Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STAREHE ya KUONGELEA nini UTAFANYA!

>> Thursday, July 17, 2008

ASHKI ya KUFANYA mara nyingi ni kubwa kuliko ya KUONGELEA UTAFANYA.

KUONGELEA nini UTAFANYA ni rahisi kidogo, INGAWA ni NGUMU KIDOGO zaidi ya kufikiria tu UTAFANYA.


Kuongelea nini UTAFANYA kama vile kufikiria UTAFANYA , unaweza USIFANYE!
:-(

Lakini....
..... ukiongelea nini UTAFANYA , mwenzako anaweza KUFANYA.

FIKIRA zako za KUFANYA au KUMFANYA kama sio KUFANYWA , kama hujaziongelea , zinaweza zikabakia kuwa SIRI YAKO.

Kwa hiyo USIPOFANYA haina maana HAKIFANYIKI.

Kuna ambao hakijakatiza tu AKILINI ndio maana HAWAJAFANYA.

Swali:

  • Unafikiri ni kwanini OSAMA bin LADEN HAFANYI baadhi ya WAFUASI wake WAFANYAVYO, kama vile kujisikia KUFAKUFA?
  • Ushawahi kutaka kuanzisha KIOSKI au KUFUGA kuku kwa sababu JIRANI yako anafuga KUKU na sio BATA?

NAACHA hii topiki MKUU nisije nikakuzingua!

BAADAYE basi kama HATUJAFA!

AU?

Ngoja ENYA atukumbushe THE FUGEES walitoa wapi mirindimo ya READY or NOT katika kibao Boadicea


AU Mario Winans aendeleze walipoachia FUGEES katika dawa iitwayo - i don't wanna know



AU twende CONGO kwa DANY ENGOBO(samahani video ina wanawake ambao kuna mwanamke au mtu fulani anaweza asifurahie WANAVYOFANYA, kuvaa au KUCHEZA.SAMAHANI!)

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Said Michael 7:58 pm  

Ni bora iwe siri kisha watu waone umefanya, kuliko uongee halafu ushindwe kufanya

Simon Kitururu 7:03 pm  

@SAID:Kweli Mkuu! Lakini kuna mtu awezaye kusema INATEGEMEA!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP