Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MADAHA ya KILE Kibwaya URUDIACHO, Chupi URUDIAYO au hata Gwaguro URUDIALO kuvaa MARA KADHAA wa kadhaa ZAIDI!

>> Friday, July 18, 2008

Mazoea ni MATAMU!

CHAI ya CHUMVI inaweza kuwa TAMU kama tu CHAI ya SUKARI ukiizoea.

Uhusiano wako na NJIA ikatiziayo MIGOMBANI kwenda KULE, labda ni MAZOEA tu na SIO kweli ILE ni njia FUPI au INAKWEPA nyumbani kwa akina NOELA.

Lakini.....
....inawezekana , ile SURUALI inabidi TURUDIE tu kuivaa kwa sababu ndio kisitiri UUNGWANA kilichopo.


ULICHOZOEA kufanya unajua jinsi ya KUKIFANYA.

Ulichozoea kufanya unaweza kukifanya bila KUUMIZA sana FIKIRA.

Unajua tu UKIMTEKENYA PALE kwenye KIPELE ataKUFYONZA kama umemzoea au UMEZOEA.

UKIZOEA utajua tu BUIBUI wanajificha wapi pale kwenye KONA au kwenye SEHEMU za SIRI za KITANDA, wakati unasafisha CHUMBA.

Swali:

  • Umezoea KUTOJIAMINI?
  • Umezoea KUONEWA?
  • Umezoea KUJIAMINI kupita kiasi?
  • Umezoea KUONEA?
  • Umezoea kuwa wewe MTOTO MZURI?

Tatizo ni:....
  • ....mazoea mengine HATA kama ni MABAYA utajikuta UNAYARUDIA tu.
  • .....unaweza kuzoea UTOTO mpaka unajikuta umekuwa MKUBWA lakini bado TOTO KUBWA.

Unaweza ukazoea UJANA mpaka ukiwa Mzeee, UZEE ukaKUSHINDA.

DUH!


BASI NAacha topiki !


BAADAYE BASI!


Ngoja mtoto mwingine wa FELA KUTI kwa jina FEMI KUTI ajaribu kutupa MOYO katika gruvu iitwayo DO UR BEST!


AU ngoja LL Cool J alainishe kwa kibao DOIN' IT

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP