Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kati ya Maisha na Kifo!Duh! Unataka kuishi mileleee eeh?

>> Monday, June 04, 2007

Duh!
Kifo nishai!

Inasemekana kuwa watu hawataki kufa kirahisi!
Inasemekana kuna watu wengi wanafuata dini kadhaa ili kuogopa wakifa wataenda Jehanamu!

Duh!

Swali:
Unafikiri ukifa sasa hivi utaenda wapi?


Kuna watu nasikia wamefikia kukana kila kitu na kajeuri kao kanaongozwa na tishio la kufa, na ni nini wamefikia kuwa ndio hitimisho wakifanya , basi wameponyeka.

Swali:
Hivi maalikaida, wanafikiaje uamuzi wa kujisikia kufakufa kwa ahadi ya mabikira kadhaa na maisha ya milele?

Nisikutishe !Labda na mimi nataka kuishi milele !

Sasaaaa.....

Akili ya binadamu inamipaka!
kuna kisehemu inafikia kuwa hakuna majibu fulani!

Unaweza kubisha... , lakini PoPu Benedikiti anabunia, Ayatolah anabunia.. Mzee Changeremba naye anabunia kuhusu maswala ya baada ya kufa ni nini kinatokea.
Na haka kaubongo tulikonako kazuri kweli kwa kujaribu kutupa majibu au kale kaahueni kakufikiri kuwa heri mimi , pamoja na kuwa na mashaka lakini nili................

Duh!

Nisikufiche!
Hii topiki kubwa!

Ila.......!

Swali:
Unajua unaweza kufa leo?

U
mefanya nini?Unataka kufanya nini? Ukifanya hivyo ndio itakuwa nini? Ikishakuwa hicho kitu ndio maana yake nini?

Duh!

Ngojea niulize tena!


Huko unakotaka kuishi milele ukisha fariki,unauhakika huta boreka?

Duh!
Samahani kwa kuuliza hivyo kwa sababu najua mimi na wewe hatuna jibu.

Sasaaaa..................!

Nawaza tu!
Maisha magumu vilevile! Na usipoangalia ndio kwanza unakufa wakati huja jinoma!


Hivi tunatakiwa tujinome kabla hatujafa eeh?
Na wale wanaozaliwa na kufa tu baada ya kasorobo je?
Na wale wengine waliofariki kabla...........?


Duh!

Kifo kigumu!
Ndio maana kuna baadhi ya watu wananiambia kuwa kila mtu anataka kwenda mbinguni lakini hataki kufa!

Duh!
Mbinguni inasemekanni ni kuzuri!

Ndio maana kila mtu akiambiwa achague Mbinguni na jehanamu anachagua mbinguni!

Duh!
Si inasemekana mbinguni kwa akili za kibinadamu hatuwezi kupaelewa?
Si inasemekana jehanamu kuna moto kisawasawa na lugha hii ya kibinadamu ya kututisha tunatakiwa kuielewa?

Duh!

Bado naandika maanayake niko hai!
Bado unasoma maanayake uko hai!


Lakini............................!
Lakini...............................?


Kama unakampango ka kwenda mbinguni uielewayo, kafuatilie!
Kama huvutiwi na kaaidia ka mbinguni kapewako kipaumbele sasa hivi, mbele kwa mbele!

Lakini matalibani na washikaji kadhaa huwa wanaanza kinamna mapema hata kabla hawajaitwa kisa ahadi fulani za kidini!

Sasa?


Maisha na Kifo! Kifo na Maisha nivikitu fulani navifikiria leo!

Sasaaaa!
Samahani na kuzingua!
Kama mdini si utubu tu halafu subiria?
Au!

Naongelea hili swala katika namna unayoweza kufikiri natania.Unaweza kuwa unafikiria nafanya mzaa! Unawezaku.....

Hili jambo liko mawazoni!Wewe haliko mawazoni kwako?

Duh!
Kama haliko mawazoni kwako wewe bomba!


Lakini.............!


Duh!
Nakuacha na baadhi ya picha za jana baada ya Shoo ya Macy Gray


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Sudan na Somalia

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Alice

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
mkuu wa kikao na mimi

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Momocat na Aliko

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mr DJ
Nakuacha na Malaika

Duh!
Nilikuwa naongelea kufa kufa, ila nimekosa wimbo fulani utuunganishao ....nawaachia waaminio katika yesu hiki kitu cha Rose Muhando kiitwacho Yesu na kupenda!

Wengine tuendelee na Prince....Akikupa BLACK SWEAT(Jasho Jeusi)

Siku njema! Baadaye basi!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Serina 3:03 pm  

Eldorado hapa duniani...wanaoamini watrudi duniani lakini kwenye mwili mwingine je? Kifo lazima...lakini si kitu cha kuweka mawazoni kila siku..labda utakapofikia ukongwe na ushachoka na ya dunia...siku njema!

luihamu 7:43 am  

Mzee Au,

Nimesema mara kwa mara,kifo nilazima kitokee kwa binadamu,mnyama,mimea na n.k.

Muda wako au wangu unapofika mwishao wa kuishi katika hii dunia iliyoo jaa UFISADI,MAJIGAMBO,ULAFI,NGONO,MAJUDA ISKARIOTI,UZINZI,PRETENDERS,MURDERERS NA N.K

Muda unapofika tamati basi binadamu anakwenda kuanza maisha pahali pengine nikama Transformation moja kwenda nyingine na huko hakuna mipaka ya inchi tofauti tofauti.

Mimi naamini nikiondoka leo au nikifa leo nakwenda kukutana na Haile Sellasi I,Robert Nesta Marley,Peter Tosh na wengine wengi so its just a matter of time.

Nashangaa kuona jinsi gani binadamu anajishuhulisha kujenga majumba ya kifahari.

Jah Rastafarian.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP