Lakini ....
Unaweza kutaka kwa sababu wenzako wanataka hicho kitumbua! Inamaana unaweza ukafikiri unataka hata kama ukweli ni kwamba hutaki.
DUH! Endeleza wikiendi njema! Mimi naacha basi! Lakini ukiweza kasikilize haka kawimbo ka SIMPLY RED
Katika nyama ya kuku , wengine hupendelea firigisi.
Ila...
......katika tamaduni na mila fulani fulani hatakama unapenda paja ,ukikaribishwa firigisi ni mwiko kuikataa.Chochote ukaribishwacho ni mwiko kukataa angalau kuonja.
Kama mstaarabu, waweza kulazimika kukaa kimya au kusifia pia paja kwa kuepuka kukiri unapendelea firigisi kwa kuogopa kuonekana wewe mtu mbaya.
Uwezo wa mtu kuvumilia asiyopenda kwa kukwepa kuonekana mtu mbaya, ni mkubwa sana. Mtu usipoangalia unaweza kukaishi maisha yako yote unajaribu upendeke.
Hebu msikilize Alpacino akizungumzia Mtu Mbaya ndani ya sinema Scarface.(ONYO:Anatumia lugha mbaya ambayo baadhi wanaweza kutafsiri kana kwamba anatukana)
Naamini , kuogopa kuchukuliwa vibaya kunasababisha ambao wameshachukuliwa vibaya waendelee kunyoshewa vidole kinafiki kuwa ni wabaya na ambao ni wabaya.
Swali:
Kama unapenda firigisi, ni mara ngapi umelazimika kuonja paja?
Uzuri wa swala ni kwamba, paja kama ni chakula, ukishikwa na njaa na kulila hufi. Njaa ikiwa kali nguvu ya uchaguzi hupungua, ukianza kushiba ndio utakumbuka zaidi kuwa wewe ni mtu wa firigisi.