Wednesday, July 30, 2008

Niko TANZANIA , najifunza KWA muda KIDUCHU kunanihii!

Niko BONGO nyoso , bado sijajulia.

Unawezakunipata kwenye namba:+255765855382

Usipoangalia, NITAKUJIBU!
Nikichelewa kurudi hapa kijiweni, NAOMBA MSAMAHA!

BAADAYE BASI!

Monday, July 21, 2008

SIKUBALIANI na WEWE kuhusu UKOKO, dini au M-BINYO kama tu NIKUKUBALIAVYO kuhusu MAISHA!

WEWE si YULE!

Kuna ambacho YULE anaweza akakudanganya UKAAMINI!
:-(

Wakati unamkubalia, unaweza ukawa unauhakika ANAKUDANGANYA ingawa unapenda tu SAUTI ya SENTENSI.

Wakati unakataa , unaweza ukawa na sura ya FURAHA ingawa labda UNGEKUBALI, ungekula PILAU, kama wewe ni MPENZi wa PILAU.

SWALI:

  • Unafikiri umekataa mara ngapi kuliko ulivyokubali KUONJA?
  • Unafikiri unakubali kuliko KUKATAA ukiNYOLISHWA?
Naacha basi hii topiki!
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Ngoja Morgan HERITAGE watukumbushe kurudi kazini katika LONGOLONGO iitwayo READY TO WORK.

au SANTANA ambaye pia amenisaidia KUPITILIZA wiki hii atukumbushe ENZI za WOODSTOCK 1969 katika SOUL SACRIFICE.


BAADAYE BASI!
AU?

Sunday, July 20, 2008

JEMADARI HAMU!

Ukiwa na HAMU!
Akili yako itajaribu kukutimizia HAJA za HAMU.


Ukiwa na haja, ni rahisi kufikiria kuwa kuna staili BOMBA za kutimiza HAJA yako kama YAKE.


Kutimiza haja yako ,inawezekana kuwa ni WEWE PEKEE unaweza kusawazisha kwa sababu UKWELI ni kwamba haja yako unaijua vizuri wewe MWENYEWE.

Swali:

  • UNAFIKIRI kuna staili nzuri ya kuongelea haja ambayo inadaka yote yaliyo kwenye MIMBA ya HAJA yako?

SIKU NJEMA!
------------------------------------------------------------------------------------------------

NAKUACHA na JESS MATADOR akija na dawa iitwayo Décalé Gwada

AU pata picha fulani KADHAA zangu na WADaU kadhAA!
Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket


Photobucket



Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket

Photobucket


Photobucket



Photobucket


Photobucket




Photobucket



Photobucket

Photobucket

Photobucket



Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket
PUMZIKA na NINA SIMONE kiduchu akija na dawa iitwayo FOUR WOMEN

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket
SAMAHANI!

FilmLOOP inanizingua kiduchu, KWAHIYO inawezekana ikawa nimeweka picha NYINGI kadhaa wa kadhaa na HEADMASTER huwa anafikiria kuwa SI mchezo MZURI kuweka PICHA ambazo labda haziFUNDISHI KIPENYO ni sawasawa na nini katika TUNDU.


:-(

Lakini nitajaribu KUSAWAZISHA!

Ziruke tu PICHA kama zinaKUZINGUA!


HALAFU ni KWELI .....


MARY J BLIGE, SHAGGY , DJ CLIFF na.....
......wamenisaidia sana kupitiliza, kama UONAVYO kwenye PICHA......
:-(



Mpate SHAGGY aendeleze DAWA iitwayo BONAFIDE MSICHANA

Friday, July 18, 2008

MESEJI ya UJUMBE wako au WAKE huweza KUPOTEA akilini mwa BIN-ADAMU umtongozaye hata kama ALIIPATA KAULI!

Kuna watakaosema kuwa ,HATA UJUMBE wa YESU au IDDI AMINI , kuna waliousikia na KUUSAHAU kama tu UJUMBE wa NYERERE au yule BABU YAKO.


NGUVU ya UJUMBE ulioupata na KUTOUFANYIAKAZI ni MZURI tu kama MABIRINGANYA uliyopewa lakini HUKUYALA.

Tatizo la ujumbe uupatao,.........

....... ni ukweli kwamba MTU MWINGINE ndio anayekupa huo USHAURI ,ilikukusaidia ufike AFIKIRIAKO unataka kwenda au inawezapia kuwa ANAKUGAWIA UJUMBE katika kujisaidia YEYE MWENYEWE kujisikia kasaidia , kakusaidia AU kakushauri!

Swali:

  • Hivi ni kweli unataka kwenda KULIA kama ushauriwavyo nawafikiriao unakwenda KUSHOTO?
  • Meseji ya ujumbe wako leo kwa YULE ni NINI?

WIKIENDI NJEMA!
--------------------------------------------------------------------------------------

Pata SOUTH AFRIKA kwa KINYUME....


Ngoja JAMES RANDI ajaribu kuangalia Psychometry



Namuacha tena MICHAEL JACKSON katika DANCE BREAK

MADAHA ya KILE Kibwaya URUDIACHO, Chupi URUDIAYO au hata Gwaguro URUDIALO kuvaa MARA KADHAA wa kadhaa ZAIDI!

Mazoea ni MATAMU!

CHAI ya CHUMVI inaweza kuwa TAMU kama tu CHAI ya SUKARI ukiizoea.

Uhusiano wako na NJIA ikatiziayo MIGOMBANI kwenda KULE, labda ni MAZOEA tu na SIO kweli ILE ni njia FUPI au INAKWEPA nyumbani kwa akina NOELA.

Lakini.....
....inawezekana , ile SURUALI inabidi TURUDIE tu kuivaa kwa sababu ndio kisitiri UUNGWANA kilichopo.


ULICHOZOEA kufanya unajua jinsi ya KUKIFANYA.

Ulichozoea kufanya unaweza kukifanya bila KUUMIZA sana FIKIRA.

Unajua tu UKIMTEKENYA PALE kwenye KIPELE ataKUFYONZA kama umemzoea au UMEZOEA.

UKIZOEA utajua tu BUIBUI wanajificha wapi pale kwenye KONA au kwenye SEHEMU za SIRI za KITANDA, wakati unasafisha CHUMBA.

Swali:

  • Umezoea KUTOJIAMINI?
  • Umezoea KUONEWA?
  • Umezoea KUJIAMINI kupita kiasi?
  • Umezoea KUONEA?
  • Umezoea kuwa wewe MTOTO MZURI?

Tatizo ni:....
  • ....mazoea mengine HATA kama ni MABAYA utajikuta UNAYARUDIA tu.
  • .....unaweza kuzoea UTOTO mpaka unajikuta umekuwa MKUBWA lakini bado TOTO KUBWA.

Unaweza ukazoea UJANA mpaka ukiwa Mzeee, UZEE ukaKUSHINDA.

DUH!


BASI NAacha topiki !


BAADAYE BASI!


Ngoja mtoto mwingine wa FELA KUTI kwa jina FEMI KUTI ajaribu kutupa MOYO katika gruvu iitwayo DO UR BEST!


AU ngoja LL Cool J alainishe kwa kibao DOIN' IT

Thursday, July 17, 2008

STAREHE ya KUONGELEA nini UTAFANYA!

ASHKI ya KUFANYA mara nyingi ni kubwa kuliko ya KUONGELEA UTAFANYA.

KUONGELEA nini UTAFANYA ni rahisi kidogo, INGAWA ni NGUMU KIDOGO zaidi ya kufikiria tu UTAFANYA.


Kuongelea nini UTAFANYA kama vile kufikiria UTAFANYA , unaweza USIFANYE!
:-(

Lakini....
..... ukiongelea nini UTAFANYA , mwenzako anaweza KUFANYA.

FIKIRA zako za KUFANYA au KUMFANYA kama sio KUFANYWA , kama hujaziongelea , zinaweza zikabakia kuwa SIRI YAKO.

Kwa hiyo USIPOFANYA haina maana HAKIFANYIKI.

Kuna ambao hakijakatiza tu AKILINI ndio maana HAWAJAFANYA.

Swali:

  • Unafikiri ni kwanini OSAMA bin LADEN HAFANYI baadhi ya WAFUASI wake WAFANYAVYO, kama vile kujisikia KUFAKUFA?
  • Ushawahi kutaka kuanzisha KIOSKI au KUFUGA kuku kwa sababu JIRANI yako anafuga KUKU na sio BATA?

NAACHA hii topiki MKUU nisije nikakuzingua!

BAADAYE basi kama HATUJAFA!

AU?

Ngoja ENYA atukumbushe THE FUGEES walitoa wapi mirindimo ya READY or NOT katika kibao Boadicea


AU Mario Winans aendeleze walipoachia FUGEES katika dawa iitwayo - i don't wanna know



AU twende CONGO kwa DANY ENGOBO(samahani video ina wanawake ambao kuna mwanamke au mtu fulani anaweza asifurahie WANAVYOFANYA, kuvaa au KUCHEZA.SAMAHANI!)

UGUMU wa kuongelea MUNGU au SHETANI au uhakika wa UJAMAA na UBEPARI!

MASWALA ya MUNGU magumu kuyaongelea kwa sababu unaweza ukajikuta UMEKUFURU kwa tafsiri zako au za YULE za kuelewa MASWALA ya MUNGU:

Uzuri wa maswala ya MUNGU , kuna dini bwelele zimsaidiazo yule, yeye au mimi kutafsiri au kuelewa ya MUNGU.

Ukishindwa zaidi kufikia kuelewa ya MUNGU, baadhi ya dini zitakushauri usali , au utubu ili hatima yako isiwe motoni au pale tu mahali pa mateso.

UZURI wake ni kwamba dini kibao tokea uanze kuijua ita-kuthibitishia kuwa MUNGU humshinda SHETANi na kwa hiyo wewe kama mjanja tokea mwanzo utajua ni nini chaguo zuri.


Lakini....
.... tunakumbushwa kuwa SHETANI atadaka wafuasi wengi kwenda nao pale kijiweni JEHANAMU kuliko wachache watakao kwenda PARADISO na baadhi ya dini maarufu.

Kwahiyo inawezekana MASWALA ya MUNGU si rahisi sana kuyaelewa, kwa hiyo hata mimi kuendelea kuyaandika hapa naweza tu nikakuzingua ingawa yako mawazoni leo ,kama jana na juzi.

LABDA hata kama hatuyaelewi......

....TUKUMBUKE kusali, Kuswali na kadhalika kadhaa, ilikujiweka katika mkao wa kwenda kijiwe cha PARADISO au kona ya MBINGUNI basi!
SWALI:

  • Unayaelewa maswala ya MUNGU zaidi ya ya SHETANI?

Ukiachana na ya MUNGU, nawezakwenda kwa ya-KIBINADAMU kama ya UJAMAA na UBEPARI ambayo waweza kukiri tu , jinsi gani kuyaelewa ya kibinadamu ilivyo vigumu pia.

SWALI:
  • Unadhani unayaelewa maswala ya KIBINADAMU?

Lakini....
...twaweza kukiri kuwa UJAMAA na UBEPARI vyote vimeshindwa kumkomboa binadamu.

Kwa waliofaidika na UJAMAA, kuna mamilioni hawakufaidi matunda, na kwa wafaidikao na UBEPARI, kuna mabilioni hawafaidiki na matunda wala juisi ya UKWAJU.

UBEPARI hata kwa jinsi usifiwavyo hasa baada ya USOSHALISTI wa URUSI kushindwa, UTASHANGAA kujua kuwa ndani ya nchi viongozi wa ubepari kama U.S.A , mambo si shwari na CHAMOTO utakiona ukiwa katika upande wa wasionacho au WATAWALAO.

Ukiongelea SIASA au UCHUMI na WATAALAMU zaidi ya MMOJA katika SIASA na UCHUMI, utajikuta hukawii kuanza kujiuliza kuwa ni nani kati yao, au ni yule au mimi MKALI kwa kubunia MAJAWABU ya matatuzi ya matatizo ya JAMII.

Kwa ujumla NAWEZA kukiri ......
.......YA MUNGU ni magumu kwangu, Lakini ya KIBINADAMU vile vile si rahisi kwangu!

:-(


Majibu mengi yetu wengi ,kuhusu kesho, KESHO ikifika, waweza kuhisi labda yangetatua tatizo jana au JUZi.

NISIKUKATISHE tamaaa!

  • Inaaminika Binadamu KAPEWA AKILI ya kutatua ya kesho, hata kama jawabu la usiwe na mimba kesho ,nikujua kuficha uchi leo.

  • BINADAMU kapewa akili, kama dini yako inasema tubu au sali iliuende MBINGUNI au UELEWE, basi sali ili usiwe katika namba ya kundi limpalo kampani SHETANI hapo baadaye kidogo baada ya KUFA

Swali:
  • Unafikiri ni kwanini katika SIASA au UCHUMI kila hoja INAMPINZANI?
  • Unafikiri ni kwanini inasemekana SHETANI atashindwa wakati dini kibao zinasema ndio atachukua watu wengi?
  • Unafikiri kwa WENGINE jehanamu haitusulubu hapahapa DUNIANI?
Naacha basi kuwaza topiki MDAU!

Tujikumbushe kidogo HAPA kuhusu SHETANI ni nani

Unakumbuka MUNGU?
SIKU NJEMA!


Ngoja ni muache FELA KUTI enzi za 1971...


Au nimuache Mtoto wa FELA KUTI , SEUN KUTI akukumbushe kupiga vita MBU na MALARIA hivi karibuni....

Wednesday, July 16, 2008

KUHUSU ubingwa wa BINADAMU katika KUSTUKIA harufu MBAYA ya WALI

INASEMEKANA ...
.....MBWA , Nguruwe au hata NGEDERE wanauwezo mkubwa wa KUSTUKIA harufu kuliko BINADAMU.



Inasemekana....
......BATA , Nyoka au hata MINYOO, inauwezo mkubwa wa KUOGELEA kuliko BINADAMU.

Labda.....
......KUKU anaweza akawa MJANJA kuliko binadamu ndio maana bado hajaanza kutafuta kuvaa chupi na bado anatembea kwa maringo BILA VIATU.

SI BINADAMU anaamini ANAAKILI kuliko viumbe vingine, ndio maana hata VISIVYO vya MAANA ni vya MAANA kwa MTU?

SI...
...ndio maana BINADAMU anadharau BATA na hata BIN-ADAMU MWENZIE kwasababu eti yule ni ANDUNJE?

BASI MKUU naacha hiiTOPIKI!

Swali:

  • Kama BINADAMU tujuavyo harufu ya MAANDAZI, unafikiria MBWA anafikiria binadamu ananuka sana WAPI na ananukia harufu GANI?


DUH!

Nakutakia HARUFU njema basi!
-------------------------------------------------------------------------------------------------



HEBU cheki WALIOKUWAnavyo tokea enzi hizo ndani ya AFRICA



Angalia tu kiendeleacho akilini mwa Binadamu akifikiria anashuhudia...

au twende tu KAMERUNI tukapate maswala ya Longue Longue

MADAIRO ya KUFANYA ujinga kwa kutumia AKILI.

Kusema NISHAI!

Unaweza ukajikuta umehakikishia UMATI upumbavu kwa kitendo chako cha KUONGELEA KITU au hata SENENE.

Tatizo la kukaa KIMYA, ni udhaifu wake katika kusaidia watu kujua NANIHII au UPUMBAVU.

Ukitaka kuongea kama unaAKILI kuhusu jambo la KIPUMBAVU, kuna watakaofikiri jambo la KIPUMBAVU ni la MAANA au ni la akili.

Lakini...
...inawezekana kwamba ni kweli kila mtu anaAKILI na ni ujazo tu katika MATUMIZI ya AKILI utofautishao UJINGA wa yule na yeye kama sio MIMI.

Natishika na JINSI wenye BUSARA na AKILI wafanikishavyo KUFANYA UJINGA kwa kutumia AKILI!

SWALI:

  • Ushafanikiwa kufanya UJINGA mara ngapi tokea JANA?

SIKU NJEMA!


------------------------------------------------------------------------------------
Kama una nafasi mcheki Joshua Klein: azungumzie maswala ya AKILI ZA KUNGURU katika :The amazing intelligence of crows




Mike Myers akughanie malalamiko yake kidogo kuhusu MWANAMKE katika Woman Beat Poem


Au nimuache tu FOXY BROWN katika OH YEAH

Monday, July 14, 2008

SIASA ya UJAMAA na KUMTEGEMEA

KUMTEGEMEA ni starehe kwa sababu unahisi ANACHO.

Huhitaji shule kujifunza KUMTEGEMEA.

LAKINI.................
..utamu wa KUMTEGEMEA ni pale UHISIVYO anaKUNYIMA.

SWALI:

  • Ushawahi kutegemea kuna KESHO kwa sababu leo umeAMKA?

  • Unakumbuka SIASA ni neno tu liwakilishalo NANIHINO isababishayo uhisi KIGOMA ni pazuri kuliko NJOMBE?


SAMAHANI tu kwa KUKUZINGUA kwa kuongea UJINGA!

:-(
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Tumsikilize kidogo NELSON MANDELA kabla hajawa MPOLE.

Ngoja SUGA RAY waendeleze LONGOLONGO iitwayo FLY

AU nikuache tu na CURTIS MAYFIELD atupe dawa iitwayo SUPERFLY.


BAADAYE basi kama sijafa!

Sunday, July 13, 2008

MASWALA ya kumtamani MKE au MTU wa MTU!

Swali:

  • Ushawahi kumtamani mke wa NYANI?
Kisicho chako kinavutia kama kufanya MATUSI!

Staili yako yakuvutiwa kugida UKOKO anaijua aliyepembeni yako wakati unajifanya unaonja UTANDU.
Asiyejua jinsi uchuchumavyo MSALANI ,wakati unatafuta KUSIGINA, anaweza akadhani kuwa anajua unavyo KUNYA kwa sababu anajua kilaMTU baada ya muda fulani KIDUCHU, ana kunya.

(SAMAHANI kwa kutamka neno KUNYA. Nilikuwa na maanisha kwenda haja KUBWA!):-(


Wakati unamtamani KIKWETE au KHADIJA, inamaanisha USHAKULA chaKULA.

Ukiwa na njaa........., HAUSIgeli, hausiBOI,au hata MWALIMU wa KEMISTRI, haTAMANIKI.

HATA ZUBEDA au SAIDI, kama unatumia afichasho SAIDI na MWAJUMA,hatamaniki kama tu KISAMVU wakati unahisi unataka kula CHIPSI mjusi.

LAKINI.....
.....wakati unafikiria kutamani kufanya UASHERATI na nanihinoo, inamaana ungetaka tu kufanya UASHERATI na nanihino kwa sababu nanihii IMEPIGA MAGOTI au imelowa kutokana na shahuku ya JEMEDARI HAMU . Tendo hilo lingekufanya UWE TU BINADAMU haLISI.


Kuna vitu wewe kama binadamu , lazima uvipitie au vikuPITIE tu.

AU?

SWALI:
  • USHAWAHI kutamani KUWA MKUBWA?

Naacha hii TOPIKI MDAU!
NAACHA kabla ujaanza kuwa na uhakika kama namtamani HAUSIGELi wako kama TIGER WOODS alivyo mpata MKEwake kpitia kwa .........

DUH!
------------------------------------------------------------------------------------
PATA kidogo TOUCH and GO wakiuliza UTAFANYA uasherati na MIMI?


Jaribu kucheka kama HAWA JAMAA watakuchekesha

AU tuende tu kumsikiliza ISPECTA akiwa na wadau zake wa BONGO NYOSO katika dawa iitwayo JELA

Friday, July 11, 2008

HONGERA mvivu UGUNAYE CHOONI kama YEYE ,yule au MIMI !

Swali:

  • Ushawahi kukutana na UAMINIYE kuwa ni MVIVU wakati ana NJAA?


Uaminiye ni Mvivu, anaweza kukushinda kwa bidii ya KUOMBA!


Mvivu kwenda KAZINI, anaweza akawa ni JEMADARI kwa kwenda MADUKANI kununua ANASA , kama unampatia au anajipatia ile PESA AMBAYO ingekuwa yakununulia Bata wa KRISMASI au ya kujipendekeza tu kwa MAMA MKWE au JIRANI

Mvivu wa kusoma KAMASUTRA aweza kuwa anajuhudi ya kupika KASHATA:

Saaaaasaaaaaaaaaaaa!

NISikuzingue MDAU!

SIna stori kama kawaida zaidi ya ujinga wangu!

WIKIENDI NJEMA!


-------------------------------------------------------------------------------------------------
SAMAHANI kwa HERUFI KUBWA!

HEBU kama si muoga wa mashetani au muoga lakini unataka kujua stori za ATOLEWAYE SHETANI , twende UFILIPINO Kidogo tukasikilize kitu....

HALAFU Kama MUOGA , usiangalie kideo hiki cha SHEKHE amtoavyo shetani pale BRUNEI

AU tulia tu au ANGALIA na SIKILIZA Morgan Heritage wakupe dawa iitwayo Liberation

Wednesday, July 09, 2008

SIRI ya WASIKILIZAO nyimbo za dini kwenye DHAMBI au wafanyao dhambi pembeni kidogo ya BIBLIA , KORANI au KILE kitabu fulani kikatazacho NANIHII!

KILA kitu ni kitu cha kumuogopesha BIN-ADAMU !

Na

MIMI NAOGOPA kufanya dhambi kutokana na kufunzwa na kujifunza ubaya wa dhambi hasa katika kusababisha kuwezesha kwenda kwangu JEHANAMU!

:-(

Tatizo la uoga wa kufanya dhambi ni uwezo wetu binadamu kuzoea vitu hasa kama matokeo ya kucheza na moto huyastukii hapahapo kuwa UMEUNGUA .

UZOEFU wa kuzoea KIPORO cha wali na MAHARAGE ya nazi ya jana, hutufanya kudhani kuwa kwa sababu hatuumwi tumbo, basi KIPORO hakina vijidudu au , bakteria wakichezeacho MDAKO wakati unakigida.


Swali:

  • Kama unapenda maziwa , ushastukia kuwa maziwa yamgando, mtindi au..... ni maziwa yaliyoharibika?
  • Ushawahi kumuogopa MZAZI , au NDUGU akutakiaye mema kwa staili zake za kukufikishia ujumbe?
  • Ushawahi kuogopa kumuambia umpendaye kuwa UMEMZIMIA na kila ukichukua sabuni yako ya MBUNJU kwenda KUOGA ,unamuona kwenye beseni?



Ukifikiria sana, unaweza kukumbuka kuwa kama wewe ni mshirikina, LIBINTI au LIMVULANA zuri MAKABURINI waweza kulikimbia kwa kudhani ni JINI wakati pale maeneo UNGELIMEZEA mate.


Kuna watu HUSAHAU ubingwa wa binadamu kuogopa kufanya jambo fulani hata kama JAMII linaita hilo jambo kuwa ni ZURI au limevaa ulimbwende.

Binadamu kwa ujumla huogopa kufanya chochote kile ukimtengenezea mazingira au akiwa katika mazingira ambayo kisaikolojia au ki AKILI ZA KIBINADAMU anaanza kustukia kuwa labda ni kweli pale MAKABURINI , kuna BINTI mchawi na HAWALA yake watakaoKULOGA ukienda kuchuma KISAMVU.

SAMAHANI labda ninakuogopa wewe kwa sababu wewe....:

  • ....... ni PADRE au Shekhe, hukawii kunikumbusha miye ni mwenye dhambi .
  • ....ni mzuri kupita kiasi na naogopa utaninyima nikikuomba kwa staili za ; HALO DADA ULE MPANGO VIPI?
  • ......unamiakili sana na kila nikiongea na wewe najisikia MJINGA!
  • ......mkarimu sana kiasi kwamba najiona mimi mtu mbaya nikiwa nawe kwa sababu sijasaidia kama nitegemewavyo wale NDUGU, JAMAA, MARAFIKI na MAADUI kama wewe usaidiavyo!
  • ......unamiguvu na hukawii kuwa na KISIRANI ukikosa nanihii pale nanihii.

  • AU nakuogopa tu kwa sababu wewe si ndio yule?

Swali:
  • Ushawahi kuogopa kulala ukupendako kwa kuogopa hutaamka?
  • Ushawahi KUTOOGOPA kufanya dhambi kabla hujajua kufanya nanihii ni DHAMBI?

NAWAZA tu hapa MDAU!
USITISHIKE!

Nakuacha na GEORGE BUSH akutangazie kuwa NELSON MANDELA KAFA!


Kama wewe HUNANOMA na YESU, kama NABII ISSA ua MWANA wa MUNGU a u unamzimia tu kwa kuwa YEYE BOMBA ,msikilize tu Rose Muhando akusimuliye

Au msikilize tu MYRON B akulalamikie jinsi asivyopenda MATAKO kwenye USO wake katika dawa iitwayo BOTTOM IN YUH FACE

Saturday, July 05, 2008

Labda UNANIPENDA au UNAMPENDA kama KONDOMU!

Pamoja na uzuri wa KONDOMU , ikitumika hutupwa!:-(

SAMAHANI !
Ngojea nikusalimie kwa sauti!



KONDOMU kiboko!

Ikishabeba ujauzito, hutupwa!
Inawezekana kuwa marafiki wengi uwaitao MARAFIKI ni kwasababu UNAWAITA marafiki na wanakupenda kama chakula kabla hujakistukia KIMECHACHA.

CHAKULA kilicho chacha kina harufu fulani ambayo unaweza usiistukie mpaka UONJE:

Labda RAFIKI yako mpenzi umuitaye RAFIKI mpenzi ni kwa sababu unaamini ni RAFIKI mpenzi.

LABDA...

...RAFIKI wa kweli ni yule umuitaye ADUI YAKO ambaye anakusaidia KUSTUKIA unacheza na moto wakati unacheza na MOTO:

DUH!

NAACHA TOPIKI HII!

ENDELEZA lakini PENZI na YULE , yeye au RAFIKI kwa furaha hata kama UTATAFUTA jalala kutupa mafanikio yatokanayo na kufanikisha ambayo hayakusitishi kutupa KONDOMU uisifiayo !:-(
--------------------------------------------------------------------------------------------------
Mpate tu RAY C akupe dawa iitwayo SOGEA SOGEA


AU pata baadhi ya PICHA zangu na baadhi ya WADAU ambao hawakunitenga maeneo fulani.
Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket

AU wapate tu

Professor Jay & MwanaFalsaFA katika dawa iitwayo JUKUMU LETU



Msikilize tu MIRIAM MAKEBA akikupa dawa iitwayo MBUBE

Friday, July 04, 2008

Katika MAHAKAMA ya MTAZAMO wa JAMII hata kama hukunyemelea KITUMBUA!

Moja ya udhaifu wa binadamu ni KUFANANISHA!

Hukawii kusikia mtu anamfananisha mtoto mwenye kitumbo kikubwa kutokana na KWASHAKOO kuwa anafanana na BABU yake mwenye kitumbo kikubwa kutokana na POMBE ya ULANZI.

Kirahisi tu, waweza kuogopwa au kupendwa kutokana na staili yako ya nywele kama MADENGE .


Watu kirahisi wataamini kuwa ULIFANYA kama unafanana na waaminiye ANAFANYA!

Ukifanana fanana na MWIZI au MALAYA pale maeneo, kama hawajui kuwa wewe swala tano au 24, watakutendea kwanza kama wamtendeavyo MWIZI au MALAYA .


Staili ya jamii kukushuku kutokana na KIMINI SKETI chako, PARA LAKO kama mvuta bange au MARASTA YAKO kama kichaa, INAWEZA KUKUSAIDIA KUPATA au KUKOSA.

Na staili ya jamii kutengeneza tuaminivyo kuwa PADRE au SHEKHE ni mwaminifu kuliko MFYEKA MAJANI au MUUZA KIGENGE pale kona, imesaidia sana kuwasababisha WAHALIFU wakubwa kutostukiwa na watenda wema kuonekana MAFALA .Na labda inasaidia wake na wanaume wa watu fulani KUONJA KITUMBUA wakikinai MAANDAZI kila siku,hasa pale watu wafikiriapo kuwa kwa sababu wewe WINNIE MANDELA basi huwezi kumfikiria CHAKUBANGA katika kutimiza kukuna NAZI.

INASIKITISHA sana kuwa BINADAMU WENYE AKILI bado tunadhani kuwa KIBAKA , MHUNI , MALAYA au MSWALIHINA ana sura fulani au anavaa kitu fulani na sio USHANGA ULE kiunoni.

DUH !
NAACHA topiki!

SAMAHANI!
Swali:

  • Unafikiri wewe si MHUNI?

Wikiendi Njema basi Mdau!



-------------------------------------------------------------------------------------------------
Twende shuleni kidogo tukaangalie wanafunzi wanafikiria nini, katika ...A Vision of Students Today



Halafu twende KENYA tukapewe MUZIKI na Wyre & Prezzo katika Gimme the music


Lakini...
Kama wewe MWEUSI hata kama staili fulani ya MUZIKI haipandi, jaribu kumsikiliza BUNNY WAILER katika kibao RISE and SHINE

Thursday, July 03, 2008

KAMA unataka NISICHEKE, usinitekenye kwenye KIDONGOLOSO!

Ukinigusa pale..

........unaamsha huku
Ukiamsha kule
......naanza kustukia maswala ya NINI na KWANINI.

NINI na kwanini, ni maswala ya kujiuliza tu.

NA.....

Nikianza kujiuliza , nitataka kupata majibu.

AU...

Bila shaka nitaanza kutafuta majibu.


Tatizo la majibu ni kwamba, hata MAJIBU ya UONGO ni MAJIBU kwa afikiriaye kapata jibu.

Kwa yoyote MJANJA, usicheze na ufikiriaye mjinga ambaye KASHATEKENYWA na KASTUKIA, na anatafuta MAJIBU kutokana na UJANJA wako.

Akipata jibu , laweza likawa si jibu ulilotegemea!

  • SI wanadai aliyelala USIMUAMSHE?

Naamini AFRIKA imeamka!
Naamini mimi na wewe tuko macho , tumeamka , na tunatafuta jibu!
AU?
Swali:
  • Wewe na mimi tunatafuta jibu la swali gani?
  • Wewe , mimi na yule tunaweza kuwa na swali moja wakati mmoja?

Samahani kama nimekutekenya!
Nawaza tu hapa katika mtiririko fulani!
Kama hunielewi naongelea nini au hutekenyeki; ASANTE kwa ushirikiano!

Siku njema!
-------------------------------------------------------------------------------------
Cheki kidogo mtu awezapo kubabaika akidhani jamii imemfumania..

AU nirudi tu katika Blues nikisaidiwa na JIMI HENDRIX katika kibao Hear My Train A Comin'


AU niwaache LENNY KRAVITZ na ERIC CLAPTON wamkumbuke JIMI HENDRIX kwa kibao All Along The Watchtower

UKIMCHUNGULIA akataye MITI katika Ule msitu pale MBELE kidogo ya NANIHII!

Kama mimi na wewe tushafundishwa maswala ya UMUHIMU wa BAJETI halafu tukachacha katikati ya mwezi, wakati mwanzo wa mwezi tulikuwa na pesa yakukupitisha mwezi mzima , kwa mtazamo mwingine , wewe na mie hatuna tofauti na aliyefundishwa UMUHIMU wa MISITU halafu akakata mti ,akifikiri atapanda mwingine baadaye kidogo kabla msitu haujaisha.

Tofauti ni kwamba ukichacha unaweza ukakopa au kuvizia misiba mpaka mwezi ukapita(si kwenye harusi ukizamia ni rahisi kustukiwa kuliko msibani?), na ukikata mti , kuotesha msitu mpya ni vigumu ,kutokana na muda au hata hali ya hewa iharibikayo au hali iuleteayo mizengweMTI KUKUA hasa pale UKUAPO wakati tunautolea macho kutokana na msitu kutokuwepo.

Sasaaaa....

Yule , yeye na mimi, tunaweza kukubali kuwa mtu na akili zake hawezi kuondoka tu nyumbani kwenda kujikatia miti bila sababu. Tunajua karibu watu bilioni tatu wanatumia kuni na mkaa ili kuhakikisha kisamvu au maharage yameiva.Kwa hiyo kila siku kuna watu bilioni tatu kinamna lazima wanyemele mti fulani uwe umekauka au la:-(

Halafu ,....
....kwa wale ambao hawajawahi kukata mti , napenda kuwakumbusha kuwa kukata mti sio kazi rahisi sana, hasa ukikumbuka wakataji miti waliowengi duniani hawana vifaa virahisishavyo sana kazi hii ya kutengeneza jangwa ,zaidi ya shoka , panga au goti.

Basi labda ....
....kuna watakao sema kuwa kupanda mbegu ya mti au kupanda mti ni rahisi kuliko kukata mti na wakaanza kushangaa kwanini wakatao mti walio wengi hawapandi mti.
Inawezekana ukafikiria hivyo kirahisi kama utasahau sifa ya binadamu ya kufikiria ya leo zaidi ya ya kesho au mtondogoo.

TATIZO hili la kufikiria kesho au kizazi kijacho linafundishika zaidi hasa pale binadamu anapokuwa na uhakika wa kwake binafsi kuhusu kesho au baadaye ataimuduje kitu ambacho ni kigumu kwa maskini .

Swali:

  • Kwani unafikiri ni kwanini raia wa nchi tajiri ni rahisi zaidi kufikiria maswala ya vizazi vijavyo kuliko masikini ambaye hata kila mtoto amzaaye anaamini amekuja na ridhiki yake?
  • Ukiwa na njaa leo huwa unakumbuka sana jinsi utakavyo kabili mambo ya mwaka kesho?
  • Ukiwa na njaa sana leo ni ndugu zako wangapi wasiohusiana na wewe kula leo wakujiao akilini pamoja na mapenzi yako kama nyonyo kwao?

Nachojaribu kusema hapa ukiachia miti na misitu ni kwamba, tabia ya binadamu umchekaye au umdharauyo inaweza ikawa sawa tu na yako wewe au mimi, ila labda mimi na wewe tunafanya makosa hayohayo katika kitu kingine ambacho hatukiangalii kwa mkao wa jicho tumchungulialo tumnyosheaye kidole.
Ukifikiria sana kosa la mkata mti na kosa ufanyalo , vyote vyaweza kuzaa matunda sawasawa tu, kama vile jangwa .

Au labda...
....Kosa la bajeti au hata lile katika kucheza mchezo wa UASHERATI a.k.a MIKASI, wakati umedhamiria kustarehe halafu ukastukia unalia kwa kupata mzigo wa KUZAA au hata bahati ya KASWENDE usiyoitarajia , laweza kuwa kisaikolojia lina mizizi sawa na kosa la asiyejali akikata mti halafu analalamika akiona JANGWA.

SWALI:
  • Una uhakika ukikata mti utapanda miti?
  • Unakumbuka kama ukikata mti halafu ukapanda mti na sio miti labda unapiga makitaimu?

Naacha basi topiki!
Labda hata mtiririko wa mawazo katika swala hili uko kushoto.
Samahani! Si kujihami IMO?
AU?
Hebu tuangalie afanyacho BILL GATES siku ya MWISHO KAZINI au hata baada ya KUNG'ATUKA

AU tumsikilize tu Teddy Pendergrass aliyekuwa maarufu kwa kupiga SHOO kwa WANAWAKE pekee, atukumbushe STAREHE yaKUJUA UMPENDAYE ANAKUPENDA PIA:


Samahani,labda nikulete miaka ya karibu kidogo na ya miaka ya sasa kwa donell jones : anung'unikie maswala ya : U know what's up

Thamani ya HESHIMA ya kijambo!

Kama unaishi inamaana unathaminisha vitu.
Kama unathaminisha vitu inawezekana unadharau kitu au kuna kitu unafikiri kinathamani zaidi ya kile , hiki au hata nywelenywele za kikwapa cha nanihiii.

Lakini ....

Labda thamani ni kama noti ya pesa ambayo ni karatasi tu, wengi mkiwa na machale nayo, inageuka kuwa kama pesa ya Zimbabwe mwaka 2008, ambayo hata uwe na noti ngapi, unawezapata tatizo lakukusaidia kununua vikusaidiavyo kukuwezesha kwenda choo.

Labda hata thamani hata ya maneno inafanya tuamini kuwa maneno fulani ni machafu na mengine ni ya kuimbia kwaya KANISANI au pale chini ya MBUYU.

AU

Labda kweli kuna uchafu na usafi, hasa kama kwako vipodozi ni usafi ingawa huvilambi, mate kwako ni uchafu ukitemewa lakini si ukipigwa busu, au ukioga unaamini ngozi ishakuwa safi kama tu uaminivyo ukipiga deki, sakafu ni safi.

Angalau bado inasemekana;
HESHIMA ni kitu cha BURE.

NA....

Labda ni kweli kuna kitu umewahi kufanya kwa thamani iitwayo bure!

Lakini ni kweli inasemekana ,
.... kuna vitu baadhi ya watu wanaweza wakakiri kutoweza kuthaminisha, kama vile, mapenzi yao kwa wazazi , ndugu ,jamaa au limpezi nanihino.
Swali:

  • Kitu cha bure ni nini?
  • Unafikiri thamani ya kitu ukiitacho cha bure ni sifuri?
  • Thamani ya kitu ni nini na inatoka wapi?


SIkuKATAliI!
Lakini......
.... kuna watakao kubaliana na mimi kuwa , hakuna kitu cha bure, inategemea tu na vitu vyako unavithamanishaje.

Unaweza kujisahau na kufikiria hela ndio kipimo cha thamani ya chupi, wakati dagaa au bata waweza kuwa kipimo cha thamani ya mahari ya Simon katika kumposa Mwajuma .
Swali:
  • Ingekuwa utumwa ni biashara bomba, unafikiri ungemdaka Kijeba mtaani leo,ungemuuza shilingi ngapi?
  • Na bei ya yule Mwanadada macho ya gololi je?


Sasaaa....

Naamini thamani ya kitu inatofautiana kati ya mtu na mtu.
Inasemekana kwa Muisraeli mmoja, ni Wapalestina kadhaa wa kadhaa jichoni kwa baadhi ya Waisraeli fulani.

Labda Kikwete mmoja anaweza akawa akina mimi kadhaa vilevile jichoni kwa yule au yeye.
Na labda Kikwete kabla hajawa Nyerere alikuwa sawa tu na Mkapa au Ali Hassan Mwinyi kabla hawajawa Nyerere.

AU

INAWEZEKANA ukweli ni hakuna chenye thamani duniani kama jamii, wewe na mimi hatujakipa au kuamini kina thamani.

NA

Kijambo kinaweza kudhalilika kutokana na harufu , lakini jamii ikiamini harufu ya kijambo ina thamani kubwa , hutakawia kuona vichupa vya pafyumu za kijambo chenye mchanganyiko wa HILIKI au MAHARAGE, ni maarufu duka fulani pale nanihii.

Lakini,
...serikali ya TANZANIA au ya ..... inaheshimu na kuthamini raia wa nchi yake, wakati askari wake hawakawii kukupiga virungu ukidai kuheshimiwa kama raia wake.

AU labda ni kweli....

..Dhahabu,almasi, pesa , ndovu ....mpaka Bata wanathamanisha vitu fulani kama unataka kujua thamani ya kitumbua.

Lakini labda wewe unathamani kwangu kwa sababu hakuna mwingine kama wewe duniani.
Labda umuhimu wa kile kwako ndio una sababisha uone hiki kinathamani kwako.

Cha ajabu ni kwamba nionacho hakina thamani chaweza kuwa ndio kitu muhimu kuliko vyote kwako.

  • Si unakumbuka kama uthaminivyo wazazi wako, wako wawauao wazazi wao ili wapate urithi?
  • Si unakumbuka kucheua kudharauliwako sehemu nyingine, kuna maeneo kinatumika kutoa heshima kwa mpishi katika kuonyesha jamaa wameshiba?
  • SI jangwa kama SAHARA tulipigalo vita kwa baadi ya makabila ya Waberiberi ndi mahali pazuri kuliko pote duniani?

Basi bwana Naaacha topiki hii Mkuu!
Nawaza tu hapa katika mtiririko fulani !
Nakuthamini lakini!
AU?
Kwani wewe au mimi unadhani ni shilingi au talanta ngapi?
...
Kila lakheri katika kuendeleza kuthaminisha vitu, watu au hata matako ya Ngedere!
TUKUMBUKE tu kuwa BURE pia ni thamani!
..........................................................................................................................................................................
Hebu kama una muda mcheki tena James Randi atukumbushe jinsi ya maajabu katika saikolojia ya sisi wenye kuamini na kusoma Nyota zetu Magazetini.
Mcheki akitazama Astrology



Ningependa kuwashukuru tena ndugu, marafiki na maadui!
Hasa marafiki hawa niliokutanao na kuwadaka muda wa karibuni kama watokeao na wasio tokea kwenye baadhi ya picha zangu zifuatazo:

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket
EBWANA samahani nilizimika!Kwa waulizao , ni kweli nilianguka:-(
Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket
Powered by beta.joggle.com




ASANTENI!
Hebu tumsikilize Aretha Franklin akithamanisha HESHIMA katika wimbo R.E.S.P.E.C.T