Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SIRI ya WASIKILIZAO nyimbo za dini kwenye DHAMBI au wafanyao dhambi pembeni kidogo ya BIBLIA , KORANI au KILE kitabu fulani kikatazacho NANIHII!

>> Wednesday, July 09, 2008

KILA kitu ni kitu cha kumuogopesha BIN-ADAMU !

Na

MIMI NAOGOPA kufanya dhambi kutokana na kufunzwa na kujifunza ubaya wa dhambi hasa katika kusababisha kuwezesha kwenda kwangu JEHANAMU!

:-(

Tatizo la uoga wa kufanya dhambi ni uwezo wetu binadamu kuzoea vitu hasa kama matokeo ya kucheza na moto huyastukii hapahapo kuwa UMEUNGUA .

UZOEFU wa kuzoea KIPORO cha wali na MAHARAGE ya nazi ya jana, hutufanya kudhani kuwa kwa sababu hatuumwi tumbo, basi KIPORO hakina vijidudu au , bakteria wakichezeacho MDAKO wakati unakigida.


Swali:

  • Kama unapenda maziwa , ushastukia kuwa maziwa yamgando, mtindi au..... ni maziwa yaliyoharibika?
  • Ushawahi kumuogopa MZAZI , au NDUGU akutakiaye mema kwa staili zake za kukufikishia ujumbe?
  • Ushawahi kuogopa kumuambia umpendaye kuwa UMEMZIMIA na kila ukichukua sabuni yako ya MBUNJU kwenda KUOGA ,unamuona kwenye beseni?



Ukifikiria sana, unaweza kukumbuka kuwa kama wewe ni mshirikina, LIBINTI au LIMVULANA zuri MAKABURINI waweza kulikimbia kwa kudhani ni JINI wakati pale maeneo UNGELIMEZEA mate.


Kuna watu HUSAHAU ubingwa wa binadamu kuogopa kufanya jambo fulani hata kama JAMII linaita hilo jambo kuwa ni ZURI au limevaa ulimbwende.

Binadamu kwa ujumla huogopa kufanya chochote kile ukimtengenezea mazingira au akiwa katika mazingira ambayo kisaikolojia au ki AKILI ZA KIBINADAMU anaanza kustukia kuwa labda ni kweli pale MAKABURINI , kuna BINTI mchawi na HAWALA yake watakaoKULOGA ukienda kuchuma KISAMVU.

SAMAHANI labda ninakuogopa wewe kwa sababu wewe....:

  • ....... ni PADRE au Shekhe, hukawii kunikumbusha miye ni mwenye dhambi .
  • ....ni mzuri kupita kiasi na naogopa utaninyima nikikuomba kwa staili za ; HALO DADA ULE MPANGO VIPI?
  • ......unamiakili sana na kila nikiongea na wewe najisikia MJINGA!
  • ......mkarimu sana kiasi kwamba najiona mimi mtu mbaya nikiwa nawe kwa sababu sijasaidia kama nitegemewavyo wale NDUGU, JAMAA, MARAFIKI na MAADUI kama wewe usaidiavyo!
  • ......unamiguvu na hukawii kuwa na KISIRANI ukikosa nanihii pale nanihii.

  • AU nakuogopa tu kwa sababu wewe si ndio yule?

Swali:
  • Ushawahi kuogopa kulala ukupendako kwa kuogopa hutaamka?
  • Ushawahi KUTOOGOPA kufanya dhambi kabla hujajua kufanya nanihii ni DHAMBI?

NAWAZA tu hapa MDAU!
USITISHIKE!

Nakuacha na GEORGE BUSH akutangazie kuwa NELSON MANDELA KAFA!


Kama wewe HUNANOMA na YESU, kama NABII ISSA ua MWANA wa MUNGU a u unamzimia tu kwa kuwa YEYE BOMBA ,msikilize tu Rose Muhando akusimuliye

Au msikilize tu MYRON B akulalamikie jinsi asivyopenda MATAKO kwenye USO wake katika dawa iitwayo BOTTOM IN YUH FACE

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP