Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jana APRILI tarehe MOJA - yasemekana ilikuwa NI siku ya WAJINGA!Leo JE?

>> Monday, April 02, 2012

Bado kidogo niitukane siku JANA,...
.... kisa kila nilichokuwa nasikia hata cha KWELI ,...
.....ilibidi nijiulize  MARA MBILIMBILI hivi hiki ni kweli au ndio nafanywa MJINGA!

Swali:

  • Hivi JANA ilikuwa siku ya KUDANGANYWA au ya WAJINGA hasa ukizingatia vingi vihusianishwavyo na hii siku ni UONGO uliotungwa MAKUSUDI?
  • Kwani MWEREVU akidanganywa maana yake ni MJINGA?


Kwa bahati mbaya,....
.... leo bado naegemea kwenye WAZO kuwa,....
....WAJINGA walikuwepo, WAPO na WATAKUWAPO,.....
... kitu kinifanyacho hasa baada ya kuangalia maswala tutendewayo na tutendayo kama BINADAMU,....
... labda kila siku ni siku ya WAJINGA!

Swali:
  • Unauhakika WEYE ni MWEREVU tu na ni akina Simon Kitururu tu  ndio WAJINGA?


Ndio,....
.... labda kwa bahati MBAYA ,....
.... UJINGA bado  ni UBINADAMU tu !:-(
Nawaza tu!
Jumatatu NJEMA Amigos!


Hebu tubadili kwa kupata moja ya mtazamo kuhusu-The History of April Fools Day

 Halafu sijui kwanini ila hebu The Temptations warudishe tena -Shakey Ground
Au na baridi hili niote tu ya Kool & The Gang katika - Summer Madness

 

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:50 pm  

nanukuu "Ndio,....
.... labda kwa bahati MBAYA ,....
.... UJINGA bado ni UBINADAMU tu !:-(" mwisho wa nukuu...mimi siamini kama kuna WAJINGA

Simon Kitururu 4:51 pm  

Mie naamini WAPO!:-(@Yasinta

Yasinta Ngonyani 8:14 pm  

NANUKUU" Swali:

•Unauhakika WEYE ni MWEREVU tu na ni akina Simon Kitururu tu ndio WAJINGA?" RUKSA KUAMINI MUTU WANGU ILA MIMI NAAMINI WEWE SI MJINGA.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP