Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Lewis Hamilton na ......

>> Saturday, June 16, 2007

Michezo ni kitu fulani ambacho watu weusi wanasifika sana ulimwenguni!Lakini ukweli ni kwamba hata katika michezo watu weusi wasifikaonayo leo , wameingia au kuruhusiwa kuingia katika michezo hiyo juzijuzi.

Mpya mwenye weusi ambaye amefungua njia katika mchezo tofauti ni
Lewis Hamilton

Swali:
Hivi lini tutakubalika katika maswala mengine zaidi ya burudani na michezo?


Duh!
Kunakale kawimbo ka Angelique Kidjo na Nile Rodgers



Je, ukiwaacha akina Mandela ,watu weusi kama akina Philip Amagweali walioko katika fani nyingine na akina......wataanza kuwa jina lililoko midomoni mwa wadunia lini?

Kwa wafuatiliaji wa michezo na wafuatiliaji wa maendeleo ya watu wa rangi wafunguao mipaka katika anga nyingine.

  • Lewis Hamilton ndio dereva wa kwanza wa Formula one aaminikaye ambaye ni Mweusi.
Akiwafuata akina Tiger Woods, ambaye hata baada yakujitetea sana kuwa yeye si mweusi, Wazungu wanamuona mweusi tu.
  • Jack Robinson, ambaye alifungua mlango kwenye baseball.
  • Na wengine kadhaa waliofungua milango katika michezo mingine.
Bila kumsahau Bill Lester ambaye kafungua mlango katika NASCAR ,mchezo wakuendesha magari mwingine ambao watu weusi hawajaweza kujipenyeza.

Duh!
Swali: Hivi mchezo wa nguti,kidali na mdako nani alianzisha?

Lakiniiiii......
Michezo mingi haijulikani nani kaanzisha.
Ila Basketiboli ambayo imewapa jina watu weusi hasa Marekani , ni miongoni mwamichezo mipya ambayo ni wazo la mtu mmoja.

Nishawahi kumuandika huyu James Naismith aliyebuni mchezo wa Basketball kipindi fulani.

Duh!
Ushawahi kubuni kamchezo hata kama ni kasiri?

Mimi mwenzio sijawahi!
Duh!
Noma!
Swali:
Hivi kwa nini Wazungu wanaamini yeyote mwenye tone hata moja la damu ya mtu mweusi ni Mweusi?

Wewe unafikiri Lewis Hamilton,Tiger Woods, Baraka Obama, Malcom X, Spike Lee, Jerry Rawlings, ........Maria Sarungi ........ni weusi?


Samahani lakini kama nakukwaza!

Wikimwisho njema!

Wapate Chic!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP