Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Adhabu!Duh!

>> Friday, June 08, 2007

Hivi....!

  • Wale mapailoti wa kijapani wa kamikaze ambao walirusha ndege kwa dhumuni la kujiua nazo, unafikiri nafasi ya kifo kwao ilikuwa inachukua nafasi gani?
  • Hivi Mkwawa alipojiua iliasishikwe na Mjerumani unafikiri yeye adhabu yake kubwa ilikuwa ni kushikwa namjerumani au kifo?
  • Hivi hawa wadau wanaovaa mabomu na kujiua kwa ajili ya dini , unafikiri ukiwakamata kabla hawajajiua utawapa adhabu ya kifo?
Ndio , hili swala si rahisi sana.
Lakini mimi naamini kuwa kila mtu anakakitu kake kamuumizako zaidi.

Kabla sijaongea sana......
Duh !
Huyu Harry Belafonte na Nat King cole

Lakini baadhi ya picha za jana.....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Memba
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Memba eeh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Memba kutoka Senegal na Joha kutoka Gambia
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Lakini....

Hakuna binadamu wawili waliosawa. Ila cha ajabu ni kwamba binadamu wanachaguo dogo la maneno , kiasi kwamba, katika kuelezea uwiano wa watu , imefikia kushindwa kukwepa kutumia sentensi kama binadamu wote ni sawa.

Nakubali kuwa kiunganishacho binadamu ni ubinadamu.Ila safari ya ubinadamu kila binadamu huipapasa kivyake.

Nilipomsoma Mwandani , alipokuwa akichambua RUSHWA=KIFO, nilishindwa kujizuia kuwaza kwa mara nyingine tena na tena ,maswala ya adhabu kwa binadamu.Nikakumbuka kipindi fulani , jinsi mwalimu fulani alivyokuwa anapenda kutupa adhabu za push ups na kichura. Kwetu wengi ilikuwa ni kweli adhabu, lakini kulikuwa na rafiki yangu Victor Lukoo , mara nyingi hizi adhabu kwake yeye ilikuwa ni zoezi tu. Kusema ukweli yeye nafikiri kipimo cha adhabu kwa mtazamo wa mwalimu kilikuwa hakifikii jinsi yeye mwenyewe alivyo kuwa akijifua nyumbani na mazoezini. Huyu jamaa alikuwa ananipigia push ups mpaka naacha mwenyewe kuhesabu. Kichura usiseme! Namkumbuka pia na mshikaji wangu mwingine, Peter Msimbe, naye alikuwa na mchezo wa kupiga zoezi mpaka unajiuliza kuwa kama kweli inamanufaa kiafya kweli? Sasa hawa jamaa adhabu fulani ukiwapa kama hizi za kutumia viungo ukafikiri umewapa adhabu , unajisumbua.

Duh !
Kabla sijaendelea, ngojea nikupe baadhi ya picha za jana zaidi....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Clemoo mtoto wa Nairobi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Hashim
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Victor mtoto wa Nairobi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Victor
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Victor eeh?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Gibson Mzee wa Nairobi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Gibson eeh?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Ronaldo ,Mzee wa London
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mzee wa London na Mimi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Elvis!Duh! Mzee tukopamoja!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Charles , Mzee wa Lusaka
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Abdi ,Mzee wa Dakar
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tidjan na ...
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi na Erick ze Producer
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Ben Mzee wa usafiri!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
....Na Dosky
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Njau na Mkuu wa Kikao

Duh!

Halafu Richie Spice aliimba kuhusu watu wa rangi za kahawia kitu kilichomfanya alaumiwe na watu wengine kwanini hakuimba watu weusi...
Hebu msikilize.....

Lakini.............

Utotoni , nilipitia adhabu za viboko , kufinywa nk. Lakini hakuna adhabu na kitu kilicho kuwa kinanitesa kama kumsikiliza mama akilalamika kuhusu vijambo nilivyokosea. Mama yangu yeye alikuwa hana mchezo wa kuchapa, kufinya wala kitu kama hicho, ila ana namna ya kusema ambayo ilikuwa inaniingia sana. Baba yeye alikuwa anatabirika.Ulikuwa unajua kabisa hii leo ni viboko tu!Cha ajabu ilikuwa kwangu ni rahisi kukubali viboko halafu yanaisha, kuliko kusubiri kuwekwa kikao na mama.
Majirani zangu walikuwa Waitaliano ,Ivan , Chesko na Simone. Hawa walikuwa wanapewa adhabu ya kutoruhusiwa kucheza nje au kutochezea matoi fulani.Ikibidi wanawekwa kwenye kona fulani ya nyumba kwa muda fulani. Hizi adhabu zilikuwa zinawaingia kweli, kitu ambacho kwa wengine kinaweza kuwa si adhabu kabisaaa!

Mimi nafikiri adhabu inakuwa adhabu iwapo mtu apewayo hiyo adhabu atatesekanayo au itamsababishia kuwepo katika hali asiyoridhika nayo. Kwa hiyo ukimpa mtu adhabu hakikisha kuwa ni adhabu kweli. Kakitu udhaniako ni adhabu kutokana na wewe mwenyewe kuingiza mitazamo ya maisha yako na kufikia maamuzi kuwa kikuadhibishacho wewe basi kinamuadhibu kila mtu, hapo unacheza hola.

Duh!

Haka kawimbo ka Richie Spice na wenzie kamenikaa kichwani lakini!Hebu kasikilize....

Lakini.....
Cheki picha za jana zaidi....

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Martin
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Martin eeh?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Njau, Martin, Mkuu wa Kikao aka Raymond na Mimi
Au..
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Siongezi picha nyingine, nimestukia hiyo!Lakini tuko pamoja!

Lakini haka kawimbao aliko katunga Michael Jackson na Lionel Richie unakapenda pia?

Au ni adhabu?

Hebu kasikilize...............

Swali:
Hivi ukimnyonga mtu au kumuua, unafikiri ameadhibika?

Si kafa tu?

Au?

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 2:22 pm  

Asante kwa Belafonte ...nimeridhika...ingawa nitausikiliza tena kesho ,kesho kutwa, mtondo, mtondogoo..kama sijapewa adhabu:)

mwandani 2:34 pm  

Sikujua kama unatembea huku umebeba mtambo wa kunasa picha. Endelea kubeba na kunasa zaidi.

Kweli unayosema juu ya adhabu, kuna watoto manunda kama 50 hivi ambao wanatetemesha sana mji wa Adelaide. Wao wanaiba magari halafu wanagonga maduka ya dawa au ya pombe, milango ikivunjika wanaiba pombe na sigara au viungo vya madawa ya kulevya.

Kutokana kwamba wengi wako chini ya miaka 18 hawafungwi jela wanapelekwa tu kwenye chuo cha mafunzo kwa mwaka au miaka miwili halafu wanatoka. Na wakitoka wanaanza tena. Sasa hawa watoto hawaogopi kufa wala jela. Imefikia wakati serikali ya hapa haijui nini cha kuwafanya... wanadai wazazi wapewe sapoti mapema ili kuepuka kukuza wahalifu wa namna hii.

Simon Kitururu 6:38 pm  

@Serina:-)
@Mwandani:Kusema ukweli ni ngumu sana.Kuna watu wengi wanapewa adhabu wasizo stahili;wengine wanazidishiwa na wengine wanapewa ambazo hata hawahisi ni adhabu

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP