Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA unataka NISICHEKE, usinitekenye kwenye KIDONGOLOSO!

>> Thursday, July 03, 2008

Ukinigusa pale..

........unaamsha huku
Ukiamsha kule
......naanza kustukia maswala ya NINI na KWANINI.

NINI na kwanini, ni maswala ya kujiuliza tu.

NA.....

Nikianza kujiuliza , nitataka kupata majibu.

AU...

Bila shaka nitaanza kutafuta majibu.


Tatizo la majibu ni kwamba, hata MAJIBU ya UONGO ni MAJIBU kwa afikiriaye kapata jibu.

Kwa yoyote MJANJA, usicheze na ufikiriaye mjinga ambaye KASHATEKENYWA na KASTUKIA, na anatafuta MAJIBU kutokana na UJANJA wako.

Akipata jibu , laweza likawa si jibu ulilotegemea!

  • SI wanadai aliyelala USIMUAMSHE?

Naamini AFRIKA imeamka!
Naamini mimi na wewe tuko macho , tumeamka , na tunatafuta jibu!
AU?
Swali:
  • Wewe na mimi tunatafuta jibu la swali gani?
  • Wewe , mimi na yule tunaweza kuwa na swali moja wakati mmoja?

Samahani kama nimekutekenya!
Nawaza tu hapa katika mtiririko fulani!
Kama hunielewi naongelea nini au hutekenyeki; ASANTE kwa ushirikiano!

Siku njema!
-------------------------------------------------------------------------------------
Cheki kidogo mtu awezapo kubabaika akidhani jamii imemfumania..

AU nirudi tu katika Blues nikisaidiwa na JIMI HENDRIX katika kibao Hear My Train A Comin'


AU niwaache LENNY KRAVITZ na ERIC CLAPTON wamkumbuke JIMI HENDRIX kwa kibao All Along The Watchtower

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP