Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNAKUMBUKA ULIPOANZA KUPENDA?

>> Thursday, June 14, 2007

Duh!
Samahani!

Nafikiri nilitaka kuuliza hivi:

  • Unakumbuka ulipoanza kuchukia?

Inasemekana watu wengi hukumbuka walipoanza kupenda kuliko walipoanza kuchukia, lakini wanachukia kirahisi kuliko kupenda.

Duh!
Kabla sijaendelea.....
Haka kawimbo ka New Edition enzi hizo...


Si unajua tena!Historia ya kupenda inasemekana ni rahisi kuikumbuka au hata kuiimajini kuwa tunakumbuka. Si unajua tena vile vimaswalaa....!:

  • Wengi wetu cha kwanza kupenda ilikuwa nyonyo ya mama.
  • Kupenda kale kadoli!
  • Kumpenda rafiki fulani pale utotoni!
  • Hata kale kamwanzo kakuanza kumpenda mwanadada fulani au mwana kaka fulani.......
  • Nakadhalika kadhaaa wa kadhaa.......
  • Kupenda msosi fulani!
Duh!
Hebu nikukumbushe kale kawimbo.....


Lakini ukweli ni kwamba moja ya tendo la binadamu alifanyalo akizaliwa tu, ni kuchukia.
Akizaliwa tu halafu yuko hai , atalia kuashiria kuwa kashastukia bughudha za ulimwengu.Kachukia kakitu ambako siye tumekazoea!

AU?

Unajua tena!Inawezekana anastukia:
  • Kikwapa cha wadau walio mzunguka
  • Hali ya hewa chafu
  • Au machale tu yamemcheza kuwa duniani starehe ni pale tu ujuapo tabu.
Duh!
Nisikufiche , sijui nini kinamliza mtoto anapozaliwa kwa sababu mimi mwenyewe sikumbuki nililizwa na nini!

Duh!
Ushastukia kuwa ni jambo la kufurahia mtoto aliapo wakati kazaliwa tu?
Akiendelea kulialia miezi yote mingine wadau walewale waliofurahia kilio cha kwanza hawafurahiii tena.

Swali:
Hivi huwa unafurahia mtu wako fulani akilia?

Nafikiri sie wanadamu tunajizoesha mambo kibao ambayo yanafanya tupende hata ambavyo tusingependa!Machale ya mtoto azaliwapo tunayaua kwa kujizoesha mambo ya dunia.
Kama uwiano katika dunia wa vipendwavyo na vichukiwavyo ungekuwa vingine , nahisi isingeshangaza mwidu kwa kamasi za ngombe adimu ingekua chakula cha kwenye Kitchen pati na harusi , halafu kuku kwa pilau chakula cha wafungwa bongo.


Usitishike ni mtazamo tu!


Duh!

Basi ngoja niseme uwiano wa vipendwavyo na vichukiwavyo ungekuwa vingine:
  • Waafrika wengi wangependa wowowo ndogo halafu Wazungu wengi wangependa sangara wakubwa.
  • Waislamu wangekula nguruwe na wa hindu nyama ya ng'ombe
  • Papa Benedicto angekuwa anahubiri kuleta rushwa hala viongozi waafrika wangekuwa wanaongoza kumpinga kwa kukataa rushwa
Duh!
Nakuzingua!
UKWELI NI KWAMBA , NILITAKA KUSEMA UWIANO UNGEKUA VINGINE, BINADAMU ANGEPENDA ZAIDI BINADAMU MWENZIYE, ANGEPENDA AMANI!

Duh!
Kuhusu hili swala la uzoefu .....
Ngoja nimuache Mr Ebo akuulize kama wewe Mbado?



Sasaa...
Nachojiuliza ni kwamba ...
Kama uzoefu wa kuchukia tunaupata kuanzia tuzaliwapo tu ,unafikiria una nguvu zaidi ya uzoefu wa kupenda tuupatao baadaye, baada ya kupewa nyonyo?

Nisikuzingue! Lakini ukweli ni kwamba mara nyingi tunasahau jinsi gani uzoefu wa kupenda na kuchukia tumetoka nao mbali, na kila siku tunaufanyia mazoezi.

  • Nafikiri ukifanya mazoezi ya namna fulani kwa ajili ya namna fulani, si ni lazima uboreshe hiyo namna fulani?

AU?


Sasaa....!

Hiyo namna fulani yako ni chuki au upendo?
Kabla sijamalizia.....Ngoja nikukumbushe JUMUWATA!




Nakuacha na Orishas wakikupa 537-Cuba

Tusisahau basi kufanyia mazoezi hii sanaa ya kupenda!
Kwa maana kwa mtazamo wangu ile sanaa ya kuchukiana imeshamiri sana!Halafu Afrika inatugawa sana kiasi kwamba mpaka tunachekesha!
Tuko pamoja!


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 7:07 am  

Mzee Simon blogu yako ni moto wakuotea mbali,hiyo picha duh.

Mzee Simon naomba unielekeze jinsi ya kuweka baadhi ya magazeti tanda katika blogu yangu,napata shida sana,lazima nianze kwa Da Mija kisha nije kwako na kuanza kutumia blogu yako wakati wakuchaguwa magazeti tando.

Mpe tough Rasta basi.

Nuff Nuff Respect.

Chikiness 12:07 pm  
This comment has been removed by the author.
Anonymous 12:08 pm  

Simon, ningelikuwa mtanzania, kura yangu ungelipata..lakini tena...tusienda huko:)
Chuki huzaliwa kutoka mapenzi, mpende adui..lakini adui ni nani?

Simon Kitururu 7:34 am  

@Rasta:sijui template yako ikoje kwa sababu sina uhakika na jinsi MK alivyo itengeneza. Kwangu mimi niki sign in na kwenda kwenye template , kinacho fuata nabonnyeza edit sehemu ambayo nina links. Naweka link nayoitaka na Jina la Mtandao wake basi imetoka.

Nafikiri itakuwa rahisi ukimuuliza MK, Miriam, Msangi Mdogo au wadau wengine waliobobea katika Tekelinalokujia. Kwangu ujuzi wa teknolojia mdogo sana. Huwa najua nacho kihitaji tu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP