Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MBWA WEE PUMBAFU! MENO KAMA NGIRI!

>> Wednesday, August 30, 2006

Mbwa wee pumbafu!Sura kama nyau! Mama yako fisi!Huwa saa nyingine nacheka mwenyewe nikisikia matusi watu wanayotukanana. Cha ajabu ni kwamba mtu anakasikirika akitukanwa hivyo. Wakati kama wewe ni mtu haiwezekani ukawa mbwa ,fisi , nguruwe wala kitu chochote kile kingine.Usishangae nikicheka ukinitukana!

Read more...

MAPENZI, ASHIKI, NGONO , DINI , JINSIA na MTANDAO

Ukisoma kichwa cha habari hapo juu utajua tu kwamba ni vigumu sana kuweza kuingia kiundani mambo haya kwa kifupi. Kwasababu mambo yote yaliyogusiwa ni magumu na nirahisi kutafsiriwa kiaina nyingi. Jambo ambalo napenda kuligusia ni jinsi jamii yetu ya Watanzania inavyoguswa na mambo haya.KAVA LA KITABBU CHA KAMASUTRA


Mapenzi, ashiki na ngono ni mambo ambayo yameandamana na binadamu tokea enzi au karne na karne zilizopita. Ukiingia kwenye vitabu kama biblia au hata Kamasutra utakuta maswala haya yameongelewa karne nyingi tu.Na ukikumbuka mila zetu nyingi utagundua ni jinsi ganni yalivyo nywea katika fikira na mioyo ya jamii.

Kutokana na sinema za Hollywood ni rahisi kudhani kuwa maswala haya yako wazi sana katika jamii ya Marekani kuliko Tanzania.Labda kuna ukweli! Lakini kama hivi leo huo ni ukweli, utashangaa ni lini hasa watu walianza kuvunja miiko ya kuongelea maswala ya ashiki na ngono Marekani. Jamii ya Marekani ilistuswa na ripoti ya Dr Afred Kinsey hapo Marekani
ya kwanza ihusuyo tabia za wanaume katika ngono mwaka 1948 na ile ya pili ihusuyo tabia za ngono kwa wanawake 1953.
DR ALFRED KINSEY


Ukisoma habari za huyu Dakitari au hata kuangalia sinema yake utakuta kuwa mambo ya ngono kinamnakubwa yalikuwa hayaongelewi katika jamii ya Wamarekani. Sababu zilikuwa nyingi ,zikiwemo za kidini na za kijamii kwa ujumla. Ukimsikiliza Dr Kinsey atakwambia katika kipindi hicho alichofanya utafiti, ingawa mambo mengi yalikuwa ni mwiko hivyo hayaongelewi,bado, asilimia 62 ya wanawake walikiri kupiga punyeto na kufarijika ndani ya dakika tatu, asilimia 92 ya wanaume walifikia faraja kwa njia ya punyeto. 50% ya wanaume waliooa walikuwa wanapata ngono nje ya ndoa, wanawake asilimia 26 waliondoani wali farijika nje ya ndoa kabla hawajafikia miaka arobaini.Kwa ujumla anasema mwanamume mmoja kati ya sita na mwanamke mmoja kati ya kumi walio kati ya miaka 26 na 50 walikuwa wanafanaya ngono nje ya ndoa.

Kikubwa katika hili ni kwamba mambo haya yalifanyika kwa siri sana.Na kila mtu alijifanya hayajui au ni ukweli alikuwa hayajui. Katika kipindi hiki kumbuka bado kulikuwa na imani katika wanaume kuwa mwanamke hana ashiki na ngono kwake ni kitendo cha kumridhisha mwanaume na cha kutungishwa mimba.Cha kujiuliza ni kwamba kama jambo kama hili lilikuwa la ajabbu mwaka 1953 je miaka hamsini imetosha kuliweka wazi Marekani? Je likowazi Tanzania?

Dini zetu pia tulizoletewa zinatuchanganya sana. Utasoma katika kitabu hicho hicho ukakuta Mfalme Solomon alikuwa na wake mia nane halafu ukaambiwa kuwa kila mtu awe na mke mmoja. Dini nyingine ika kuambia unaweza ukaoa wake mpaka wanne halafu mafundisho yakakubana uwe na mmoja. Ukakuta sehemu nyingine unaambiwa ngono ni kitu kizuri , halafu ukakuta unaambiwa ni maswala ya uchafu sehemu nyingine. Yote hayo yasingekuwa ni kitu kama yasingekuwa yana gusa jamii zetu sana. Ngono uko uchina ikabidi ifundishwe upya maana watu walizidi, na sasa katika jamii yetu ya Waafrika mdudu unaangamiza.

Je ni kweli tunaongelea maswala haya? Je tunachunguza tabia za kikwetu zihusiano na maswala ya mapenzi ,ashiki, ngono na dini?

Matumizi ya mtandao yanakua Afrika. Mpaka nimesoma baadhi ya ripoti kuhusu matumizi ya mtandao kutafuta ngono Afrika. Mimi siamini kuwa bado tunaweza tukawa na ripoti za kuaminika kuhusu hili swala Afrika, hasa kwa kupitia utafiti unaozingatia matumizi ya mtandao.Kwa maana ni watu wengi Afrika hawajaweza kutumia mtandao au kuwa na kompyuta. Lakini kama kuna ukweli ndani ya mtandao, basi Watanzania nasi tumo katika watu waliobobea katika kutafuta ngono mtandaoni. Kwa ujumla bado ni nchi za kiislamu zinazoongoza katika kutafuta ngono mtandaoni.Watanzania inasemekana tunaongoza zaidi katika kutafuta ngono ya watu wa jinsia moja.Inasemekakana Wakenya wakifuatiwa na Watanzania wana google zaidi neno Gay Sex. Soma moja ya ripoti kama hizi hapa ambazo zinagusia mambo haya. Siwezi kusema kuna ukweli katika mambo haya , lakini ni jambo lisemwalo.

Katika kipindi hiki ambacho bado mdudu anaendelea kuua watu katika jamii na elimu ya ngono inafundishwa.Je tunaifundisha sawasawa? Je tabia kuhusu maswala ya mapenzi,ashki,ngono, dini, jinsia yako wazi? Mtandao ni muhimu lakini je wasoma habari mtandaoni wanashirikije kupeleka habari za kuhusu mambo haya katika jamii kwa ujumla?Mimi nadhani bado tuna usiri ambao utatuangamiza. Enzi ambazo mila za asili zilikuwa na nguvu kila kabila lilikuwa na jinsi ya kufundisha mambo haya. Hata kama kulikuwa na upungufu lakini maswala haya yalifundishwa.Siku hizi ndio twazidi kuchanganykiwa.Hata habari za katerero ni mara chache kuzisikia. Nafikiri inabidi kuliangalia swala hili kwa umakini tena.kwa maana sidhani elimu iwafaayo wa ulaya na marekani ni elimu ambayo inatufaa sisi. Naamini tuna hitaji njia ya kikwetu kutatua na kuelewa mambo ya kikwetu.Matthew chapter 5 (NLT)

27 "You have heard that the law of Moses says, 'Do not commit adultery.' 28 But I say, anyone who even looks at a woman with lust in his eye has already committed adultery with her in his heart. 29 So if your eye - even if it is your good eye - causes you to lust, gouge it out and throw it away. It is better for you to lose one part of your body than for your whole body to be thrown into hell. 30 And if your hand - even if it is your stronger hand - causes you to sin, cut it off and throw it away. It is better for you to lose one part of your body than for your whole body to be thrown into hell.


31 "You have heard that the law of Moses says, 'A man can divorce his wife by merely giving her a letter of divorce.' 32 But I say that a man who divorces his wife, unless she has been unfaithful, causes her to commit adultery. And anyone who marries a divorced woman commits adultery."


Be fertile and multiply; fill the earth and subdue it" (Gn 1:28)

Read more...

Swahili Time!

>> Monday, August 28, 2006Nimeipenda hii.Nashangaa kwanini imechukua muda hivi kuwa na saa inayoeleza muda kikwetu.Halafu ukiinunua unachangi mradi wa kamusi ya kiswahili.
Icheki hapa kwa maelezo zaidi.

Read more...

Je Waafrika tumeathiriwa na Stockholm Syndrome?

>> Friday, August 25, 2006

Kama vyombo vya habari havitudanganyi, basi ni kweli kuwa, katika makundi ya watu ambao wanawapenda watu wanaowanyonya na kuwaonea, Waafrika wanaongoza. Kuna hali ya kisaikolojia ambayo inajulikana kama Stockholm Syndrome ambayo inasababisha watu ambao wako kwenye kibano wawapende na kuchagua kuwa upande wa watu wanaowapa kibano.Hali hii ilipata jina kutokana kitendo kilichotokea hapo Norrmalmstorg, Stockholm , ambapo majambazi yalichukua mateka wafanyakazi wa benki. Pamoja na amjambazi kuwa ni ya hatari wale mateka wafanyakazi wakawazimia majambazi. Badala ya kutaka kujiokoa, wakawa wanawasaidia na kuwatetea majambazi hata walivyobaini kuwa wangeweza kuwatosa majambazi na kujiokoa. Kwa mtazamo wangu wa kila siku hii ndio hali ambayo bara zima la Afrika inalo. Tofauti ni kwamba nchi gani imechagua nchi za kiarabu na nchi zipi zimechagua nchi ziongozwazo na waulaya,marekani nk.Au unaweza ukaiangalia kuwa hawa majambazi ni kama hawa viongozi wetu Afrika ambao kwangu mimi ni sawa tu na hawa wageni ambao wanajinoma kutunyonya na kutudhalilisha.

Waswidi ambao walitekwa kwenye banki lakini badala ya kuwachukia majambazi wakawa wanawahusudu.


Pamoja na kujua kabisa kuwa tunanyonywa na nchi za nje, bado hupendelea mahusiano hayo kuliko kutetea kujijenga na kutengeneza mazingira ambayo tunaweza kucheza mchezo sawa na hawa wanyonyaji.Na kama hatuamki wenyewe hakuna hata haja ya kuwalaumu hawa watu kwa kujinoma katika kutunyonya. Huwezi kuamini eti mpaka leo Nigeria inaagizia nje mafuta yaliyosafishwa(refined), wakati yenyewe ndio nchi ya Afrika iongozayo katika kuuza mafuta ghafi nje.Huwezi kuamini mpaka leo asilimia karibu zote za mali ziuzwazo nje kutoka Tanzania huwa ni mali ghafi.Na si siri kuwa wote tunajua mali ghafi haina thamani kama bidhaa iliyo kamilika. Tanzania ukiachilia sangara ambao angalau wahindi pale ziwa victoria wanalipwa huwezi kusema kuna mali nyingine ambayo ni asilimia miamoja inatoka kama bidhaa iliyo kamilika.Sijui labda maua. Na kama sikoseiwafanyakazi wanaofanya kazi katika viwanda vya samaki Mwanza huwa hawana mishahara mizuri pamoja na kuwa mashirika yao hulipwa vizuri.Unaambiwa ni Botswana peke yake ambayo serikali inalipwa ipaswavyo na inaelekeza pesa kwa wananchi ipaswavyo Afrika.
Narudia, nadhani sisi Waafrika tuna Kastockholm Syndrome. Kama tusingekuwa nako, na kama ni kweli maisha ni magumu Afrika kuliko sehemu yeyote duniani je kwanini ni Waarabu wanaongoza kujilipua mabomu katika kudai haki zao?. Sawa utasema ni maswala ya udini. Kuwa ukijiua unapata tiketi ya first class kwenda mbinguni ambako kuna unono kibao, na kama mwanaume utapata mademu kibao mbinguni. Sasa utasemaje kuhusu Kamikaze Pilots wa Japan ambao walikuwa wanajiua kutetea nchi yao. Vile vile usisahau akina Tamil Tigers .Chini ya The Liberation Tigers of Tamil Eelam hawa watu wako tayari kufa nawe ukiingilia angazao. Hakuna cha kusema kuna mbinguni wala nini.

Mapailoti wa Kijapani wa Kamikaze

Bado naifikiria siku ambayo Waafrika watagundua adui yao na kupambana kama waarabu wajilipuao , watamil au hata mapilot wakijapani. Silaha za muafrika ni nyingi. Lakini fikiria ikiwa SILAHA KUBWA KULIKOZOTE KATIKA VITA HII ZIWE NI UMASIKINI, UJINGA NA MAGONJWA! Waafrika kila siku tunaongelewa katika kila televisheni duniani kwa umasikini wetu, ujinga wetu na magonjwa yetu . Sasa tukaamua haya mambo matatu ndio silaha. Kwanza kutokana na umasikini, itu halalishie kuwa hakuna mpango kuishi, lakini katika kujiua tunakufa nao mwanyonyaji wetu wanaotudhulumu. Kama wajinga basi hatujui thamani ya maisha yetu, lakini katika kufa tunakufa na wanyonyaji zetuwanao tudhulumu.Halafu kunakaukweli kuwa hatuthamini maisha yetu Afrika , kumbuka askari wanavyo tupiga marungu kila wakati. Kama wagonjwa basi tunajua kabisa tayari tuna kufa hivyo tuna chagua kufa na wanao tunyonya. Naamini hakuna nchi duniani haitataka kusaidi kutatua matatizo yetu Afrika baada ya muda mfupi tu tukianza kujiuanao. Na kwa maswala ya magonjwa hatuitaji hata kujilipua maana magonjwa tusifiwayo nayo Afrika nafikiri yana makali ya usuisado bomu kabisa.

Mwanamama Wakiarabu akiwandani ya fani
Naombea siku hii isifike!Naombea tuwezekuchukulia matatizo yetu kama changamoto ya kutuwezesha kugundua njia zetu wenyewe zakutatua matatizo yetu! Lakini najua ukimsakama mjusi sana hugeuka nyoka. Bado na kumbuka ile Tanzania bikira iliyouwa na matumaini angavu iliyosakamwa mpaka sasa imegeuka kuwa Tanzania ya majambazi, walarushwa, malaya nk.Lakini bado nina imani na Tanzania.Mungu ibariki Tanzania! Mungu ibariki Afrika!

Read more...

Chakula cha mawazo-Is U a Ni..er?

Mambo ya mfurukuto katika jamii kutokana na tofauti za Rangi,dini,jinsia nk huwa hayanichoshi hata siku moja.Ila haya ni mambo ambayo kila mtu hufikia majibu yake mwenyewe. Au mara nyingi walio wengi hupenda kuuliza tu maswali bila ya kuwa na majibu.Ila majibu ya maswali yetu tukumbuke kuwa ni majibu.Na katika majibu kuna mawili, unaweza ukapatia au ukakosea.Lakini kama binadamu kukosea au kupatia ni njia ambazo hutujenga. Leo ningependa kutoa chakula cha mawazo kwa kuwashirikisha Profesa Kamau Kambon ambaye anaamini inabidi tuwaue Wazungu wote kama moja ya dawa itakayosaidia kuokoa dunia.Cheki hotuba yake hapa.

Profesa Kamau KambonPia bila kumsahau Adolf Hitler ambaye naye alikuwa kafikia jibu kuwa kuwaua watu kama wayahudi, vilema, wasenge, majipsi au waromani na nauhakika watu weusi tungekatiza anga zake angetufyeka zaidi au kisawasawa kama jibu la maswali aliyokuwa akijaribu kutatua.Mcheki hapa akionyesha maringo yake


Adolf Hitler
Ningependa tujaribu kuendelea kutafuta majibu.Watanzania tuendelee kufikiria na tuendelee kujikosoa.

Read more...

Kitendawili?Tega. Kuna Nchi inayojidanganya kuwa ina amani na umoja.....Jibu ni ...

Sehemu zote nilizotembea utaambiwa Watanzania ni tofauti. Ni wapenda amani na wana umoja na sifa kemukemu hasa ukilinganisha na wananchi wa nchi nyingine za kiafrika.Utaambiwa Tanzania ni nchi yenye umoja na amani. Unaweza ukaamini kuwa ni ukweli, mpaka uanze kujichanganya kwenye jamii ya Kitanzania ndio utastukia kuwa mambo mengi ambayo yana sadikika kuwa yamekufa bado yananawili na yapo tu katika uvuguvugu ambao kirahisi tu yanaweza kulipuka.Utagundua Watanzania hawapendani.Husengenyana na kutaka kuvutana chini kama kawaida tu.

Kuna mambo mengi ambayo unaweza kuyapa uzito lakini kubwa ambalo linaweza kutoa kasheshe kirahisi Tanzania ni la udini. Hasa, ni vigumu kukana kuwa bado kuna vichokochoko vinaendelea kati ya Uislamu na Ukristo ndani ya Watanzania.Kama wewe ni mtu usomaye mablogu ya Watanzania utagundua hakuna habari itakayo changiwa na wengi kuliko inayo husu maswala ya dini hizi mbili. Mtu tu akithubutu kusema hoja yake ambayo inagusia swala la udini na linaloonyesha kuegemea katika dini moja basi lazima iwe kasheshe. Cha ajabu ni kwamba majadiliano mengi ya maswala ya dini humu katika Mablogu ya Watanzania hujaa matusi mpaka utaanza kujiuliza, hivi si ni kweli kuwa dini zote hizi mbili zinakataa maswala ya matusi?

Chakusikitisha ni kwamba asilimia kubwa ya Watanzania kwa mtazamo wengi, wana majina tu ya Kikristo au Kiislamu, lakini ni wachache tu ambao wanaweza kusema kuwa ni wanadini asilimia mia.Hapa nawaachilia mbali wale waliokuwa na bahati ya kuwa na majina ya asili ya Kitanzania wenye dini za asili. Lakini pamoja na kutofuata kikamilifu mafunzo ya Mtume na Yesu, ni rahisi kwa Watanzania kutukanana hata kupigana katika jina la dini hizi ambazo hata kutimiza sheria zake hawatimizi.Sasa ni nchi ya amani gani kama ina watu ambao wanaweza kupigana na kutukanana bila mpango? Kwa sababu kama unaweza kupigania kitu ambacho hata uhusiano wako nacho ni hafifu mimi naona ni vita isiyo na mpango.Siamini kuwa hata uko mbinguni utakwenda. Naamini kabisa kama ari hizi za kutetea dini tungekuwanazo hata katika kutetea haki zetu na hata kujenga nchi, tungekuwa mbali. Hivi Raisi JK kawapa kazi zenye wadhifa waislamu wangapi?Ni moja tu maswali yaulizwayo na hili litakuonyesha kuwa dini yako inakuweka katika kitengo fulani na kwamba udini bado unanguvu sana Tanzania.

Tanzania bado kuna ukabila sana tu. Dalili zake ni nyingi.Moja yapo ya dalili ni jinsi watu wanavyopenda kuchunguza nani anaajiriwa na kama anatokea kwenye kabila la bosi. Na ni kweli watu bado hupeana kazi kikabila, pamoja na mambo mengi tu. Sasa ni nchi gani ambayo ni ya amani yenye watu wamakabila yaliyochanganyika kila mkoa ambayo inaendeleza ukabila?Kwa maana hili ni jambo ambalo linaletamchafuko wa amani kirahisi kabisa.

Huko kwenye umasikini na kukosa elimu ndio usiseme. Kwa kukosa elimu sizungumzii kama ni kwenda shule tu. Maana mimi naamini kuwa unaweza kuwa umekwenda shule lakini ukawa hujaelimika. Umasikini unasababisha ukosaji wa amani. Unawezaje kusema kuwa nchi ina amani wakati kila mtu aliyepata kidogo anajenga fensi kuzunguka nyumba yake. Nchi yenye masikini wengi wasio shiba vizuri si nchi ya amani.Sijawahi kusikia mtu mwenye njaa akawa na amani hata rohoni mwake.Sasa mtu huyu hawezi akawa anachangia kuweka nchi iwe ya amani.Nchi si kitu bila watu. Na nchi yetu kama haitaweka misingi ya kuwa na wananchi walioelimika haiwezi ikawa ya amani. Maana mafanatiki wengi ni watu ambao wana zugwa kirahisi na mtu wanayemuamini bila kufikiri au kuwa na nguzo za kumuezesha kupata majibu binafsi. Raia walioelimika ndio pekee ambao wanaweza kufikiria na sio kufuata tu mambo na kuanza kuchinjana.Raia hawa watakuwa nauwezo wakuona picha kubwa na hatima ya hatua zao katika jamii na kwao binafsi.Mpaka sasa hivi elimu ya Tanzania kwa kiasi kikubwa haimuelimishi Mtanzania.Inamsaidia kupata digrii na ikiwezekana asilimiakubwa akiwa amekariri masomo. Hivyo siwezi kuiita nchi kuwa ina amani ikiwa elimu ambayo bado inatupa haituwezeshi kutujenga kujitatulia matatizo yetu binafsi na ya kijamii.Mfano haituwezeshi kujiajiri.

Nirahisi kuandika mambo mengi lakini bado naamini haya mambo manne tu, udini , ukabila, umasikini na kutokuelimika kumenifanya ni amini kuwa Tanzania amani tunayodai tunayo si ya kweli. Kinachofanya tujiamini tuna amani ni kutokana na kuzungukwa na nchi zilizoko ndani ya vita kabisa. Naomba tusijisahau na kudhani kuwa siye tumesalimika.Na vita ikitokea bongo itakuwa mbaya kuliko zote .Kwanza tumechanganyika.Mtaa mmoja makabila kibao halafu achilia mbali dini.Mungu ibariki Tanzania.

Read more...

Tanzania Kununua JET mpya lakini....

>> Wednesday, August 23, 2006

Naona inasemekana ile JET ya Raisi ilionunuliwa baada ya malumbano makali, imeonekana kuwa inasaidi kubana matumizi ya misafara ya Raisi. Hivyo imependekezwa inunuliwe Jet nyingine ili kuzidi kubana matumizi ya misafara ya Raisi.Habari hii hapa

Nisingependa kuiingilia habari hii ya ndege bado lakini ilinizingua kuona msafara unaobana matumizi ya nchi uliotokea kiwanja cha ndege kumuaga Raisi.
Dr Ali Mohamed Shein ,waziri mkuu Edward Lowassa, waziri wa ulinzi, Prof Juma Kapuya, waziri wa elimu, Prof Peter Msolla, waziri wa madini, Dr Ibrahim Msabaha, Waziri wa maji, Stephen Wassira, Utalii, Anthony Diallo , waziri wa nchi katika ofisi ya Raisi ,Kingunge-Ngombale Mwiru na kadhalika kadhaa. Hii imenikumbusha kile kipindi tulichokuwa tunatolewa mashuleni kwenda kujipanga Mabarabarani kumshangilia Raisi akipita. Labda walikuwa na kamkutano pale lakini ninamashaka na hili. Nahisi inawezekana lazima umchekee Raisi iliasije akahisi huko kwenye kambi lake kama huji kumchekea. Safari Njema Raisi!

Read more...

Mzee Jomo Kenyatta!

Tarehe 22 mwezi wa nane 1978, Afrika ilimpoteza Mzee Kenyatta. Kwa kujikumbusha tu nenda hapa

Read more...

Joseph Hill Wa Culture Afariki:-(

>> Tuesday, August 22, 2006

Du kwa wale wapenda reggae Joseph hill Kafariki akiwa katika ya tour Ujerumani. Mcheki hapa akikupa Ule wimbo I tried!

Read more...

Kwa Malenga wetu na wale wachekeshaji!

>> Thursday, August 17, 2006

Kwa sababu nisizozijua nimejikuta nafuatilia mashairi katika Def Poetry.Na huyu Black Ice amenisaidia kusikiliza hadithi za wamarekani weusi kutoka mtaani bila ya kusikiliza HipHop.Cheki moja ya kazi yake hapa .Nikakumbuka bongo tulikuwa na Malenga wetu radioni, sijui bado ipo? Hivi Malenga wetu imeingia katika Luninga Tanzania? Pia katika maswala ya wachekeshaji weusi wa Kimarekani nimerudi nyuma kwa wachekeshaji wazamani kama akina Richard Pryor.Ingawa huyu jamaa analalamikiwa ndio kachangia sana kusababisha waburudishaji weusi wawehuru kutumia neno Nigga. Cheki kipande hiki . Mwandani lini kitabu cha mashairi yako kitatoka?

Read more...

Are U Coloured?

Ilibidi nicheke mwenyewe baada ya kuona hiki kipande cha Daily Show. Kilicho nichekesha ni jinsi jamaa anavyojaribu kutumia hoja za Martin Luther King Jr kutetea hoja yake. Cheki hapa.

Read more...

Usenge na Ubasha ndani ya Tanzania ni Vitendo vya uvunja sheria lakini.....!

>> Monday, August 14, 2006

Siku hizi hasa jinsi teknolojia inavyonifanya nijikute sina maneno ya kiswahili ya mambo mengi, huwa ninajiuliza maswali kuwa imekuwaje kwa kiswahili tumeweza kuwa na maneno hata ya kutofautisha wanaopenda kulawitiwa na wale wanaolawiti wenzao. Nakumbuka kuna kipindi nilikatisha mitaa ya pwani na kusikia kabisa mtu akisifiwa kuwa yeye ni basha, lakini hapo hapo msenge huonekana hafai kuishi.Mimi huwa najiuliza inawezekanaje Basha akawepo pasipo na msenge? Sasa naona Tanzania tumepata na kesi ambazo zilivuma duniani za Mapadre au maaskofu kulawiti watoto wa watu wakiume. Soma hapa ujionee.

Chakusikitisha ni kwamba bado Tanzania watu hatuzijui sheria zetu zitulindazo.Ingekuwa Watu wangezijua sheria kama zijulikanavyo zile za uasherati basi ingesaidia hata kuondoa rushwa nchini.

Read more...

Rangi Nyeusi Nishai?Kutoka kwa Dokumentari ya Kiri Davies.

Nimebahatika kuicheki Dokyumentari ya Kiri Davies akiwa anawahoji wanawake weusi kuhusu Rangi ya ngozi.Inaonyesha kuwa bado katikati ya wanawake weusi bado nywele na rangi ya ngozi ni kitu kikubwa kibainishwacho uzuri.Cheki kidogo hapa uicheki kidogo hiyo dokyumentari.Inaitwa A Girl Like me.Nikakumbuka utafiti wa Kenneth B Clack ambaye alifanya mautafiti ya maswala ya rangi miaka iliyopita.Alipata umaarufu kwa utafiti wake wa mwaka 1940 uliojulikana kama The Doll Test.Ni mtu aliyechangia sana kuondoa ubaguzi mashuleni Marekani. Inasemekana tokea miaka hiyo mpaka sasa hivi watoto weusi huchagua doli la kizungu kuchezea kuliko jeusi la Kiafrika.Na huamini kuwa Wazungu ni wazuri kuliko Waafrika. Lakini sijui kama kuna ukweli katika hili maana sijui ni watoto wangapi wa Kiafrika wamwewahi kuwa na doli la Kizungu.Hivi documentary ni nini kwa kiswahili?

Read more...

Mmecheki Darwin's Nightmare?

>> Saturday, August 12, 2006

Nimepata link za documetary hii kutoka kwa washikaji . Kongoli hapa. Ukifika hapo utapata kuzipata sehemu zote za filamu hii.Iliozaa habari ifuatayo kwenye Nipashe.


2006-08-12 09:53:52
Na Namsembaeli Mduma, Dodoma
Wabunge wa Bunge la Muungano, wameiomba serikali iwakamate washiriki wote waliohusika kutengeneza au kufanikisha filamu ya The Darwin’s Nightmare(Jinamizi la Darwin), maarufu kama filamu ya mapanki, kufuatia uongo walioutumia katika sinema hiyo kuichafua sura ya Tanzania nje, pamoja na kuwadhalilisha Watanzania.

Aidha, imeombwa iwachukulie hatua kali za kisheria Watanzania wasaliti hao, pamoja na wahusika wengine, badala ya karipio tu, ili wawe mfano kwa wote wenye nia au watakaojaribu kufanya udhalilishaji kama huo ulioonyeshwa kwenye filamu hiyo, mara baada ya uchunguzi unaoendelea juu yao kukamilika.

Sambamba na maombi hayo, wabunge hao, bila kujali ni wa upinzani au chama tawala, wameitaka serikali iandae filamu mbadala itakayoonyesha uwongo uliotumiwa kwenye hiyo ya The Nightmare, ili kuuonyesha ulimwengu ukweli kuhusu Ziwa Victoria na biashara yake ya sangara, kwa kuwa asilimia kubwa ya yaliyozungumzwa ni uzushi.

Lengo jingine lililotajwa ni kuisafisha Tanzania kwa ujumla kuhusiana na kashfa hiyo nzito ya silaha, inayoelezwa kulenga kuiharibia nchi kwa mataifa mengine juu ya amani iliyoigubika.

Hoja hiyo ya kutengenezwa filamu mbadala, licha ya kuungwa mkono na wabunge karibu wote wa Bunge hilo, iliwasilishwa kwanza na Bungeni hapo jana asubuhi na Kambi ya Upinzania kupitia Msemaji Mkuu wao, Bw. Khalifa Suleiman Khalifa.

Aliungwa mkono kwa karibu na Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA).

Vile vile, hoja ya kutengenezwa filamu hiyo nyingine ya kweli ilisemwa Bungeni hapa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Bw. Johnson Mwanyika, wakati akisoma azimio la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu filamu hiyo yenye utata.

* SOURCE: Nipashe

Cheki mwenyewe.

Read more...

Siasa za Bongo zinavindumbwe vyake, lakini ukicheki Kongo sijui utasemaje!

>> Wednesday, August 02, 2006

Joseph Kasavubu

Raisi wa kwanza ambaye alimpiga vita waziri mkuu wake Lumumba ilakujikuta anapigwa chini na Mobutu.


Patrice Lumumba Tarehe May 11-25, 1960 alishinda uchaguzi uliowezesha yeye kuchukua uwaziri mkuu wa nchi .Hivi unakumbuka kuwa ni UN iliyokataa kumuokoa kutoka kwa majeshi ya Mobutu kutokana na amri kutoka makao makuu New York?
Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa za Banga alipindua tarehe 14,septemba 1960

Laurent Kabila. Aliyempindua Mobutu Mei 1997.

Joseph Kabila mtoto wa Dar au tuseme Mbeya? Alichukua nchi tarehe 26 January 2001 mpaka kwenye uchaguzi huu wa Julai 30,2006.


Nzanga Mobutu . Mtoto wa mke wa pili wa Mobutu atakaye kuila nchi tena.
Haya inavyoonekana bado Kabila na Mobutu wamo katika siasa za Kongo. Siasa zetu Afrika zinahitaji ukarabati wa hali ya juu. Afadhali Tanzania viongozi bado wanang'atuka bila vita. Lakini wanapeana ulaji katika staili ambayo hatuwezi kubadilika au kuendelea kwa kirahisi. Haya tusubiri matokeo ya mwisho. MUNGU ibariki AFRIKA!

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP