Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UGUMU wa kuongelea MUNGU au SHETANI au uhakika wa UJAMAA na UBEPARI!

>> Thursday, July 17, 2008

MASWALA ya MUNGU magumu kuyaongelea kwa sababu unaweza ukajikuta UMEKUFURU kwa tafsiri zako au za YULE za kuelewa MASWALA ya MUNGU:

Uzuri wa maswala ya MUNGU , kuna dini bwelele zimsaidiazo yule, yeye au mimi kutafsiri au kuelewa ya MUNGU.

Ukishindwa zaidi kufikia kuelewa ya MUNGU, baadhi ya dini zitakushauri usali , au utubu ili hatima yako isiwe motoni au pale tu mahali pa mateso.

UZURI wake ni kwamba dini kibao tokea uanze kuijua ita-kuthibitishia kuwa MUNGU humshinda SHETANi na kwa hiyo wewe kama mjanja tokea mwanzo utajua ni nini chaguo zuri.


Lakini....
.... tunakumbushwa kuwa SHETANI atadaka wafuasi wengi kwenda nao pale kijiweni JEHANAMU kuliko wachache watakao kwenda PARADISO na baadhi ya dini maarufu.

Kwahiyo inawezekana MASWALA ya MUNGU si rahisi sana kuyaelewa, kwa hiyo hata mimi kuendelea kuyaandika hapa naweza tu nikakuzingua ingawa yako mawazoni leo ,kama jana na juzi.

LABDA hata kama hatuyaelewi......

....TUKUMBUKE kusali, Kuswali na kadhalika kadhaa, ilikujiweka katika mkao wa kwenda kijiwe cha PARADISO au kona ya MBINGUNI basi!
SWALI:

  • Unayaelewa maswala ya MUNGU zaidi ya ya SHETANI?

Ukiachana na ya MUNGU, nawezakwenda kwa ya-KIBINADAMU kama ya UJAMAA na UBEPARI ambayo waweza kukiri tu , jinsi gani kuyaelewa ya kibinadamu ilivyo vigumu pia.

SWALI:
  • Unadhani unayaelewa maswala ya KIBINADAMU?

Lakini....
...twaweza kukiri kuwa UJAMAA na UBEPARI vyote vimeshindwa kumkomboa binadamu.

Kwa waliofaidika na UJAMAA, kuna mamilioni hawakufaidi matunda, na kwa wafaidikao na UBEPARI, kuna mabilioni hawafaidiki na matunda wala juisi ya UKWAJU.

UBEPARI hata kwa jinsi usifiwavyo hasa baada ya USOSHALISTI wa URUSI kushindwa, UTASHANGAA kujua kuwa ndani ya nchi viongozi wa ubepari kama U.S.A , mambo si shwari na CHAMOTO utakiona ukiwa katika upande wa wasionacho au WATAWALAO.

Ukiongelea SIASA au UCHUMI na WATAALAMU zaidi ya MMOJA katika SIASA na UCHUMI, utajikuta hukawii kuanza kujiuliza kuwa ni nani kati yao, au ni yule au mimi MKALI kwa kubunia MAJAWABU ya matatuzi ya matatizo ya JAMII.

Kwa ujumla NAWEZA kukiri ......
.......YA MUNGU ni magumu kwangu, Lakini ya KIBINADAMU vile vile si rahisi kwangu!

:-(


Majibu mengi yetu wengi ,kuhusu kesho, KESHO ikifika, waweza kuhisi labda yangetatua tatizo jana au JUZi.

NISIKUKATISHE tamaaa!

  • Inaaminika Binadamu KAPEWA AKILI ya kutatua ya kesho, hata kama jawabu la usiwe na mimba kesho ,nikujua kuficha uchi leo.

  • BINADAMU kapewa akili, kama dini yako inasema tubu au sali iliuende MBINGUNI au UELEWE, basi sali ili usiwe katika namba ya kundi limpalo kampani SHETANI hapo baadaye kidogo baada ya KUFA

Swali:
  • Unafikiri ni kwanini katika SIASA au UCHUMI kila hoja INAMPINZANI?
  • Unafikiri ni kwanini inasemekana SHETANI atashindwa wakati dini kibao zinasema ndio atachukua watu wengi?
  • Unafikiri kwa WENGINE jehanamu haitusulubu hapahapa DUNIANI?
Naacha basi kuwaza topiki MDAU!

Tujikumbushe kidogo HAPA kuhusu SHETANI ni nani

Unakumbuka MUNGU?
SIKU NJEMA!


Ngoja ni muache FELA KUTI enzi za 1971...


Au nimuache Mtoto wa FELA KUTI , SEUN KUTI akukumbushe kupiga vita MBU na MALARIA hivi karibuni....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP