Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

EU inasherehekea Miaka 50 .......

>> Saturday, March 24, 2007


Wakati wa Ulaya(EU) wanasherehekea miaka 50 tokea Triti ya Rome kupigwa sahihi, mimi nashindwa kujizui kuwakumbuka akina Kwame Nkurumah ambao nao tokea mbali waliwaza na kujaribu kuunganisha bara la Afrika. Waulaya imepita miaka hamsini angalibado wanajenga himaya yao. Tukikumbuka hawa ndio waliokuwa na ambao wamechangia sana kutugawa Waafrika mpaka leo hii bado wanajenga muungano wao. Hivyo naamini kabisa inawezekana kuwa Afrika pamoja nayote yatukabiliyo ni jambo zuri tu tumefanikiwa angalau kulitunza wazo la muungano wetu. Mimi naamini sisi tunahitaji sana kuungana hata kama si kwa staili ya hawa wa Ulaya. Tunahitaji kuungana ili kusaidiana kuokoa vizazi vyetu vya watu weusi vijavyo kunyanyasika hapa duniani.
Jumamosi nyema!
Duh !Lakini unamkumbuka Abeti Masikini?

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mjengwa 10:40 pm  

Simon,
Umenikumbusha mbali, Abeti Masikini!
Kazi nzuri!
/Maggid

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP