Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Unamjua Sunday Adelaja?

>> Wednesday, October 25, 2006

Pastor Sunday Adelaja akishusha kauli katika kanisa lake la Embassy of the Blessed Kingdom of God for all Nations.







Katika Wanageria ambao nimewasikiliza hivi karibuni huyu Sunday Adelaja ni jamaa ambaye amenifikirisha kidogo siku za karibuni. Huyu Mnigeria ni miongoni mwa Wanageria waliofanikiwa katika biashara ya dini hivi sasa. Akiwa Ukraina , aliaamua kuanzisha kanisa ambalo kwa sasa hivi lina watu zaidi ya 20,000. Anachonizingua ni jinsi alivyoweza kuanzisha kanisa katika mazingira magumu kama ya Ukraina hasa akiwa Muafrika. Ubaguzi katika nchi zilizokuwepo ndani ya Soviet Union ni mkubwa mara nyingi zaidi ya zile za magharibi. Halafu mifumo ya nchi hizi ni dhaifu hivyo ni vigumu kwa wageni kupata usalama. Kwa hilo tu, naweza kumvulia kofia kwa kuweza kutumia udhaifu huo huo na umasikini uliozidi baada ya kuvunjika kwa Soviet Unioni kusimama kivyake. Kuhusu ukweli wa kanisa lake,hilo mimi sijui. Changamoto anayonipa ni kuwa penye nia pana njia.

Hivi hili hapa chini ni kweli? :
"Nigeria's Christians have a prophetic mandate," says Matthew Ashimolowo, a former Muslim who now leads England's largest church, the Kingsway International Christian Centre in east London. "God gave us a prophetic word that his servants will go out from our nation and shake the world." The 15,000-strong Word of Faith Bible Church, Ukraine's largest church, was founded by Sunday Adelaja, also a Nigerian, and the largest churches in Kenya, Tanzania, Ghana, Zimbabwe and Jamaica are also led by Nigerians.

Read more...

Chakula cha mawazo!

Hivi tutawalalamikia Wazungu na Waasia kwa kutunyonya na kuendelea kutufanya watumwa mpaka lini?Mwanzo tulisema kuwa hatukuwajua hawa watu na hila zao.Sasa asilimia kubwa ya wasomi wetu ambao wamewasoma hawa watu wanajua hila zao.Sasa tunafanya nini na ugunduzi huu wa hila zao? Tunafanya nini kukabiliana na mifumo yao ambayo sasa hivi tunao wasomi wengi tu Afrika waliobobea katika taaluma za mifumo yao?Hivi wasomi wetu wa Afrika walio wengi siku hizi si wamesoma shule hizi hizi za hawa wamagharibi waongozao nchi hizi?Hata akina Sumaye , Malima nk si baadhi tu ya hawa ambao vikorido vya vyuo vikuu kama Harvard, nk, wanavijua kama nyuma ya viganja vya mikono yao?

Sasa swali ni kwamba, kama tunajua wanafanya nini hawa wamagharibi kwanini tunashindwa kujikwamua au hata kuwa na laghai zitakazotufaidisha sisi?Wachina walivyostuka wakaamua kubadili mtazamo na kutumia mpaka laghai ilikujifaidisha.Wajapani, Wakorea nk walifanya laghai kulingana na mazingira yao.Sasa sisi je?


500 YEARS LATER: AFRICA AND SLAVERY Dr Kimani Nehusi akilalamika.Nakubaliana naye lakini najiuliza hivi tutafanya hivi mpaka lini?

Read more...

Behewa la mawazo: kwa nini Tanzania imechelewa kufanikiwa?...-N.1

#UTAIFA
Naamini Raisi Nyerere na uongozi wa kwanza ulibidi kutumia muda mwingi kujenga utaifa.Kuweka misingi ambayo ingeweza kutufanya taifa.Lugha ya kiswahili na kujenga mfumo mzima ambao ungetuwezesha kujiendesha kama taifa huru.

Swali: Je, Utaifa tunao hivi sasa?Kama tunao unatuweka katika nafasi gani nzuri ya kuendelea mbele kupita mataifa mengine ya jirani ambayo hayana Utaifa?Je kama Nyerere alikuwa anatumia baadhi ya muda kuhakikisha maswala mbalimabli ya utaifa yanaendeleaje akiwa chini ya upungufu wa viongozi wasomi, je, Raisi wa leo anatumia muda huo kufanya nini ikiwa idadi ya wasomi imeongezeka kupita ya kipindi cha Nyerere? Je , wasomi wetu wameelimika au wamekwenda shule tu na kuwa na vyeti babu kubwa?

Usistuke kama unasoma hapa maana yake uko ndani ya treni ya mawazo.
Katika behewa hili namba moja najiuliza tu kwamba kama utaifa ulikuwa lazima kujengwa hivyo lazima muda ulitumika kuujenga.Hii inaweza ikawa sababu ya kuchelewa kuendelea. Sasa kama huu utaifa umejengeka basi muda huu ni wa kuutunza Utaifa na kuutumia Utaifa wetu kama chanzo kimojawapo cha kwenda mbele.Je, mikakati ya nchi yetu inatumia faida zote ziletwazo na utaifa? Najaribu kufikiria kwanini tunajisifia sana Watanzanina kwa amani wakati sioni kama amani imetusaidia sana kupiga hatua kimaendeleo? Ukiwa unawasikiliza watu kama akina Jared Diamond, hasa katika kitabu chake cha Guns, Germs and Steel, utamsikia akikueleza ni jinsi gani Wazungu waliweza kufanikiwa . Atakupa jiografia, atakupa jinsi hata uwezo wa kugundua kilimo , kufuga wanyama mapema kulivyowezesha jamii mbalimbali duniani kuendelea mapema na kutawala nyingine.
Sasa hayo yalikuwa zamani lakini kikubwa ni kwamba jamii zote zilizo piga hatua ziliweza kutumia faida zilizoletwa na mambo ambayo wameyamasta tayari. Je sisi kama Tanzania na utaifa wetu na amani yetu , tumepungukiwa nini sasa hivi ambacho kinatufanya tusiwe Taifa lililofanikiwa kufaidika na yale tuliyoyamasta tayari? Mapungufu yapo, lakini tunajifunza nini kutokana na mapungufu hayo?Kwanini tokea enzi hizo za uhuru mpaka sasa bado tunazungukwa na magonjwa,mfumo dhaifu wa elimu,mfumo wa uongozi hata mori mbaya wa kazi?

Sasa siri ya kutatua jambo hili ni nini? Je, ni mpaka Taifa zima lielimike ili tuweze kuwa na mabadiliko?Je, hivi historia inatufundisha kitu kweli?

Naendelea kusafiri katika Treni hii ya mawazo........

Read more...

Simon , kwa nini?

>> Tuesday, October 24, 2006


Rasta Luihamu na baadhi ya wadau wamekuwa wananipiga maswali kibao hivi karibuni. Najaribu kujibu hapa baadhi ya maswali ambayo yanazidi kujirudia.

Kuhusu Waafrika kuogopa kurudi Afrika
Mimi sidhani kwamba ni vigumu kuelewa kwa nini Waafrika wengi wanavyowezakuogopa kurudi nyumbani. Pia siwezi kusema kuwa Waafrika wengi ni ukweli kuwa ni woga uwafanyao waishi mabara mengine. Mpaka sasa hivi elimu itawalayo Afrika ipo katika vitabu vya wageni kutoka nchi nyingine. Luninga watazamazo zimetawaliwa na maonyesho yaelezwayo na watu wengine na kwa mtazamo mkubwa usioupa sura nzuri Afrika. Kama uijuavyo tabia ya binadamu, ni rahisi kuelewa kwanini atajaribu kutembelea sehemu zisifiwazo ilikujionea mwenyewe. Kila muafriaka aliyeko nje ana stori yake. Wengine walishakata tamaa na Afrika. Kwa sababu hakuna wanachokiona ambacho kina wapa moyo kuwa wanamchango wowote wakutoa.Hii hasa ni kutokana nakuamini mfumo ambao upo ni vigumumu kuwapa nafasi ya kutoa mchango wao. Wapo ambao wamekwama nje ya bara. Maisha ni magumu, lakini bado wameweza kutunza hali ya utu wao kwa kujificha mbali na Afrika ambako ndugu na jamaa hawatashuhudia kasheshe ya maisha waishiyo. Wako ambao maisha yao na ujuzi wao hawawezi kuutimiza ndani ya Afrika kutokana na kukosekana mfumo uwianayo na elimu ambayo msingi wake wameupata tokea shule zetu za Afrika zinavyotuandaa. Wako wanaodhalilishwa kila siku. Wapo ambao wanaheshimika na kuthaminiwa. Kuhusu kujiandaa kabla ya kuvamia jambokwangu naona ni jambo ambalo kila mtu anatakiwa kufanya kwanza. Hivyo kwa wale walioishi muda mrefu nje ni lazima waliangalie hili swala. Hata kwa wale amabo wanaamini vijana wote wa mijini warudi vijijini, kama aaminivyo Mzee Luihamu,si busara tu ukaamua kwenda tu huko kijijini na jembe lako begani bila kujiandaa na hali halisi ya maisha ya kijijini. Maisha ni mchezo wa ajabu. Ukikua unastukia maamuzi yako kimaisha haya kuhusu wewe peke yako.Maamuzi yako hugusa ndugu na jamaa hadi jamii nzima. Maamuzi yasiyokuwa na mipangilio maalumu mara nyingi hayana nguvu ya majawabu ya kudumu.Kuna maamuzi yenye majina matamu lakini sio ukweli kuwa ni ya matatuzi ya kudumu.


Kuhusu nani atavaa viatu vya Martin Luther King Jr au Malcom X

Mimi binafsi sidhani kuwa kuna mtu atavaa tena kiatu cha Martin Luther King wala Malcom X. Kwa sababu sidhani kuwa kuna mtu yeyote amabaye anaweza kuwa kama mwingine. Nacho amini kila muda katika historia una matatuzi yake yalinganayo na muda huo. Hivyo yeyote mwenye busara atajifunza kutoka kwa akina Martin Luther Jr,Malcom X, Mwalimu Nyerere, babu, bibi, msaidizi wa kazi za nyumbani, na jamii kwa ujumla ilikufikia busara zimwezeshazo kutatua matatizo yamkabiliayo . Kumwezesha kutabiri mwelekeo wa mambo ilikuepuka au kuweza kukabili matatizo yatarajiwayo nk.

Kuhusu imani
Imani ni ya mtu binafsi na naamini kuwa mtu hawezi kulazimishwa kwamba aamini nini. Naulizwa sana mambo ya Urasta na Mzee Luihamu ameniambia kuwa tusiogope Urasta na Marasta , kwa kuwa ni wana wa Yosefu wa Israeli. Namuelewa kwanini anasema hivyo. Lakini chakujiuliza ni kwamba dini nyingi hizi watu wafuatazo sasa hivi zimekuwepo muda mfupi sana ukizingatia historia ya uwepo wa binadamu duniani. Je, kabla ya Yosefu Waafrika si walikuwepo? Je siinakumbukwa mikutano ya kujadili ni vitabu gani viingizwe kwenye biblia? Je ina maana Mwenyezi Mungu kabla ya dini na vitabu hivi vitakatifu viongozavyo imani karne hii alikuwa hana mapenzi na viumbe wake?Kwa mtazamo wangu ni kwamba imani ni kitu cha mtu pekee. Mtu akifa anaanza kivyake mwenyewe hivyo haya maswala ya imani za watu sitaki kuyaingilia. Kwa rasta Luihamu, mimi binafsi siogopi kuwa Rasta. Nilishawahi kuwa Rasta na kujikuta na pingana sana na baadhi ya misigi ya imani hiyo.Kwa kifupi, nilizaliwa katika familia ya kikristo.Nikawa Muislamu kwa muda, nikaokolewa na Mozesi Kulola, Nikarudi kwenye Ulutheri, na nikaendelea kujiuliza maswalali na naendelea kujifunza kuhusu imani.Hivi sasa naamini Mungu bila kufungamana na mfumo au institution yeyote.

Kuhusu vilevi

Mimi simshauri mtu yeyote atumie vilevi. Madhara yake hujulikana vizuri tu. Sidhani kuwa kuna kilevi hata kimoja ambacho hakina madhara. Pia, hili swala kila mtu anakichwa chake. Kwa ujumla sidhani kuna mtu anweza kupinga madhara ambayo yanaweza yakajitokeza na kumharibia mtu maisha. Lakini kumbuka hata chakula kina weza kukudhuru pia kama unakila bila mpango.Hivyo maswala haya ya vitu tuviwekavyo kinywani si yakuharakisha majibu kirahisirahisi. Sasa, mimi sivuti bangi wala kutumia madawa yoyote. Ndio nakunywa pombe za aina kadhaa. Simshauri mtu kuwa akiniona nakunywa basi naye aanze?Hapana hilo sifanyi.


Kuhusu muonekano wa kiafrika
Kwanini huwa najibu sana kuwa mimi ni muafrika lakini wakati mingine navaa suti? Mimi siamini Uafrika ni mavazi. Sidhani ukivaa Kichina basi unahalali yakuitwa Mchina. Napenda mavazi ya kiafrika. Huvaa mavazi ya kiafrika. Napenda kuvaa navyojisikia na siamini kuwa Uafrika wangu unapungua kwa kuvaa hivyo. Sidhani kuwa Mandela kwa kuvaa Kiindonesia amepunguza Uafrika kusini wake.Halafu sioni kwanini muonekano wa nywele zangu uwe ni tatizo . Siamini kuwa muonekano wa nywele ni kipimo cha ubinadamu wa mtu.Muonekano wa nywele zangu mimi kama Muafrika naona ni wa kawaida tu.Na naamini ni wa kiafrika sana ambao isingekuwa wamagharibi kuunganisha na tafsiri mbalimbali ungeweza kuwa wakawaida sana katika maofisi ya Afrika. Nashangaa sana kuona kuwa bado watu huchukua muda sana kufikiria swala hili. Je na wewe ufuge nywele kama zangu?Hilo ni juu yako. Je, wewe unavaa nguo za Kiafrika zipi? Jinsi au lubega?

Sidhani kuwa nimepungukiwa Uafrika kwa kuwa hapa sijavaa nguo zitafsiriwazo kama ni za Kiafrika. Ila sikushauri unywe pombe, unajua mwenyewe :pombe si chai

Read more...

Jerry Rawlings , Babangida wanarudi, Mwinyi Je?



Mzee Jerry







Kama Jerry Rawlings anataka kurudi, hii inatuambia nini kuhusu imani ya Wazee wa Kiafrika kuhusu damu mpya katika ukombozi wa Afrika? Nigeria,Ibrahim Babangida anataka kurudi.Soma hapa habari za tetesi za kwamba Jerry anataka kurudi. Jambo hili kwanza likanifanya nifikirie kuwa sisi Tanzania tuna bahati, kwani sijasikia tetesi za viongozi waliopita wakitaka kurudi. Lakini nikaanza kujiuliza, hivi hawa Wazee wetu Tanzania waliondoka kweli? Tanzania ndio hivyo hata kama Raisi Mwinyi hajasema anataka kugombea tena Uraisi ili kuongeza ruksa, bado tumefanikiwa kutunza utamaduni wetu potofu wa kuwatunza viongozi ambao washaonyesha kushindwa kazi. Tabia ambayo labda wakati wa Nyerere ungeeleweka kuwa unatokana na nchi kutokuwa na wasomi wakutosha kushika uongozi, inazidi kuneemeka katika kipindi cha Muheshimiwa Raisi Kikwete. Na hii ni ya kuwaamisha viongozi walioonyesha mapungufu kutoka katika ofisi moja kwenda kwenye nyingine. Naamini kitendo hiki ndicho kimesababisha maraisi waliopita Tanzania kutosema wanataka kurudi kwa sababu kwa ujumla hakuna kilichobadilika.Natumaini jambo hili litakemewa na sisi wana jamii ya Tanzania mpaka lionekane ni la aibu kwa viongozi wetu. Au labda Raisi Mwinyi atataka kurudi tena na kuwa na waziri wake mkuu John Malecela.Tusubiri tutaona!
Kwa kuandika hivi simaanishi kuwa Wazee mchango wao hautusaidii bali ningependa wajaribu kuelewa kuwa pale ambapo mtu mwingine anaweza kutoa mchango zaidi basi apewe nafasi. Busara ya Wazee inahitajika. Hawa Wazee wangekuwa na mchango mkubwa sana katika kutambulisha ni mambo gani na njia gani walipita ambazo zimekuwa ni kikwazo cha maendeleo. Ingekuwa bora wawewakweli na makosa yafanyikayo na hii ndio busara ambayo inahitajika. Kuhusu kung'ang'ania ofisi na kushauriana jinsi ya kubaki ofisini sidhani ndio busara tuihitajio kutoka kwa Wazee wetu. Basi Wazee mlioshindwa ondokeni , mpishe damu mpya yenye mtazamo mpya. Au andikei basi hata vitabu kuelezea undani wa kiini cha kushindwa kwenu kututoa katika hali hii mbaya tuliyonayo Tanzania.Mkitoka kuweni washauri wema kwa kuwa wazi na jinsi kirahisi mzunguko wa makosa unavyoweza kujirudia.Ingefurahisha kuona heshima za shikamoo viongozi wetu mpewazo zingelingana na hekima na busara ambazo mnaziangaza kwa Taifa. Shikamooni Wazee!

Read more...

Watu maarufu wachukuapo Watoto Yatima Afrika

>> Wednesday, October 18, 2006

Hivi karibuni swala la watoto yatima Afrika limekuwa jambo kubwa katika vyombo vya habari vya magharibi. Hasa ni baada ya Madonna kwenda Malawi na kuchukua mtoto mmoja wa kiyatima hapo. Nimekuwa nafuatilia mambo mengi yaliyozuka katika mjadala kuhusu kwanini ni sahihi au sio sahihi jambo hilo alilofanya Madonna. Wengi walisema kuwa mtoto wa kiafrika anapaswa alelewe na familia ya kiafrika ili awezekukua katika maadili ya kiafrika. Wengine wakasema kuwa mtoto ambaye hana ndugu wanaoweza kumlelea ,hana kwake ni afadhali apate tu pakuishi kuliko kutokuwa na sehemu aitayo nyumbani. Wako wengi wakasema, hawa watu wanatumia hii njia ya kudhamini watoto ilikujitengenezea jina zuri.Mimi ninakubaliana na wote. LAKINI NINGEPENDA WATU WOTE WASEMAO, WASEME ZAIDI YA MANENO MATUPU WAO WANAFANYA NINI KIVITENDO KUSAIDIA WATOTO YATIMA?Isije ikawa kuwa sio hawa watu maarufu kuwa wanajitafutia umaarufu, bali ikawa ni hao wawasemao akina Madonna ndio wakawa wanatafuta umaarufu.Chakujiuliza ni kwamba tunavyodai watoto wa kiafrika wanapochukuliwa kwenda nchi za magharibi wanapoteza Uafrika wao, je ni nini kinachotunza Uafrika wamtoto wa kiafrika Afrika kitamaduni sasa hivi? Kwa maana ni ukweli asilimia kubwa za mambo yanayozidi kumzunguka mtoto wa kiafrika Afrika yanamizinguo ya kimagharibi.Yaonyeshwayo kwenye televisheni ya asilimia kubwa ni ya kimagharibi.Shule zetu zinashinikiza elimu ya kimagharibi.Dini zetu ndio hizo zakutoka nje. Sasa tunafanya nini kumtunza mtoto wa Kiafrika abakie na maadili ya kiafrika? Halafu sisi Waafrika tunafanyanini kumfanya mtoto wa Kiafrika aliye nche ya bara la Afrika kujivunia Afrika? Je tunaendeleza vita na njaa+ je tunaendelea kujidharau wenyewe?

Nachoshukuru moja ya jambo lililojitokeza katika mshawasha huu ni kuwekwa hili swala la watoto yatima kwa siku kadhaa katika kurasa za mbele za vyombo vingi vya habari duniani. Natumaini kama umaarufu basi uwe katika swala zima la tatizo hili na sio kwa watu binafsi.Kwani inajulikana kwa miaka mimi wako watu binafsi ambao wanafaidika na miradi ya watoto yatima zaidi ya watoto yatima wenyewe.Tatizo hili ni kubwa.Na ninawapapongezi wale wote wajitoleao kwa moyo kusaidia kwa lolote wawezalo kutatua swala hili.

Hivi unahisi Michael Jackson angetaka kuadapti mtoto angeadapti kutoka wapi?

Read more...

Chakula cha Mawazo!- Dume Jike!

>> Tuesday, October 17, 2006

Nakumbuka nilipokuwa mdogo katika jitihada za kuhakikisha kuwa mimi naitwa dume ilibidi nipitie mambo kibao. Nishakula pilipili kali , kupigana na mengine mengi tu ili mradi nipasi kama dume. Sasa hivi karibuni nilipata kuongea na Mbongo ambaye alikuwa anauelezea utamaduni wa ubasha na usagaji ulivyo neemeka katika baadhi ya sehemu Tanzania. Hili swala ingawa mara nyingi haliongelewi sana ni jambo ambalo liko sehemu kibao. Katika kipindi hiki cha karibuni, hasa baada ya Louis Farrakhan kuzidi kuugua nimekuwa nikipitia kazi zake. Yeye analake la kuongea, hasa mtazamo wake juu ya wanaume kama akina Michael Jackson na Prince, unanifikirisha. Kwa kuonekana kikekike anaamini si mfano mzuri kwa wanawake, kwani wnaanza kupotoka kuwa mwanamume halisi ni yupi.
Je unasaidia wanaume kuwa kama wanawake?


Read more...

Mtazamo wa Kiafrika

Kuna kipindi hapo nyuma niliongelea kuhusu jinsi Watanzania tunavyoweza kutoa heshima zote kwa wageni katika nchi mambo hambayo hatupeani wenyewe. Nilisoma habari moja iliyotoka kwenye tovuti ya The Black Star News, ambayo ilinigusa pia. Hii habari ilikuwa inaongelea jambo la kuenzi wageni kuliko wazawa nchini Kenya. Inasemekana Seneta Barak Obama, alipata muda wa vyombo vya habari kuliko mwanasiasa yeyote mwingine Kenya . Lakini kilichoniua ni kwamba inasemekana hata timu ya mpira wa miguu ya Kameruni ilipofika Kenya ,maafisa wa Kenya wakaiondoa timu ya Taifa ya Kenya kwenye uwanja mzuri iliiipishe ya Kameruni. Kumbuka ni katika kipindi ambacho timu ya Kenya ilipokuwa inajiandaa kucheza mechi ya kimataifa. Soma habari hii mwenyewe:
African Inferiority Complexes. Mtazamo huu wa kimawazo nimeushuhudia sana Tanzania.

Sawa watu wengi husema sisi Watanzania ni wakarimu. Lakini mimi nahisi ukarimu wa kuufanya tu kwa kuwa tu mgeni kutoka nchi za nje anahusika hautatupeleka mbali.

Read more...

Tanzania gizani!

Kila nikisikia juhudi za viongozi wetu kufanya ziara duniani hujiuliza hivi ni wawekezaji gani ambao ni walengwa? Karibu wawekezaji wote hawataweza kufanya mengi ikiwa hakuna umeme wakuendeshea shughuli. Labda ikiwa walengwa sasa ni wale wawekezaji ambao watasaidia kutatua matatizo ya umeme au safari hizi zenye gharama za kutafuta wawekezaji hazitakuwa na manufaa sana.

Chakujiuliza tu ni kwamba:inawezekanaje katika nchi za Afrika Mashariki ni sisi tu tunaathirika sana na swala hili la umeme mara nyingi kuliko wengine?
Je, kwanini hakuna mipango ya muda mrefu ya kujua jinsi ya kukabiliana na swala hili la umeme?
Hivi katika maswala ya kupewa kipaumbele, ndege ya raisi, radar ya jeshi au umeme uwezeshao viwanda kufanyakazi ni nini muhimu sasa hivi?
Je umeme kuwepo siku za mapumziko na kukatwa siku za kazi sio dalili kuwa wahusika wanatoa kipaumbele potofu?

Natumani siku moja taifa letu litafikia uwezo wakutabiri maswala yafaayo kupewa kipaumbele katika wakati ufaao kuandaa matatuzi.Kwa maana kama ilikuwa haijulikani kuwa taifa litaingia katika kisa hiki kabla basi sishangai Tanzania ikijikuta inakabiliana na kasheshe nyingine kama hii kienyejienyeji tu.

Read more...

Chakula cha Mawazo!

>> Tuesday, October 10, 2006

Dini yako ni ipi?

Je wewe ni mkristo au muislamu?
Hivi kwanini siasa ya Taifa kama Tanzania haichezi mbali na maswala ya dini?
Kwanini dini ni muhimu Marekani na siyo Japani?
Hivi Louis Farrakhan unamkumbuka?Naona naye anasubiri kufa kwa kansa sasa hivi.


Duh hivi kweli asilimia kubwa ya Wachina, Wahindi , na Waafrika ambao hawako kwenye Ukristo au Uislamu kwao ni motoni tu? Hivi Wayahudi wasio wakristo au waislamu kwao ni motoni? Hivi Uislam wa Wamarekani weusi ni sawa na Uislamu wa Uarabuni?Hivi Ukristo wa Afrika ni sawa na wa nchi za mgharibi?

Hivi wewe ni mdini wa kweli?

Read more...

Hivi Histori inatufundisha kitu?


Ukicheki haya ya Afrika Kusini utapata moyo.
Alaah!Sasa mbona Askofu Desmond Tutu mwezi uliopita tu amekiri kuwa Waafrika kusini wamepoteza dira?

Je kweli sisi watu weusi tutaamka na kung'ara kama asemavyo Bunny Wailer hapa chini?

Read more...

Mkuki kwa Nguruwe, kwa binadamu ......

Katika pita pita kwenye mtandao nikakutana na kijiwe cha Wakazakstani wakijadili jinsi mchekeshaji aitwaye Sacha Baron Cohen awazalilishavyo katika skechi zake ambazo anaigiza kwa jina la Borat. Huyu Borat ni mwandishi wa habari mshamba kutoka Kazakstani ambaye anatembelea Uingereza na Marekani katika kujaribu kupata mafunzo ya ustaarabu.Muangalie hapa chini akijifunza kutongoza.


Huyu Mzee Cohen ni Myahudi wa kutokea Uingereza. Kwa kuigiza kama yeye ni Mkazakstani mshamba alifikia kutaka kufanya sinema yake kuwa ni gumzo kati ya George Bush na raisi wa KazakstaniNursultan Nazarbayev . Wakati nikielewa kwanini watu wanacheka lakini natambua kwanini Wakazakstani wanachukia. Kwanza kitendo chake kinafanya wahisi kuwa dunia nzima itawaona kuwa hawajastaharabika.
Angalia hapa chini trailer la sinema yake.

Borat aipavyo sura Kazakstani.
Je, kama mtu huyu badala ya kujifanya Mkazakstani akajifanya Mtanzania , Watanzania wangejisikiaje? Mimi na uhakika tungelalamika kuwa ni ubaguzi wa rangi nk.

Lakini tena huyu jamaa kama Myahudi hupenda kuwajitania mwenyewe. Ingawa mimi naamini kuwa Wayahudi ni watu ambao ni rahisi sana kulalamika kuwa wananyanyaswa.Kitendo cha Mzee Cohen chakutania Wayahudi hakija lalamikiwa na Wayahudi.

Muangalia hapa chini aimbavyo kuwa Wayahudi watupwe kisimani kwani wao ni chanzo cha matatizo.


Bado nafikiria kuwa Tanzania na Watanzania wangepewa sura hii Borat aipakavyo kwa Wakazakstani, sijui ingekuwaje. Kwa maana hata maswala ya ukweli kama yale ya samaki waliooza ziwa nyanza tulikuwa tunakana kwa nguvu zote.

Sawa wengi wanasema hii ni matani tuu. Labda ni kweli!
Sasa huu mkuki kwa nguruwe ..... ?

Read more...

Vilevi vya akili

>> Sunday, October 08, 2006

Kilevi kikubwa kisicho cha kawaida ni dini.
Pombe kwa Wabongo, na karibu kila kabila lina vyake.
Bangi Wahindi. Wajamaika nk....
Pombe kali, Warusi, Wafini nk.........
Bia, Wajerumani. Wana viwanda zaidi ya 1200 vya kutengenezea kifyonzo hiki.nk..........
Sigara, Wahindi wekundu, dunia, nk.........
Ngono, Dunia.nk......
Elimu, dunia. nk.........
Je umelewa?
Kilevi chako ni nini?
Je ni ngono?

Read more...

Ukiwa Mbali na Nyumbani....

Ni kawaida kukumbuka nyumbani.
Ni kawaida kutokuweza kujua yote wanayokabiliananayo nyumbani.
Ni kawaida kua nyumbani hawawezi kujua yote ukabilianayo nayo wewe.
Ni kawaida kutoambiana yote kwa nia ya kuepushania hali fulani ya mizinguo.
Ni kawaida kukosea kutoona mambo kwa mtazamo wa mwingine.
Lakini...
nikawaida kufarijika kuwa kuna nyumbani kwa walio mbali na nyumbani.
Natumaini...
baadhi ya matukio magumu ya sababishwayo na ukiritimba wakuwa mbali na nyumbani yanajenga zaidi ya kubomoa.
Natumaini! Natumaini! Natumaini!

Je, Mtanzania ambaye hayuko Tanzania hayuko nyumbani?
Je, Je ni kawaida kulaumiana?
Inawezekana kawaida ikawa si kawaida!

Read more...

Hivi akina Ndesanjo hawako Nyumbani?

Ndani ya wiki mbili hivi sasa nimeulizwa sana kuwa kwanini akina Ndesanjo hawako nyumbani+ Mawazoni nikaanza kujiuliza kwanini hili swali hapelekewi Ndesanjo mwenyewe? Lakini baada ya muda kidogo nikagundua kumbe wote Watanzania ambao hatuko Tanzania ndio akina Ndesanjo. Nikaanza kufikiria sana kuhusu hili swala. Kwanza nikaanza kujiuliza Mzee Ndesanjo anafikiria nini kuhusu sisi wote tunavyojumuishwa kwa kutumia jina lake. Pili nikaanza kufikiria kwanini sipo Tanzania hivi sasa ingawa ni mpango wangu kurudi nyumbani. Nikaanza kufikiria jinsi ilivyokuwa ngumu kwa familia yangu kutoka Kilimanjaro ,Musoma, Mbeya kwenda Songea halafu Morogoro.

Swali hili lilinikumbusha sana Kwame Nkurumah. Huyu Muafrika ambaye aliamini sana katika kuiunganisha Afrika. Na mpaka sasa hivi hakuna kiongozi wowote wa Afrika ambaye amejaribu kwa nguvu zote kufanya Afrika iungane kama yeye. Nakumbuka alivyorudi nyumbani na imani yake na juhudi zake lakini bila ya kuwa na ukweli wa hali alisi ya mtaani Afrika na majibu ya kukabili shaghala baghala zake. Sijaribu kusema kuwa kila mtu ana ndoto kama zake ambaye yuko ughaibuni. Lakini jibu la swali naloulizwa ni kwamba, maisha si rahisi kienyeji enyeji namana hiyo.
Watu wengi naokutana nao Ughaibuni wako shule. Pili wako ambao wana elimu ambayo hata kazi za kukizi ujuzi wao haziko bado Tanzania. Wako watu ambao wamekwama Ughaibuni kwa sababu kihali alisi hawawezi kuishi bongo. Kumbuka watu huiita tanzania Bongo. Sababu moja ni kwamba si sehemu unaweza kuitokea tokea tu kienyeji halafu ukategemea mambo yakawa shwari.

Nawakumbuka sana leo Nkuruma ,akina Sekou Toure mpaka Patrice Lumumba. Ingawa pia siwezi kumsahau Mwalimu Nyerere katika kundi hili. Nyerere na Nkurumah walirudi na kufanya mambo. Ingawa nafikiri Nkurumah aifanya maswala yake kabla ya muda wake. Maana jambo lake la kutaka Afrika yote iungane wakati sisi kama Watanzania bado hatujapata suluhisho kamili kati ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar , unaweza kuona ugumu uliopoa ukitaka Tanzania na Somalia ziungane.

Lakini hivi Ndesanjo hayuko Nyumbani?. Si ndio huyu huyu Ndesanjo aliyekuwa kwa nguvu zote akitetea Watanzania na Raisi wetu tulivyoitwa kuwa sisi Watanzania ni maimuna na Kikwete ni kiwete?Si ndio huyu huyu Ndesanjo apendaye kutukumbusha tutumie kiswahili katika mtandao kwa kuwa sisi ni Watanzania?Cha ajabu baadhi ya watu waliokuwa wananiuliza kwa nini akina Ndesanjo hawarudi nyumbanni waliniuliza hivyo wakitumia lugha ya kizungu.

Sasa kwanini bado sijarudi Tanzania. Jibu kubwa kuliko yote ni majukumu ambayo yana nibana ki jiografia sasa hivi. Je nitarudi Tanzania hivi karibuni? Jibu ni ndiyo. Je ninamshauri Mtanzania arudi nyumbani? Jibu ni ndio. Je We Mtanzania ulioko nje ya nchi urudi tu pale ki holela. Jibu ni hapana. Kumbuka ukirudi kiholela hata mchango wako katika jamii unaweza ukawa mdogo kuliko mchango wako ukiwa nje ya nchi.

Hivi tokea Wayahudi waanzishe mradi wao wa Israel ni asilimia ngapi bado hawajarudi? Hivi mchango wao nje ya nci si ndio uendelezao Nchi? Hivi wachezaji wa mpira kama akina Samuel Eto'o, mchango wao nje ya nchi hauifaidishi Kameruni?

Ntaendelea kujibu swala hili siku nyingine.

Read more...

Chakula cha Mawazo!

>> Saturday, October 07, 2006

Read more...

Marehemu Alikuwa Mtu Mzuri!

>> Friday, October 06, 2006

Marehemu Simon..

Mtu wa Kwanza: Kwa heri Simon! Upumzike mahali pema peponi.
Mtu wa Pili: Alikuwa rafiki yangu sana!Nakumbuka alikuwa ananisaidia kuchuma kisamvu.

Mtu wa tatu:Duh !Sasa sijui nitafanyaje maana ana madeni yangu! Alikuwa hajali watu! Lakini afadhali kaanza tu!
Mtu wa nne:Duh !Msiba huu bomba! Msosi na vinywaji kibao!

Marehemu IDD AMIN

Mtu wa kwanza:
Alikuwa bomba la mnyama afadhali kafa.

Mtu wa pili:
DUh! Aliwanyosha Wahindi na Wazungu alikuwa bomba sana.


Marehemu kwa ujumla.


Watu asilimia kubwa kuliko:
Marehemu alikuwa mtu safi sana.

Hivi marehemu wanasikia? Kwa nini usimshukuru na kumsifia mtu wakati yuko hai? Hivi yale maua na vitu vinginevyo umleteavyo katika mazishi au kaburini vinamaana kwa mrehemu?

Au unajifariji mwenyewe katika kifo cha mwenzio?

Oho! Naona unajisikia vibaya kwa sababu unataka kucheka kilioni baada ya kushuhudia mtu analia mlioa dizaini!

Samahani nabunia tu. Usijali!

Read more...

Unakumbuka ulipocheka baada ya kuona mtu kaanguka?

Nilipopita katika blogu ya Mzee wa Mshitu niliona picha hii hapa chini ambayo ilinifikirisha kidogo.




Picha imepigwa na Edwin Mjwahuzi





Picha hii imenikumbusha jinsi jambo limsikitishalo mtu mmoja lavyoweza kuwa ni la kumfurahisha mwingine. Likanikumbusha jinsi ma- stock broker wenye madili ya mafuta na dhahabu ambavyo walifurahia vita vilipoanza Iraki. Unaambiwa kila siku walikuwa wakisubiria kwa hamu vita ianze kwa sababu walijua ikianza tu bei ya mafuta na dhahabu zitapanda, hivyo faida itakuwa bwelele.Kumbuka hiki ndio kipindi hicho hicho ambacho wengine wakiombea vita isitokee.

Duh! Baada ya kunyoshea wengine vidole nimekumbuka kuwa mimi mwenyewe ishawahi tokea nikacheka wakati nashuhudia mtu kakanyaga ganda landizi halafu anaanguka. Ukweli kicheko kiliisha baada ya kugundua aliyeanguka kavunjika mkono. Lakini kwanini kitu kimuumizacho mmoja chaweza kumkenulisha meno mwingine? Ukiangalia kwenye picha hapo juu utashangaa kuona mwenye kibanda akifa moyo wakati pembeni yake mtu anafurahia!

Hivi kwanini watu wengine hucheka mpaka vilema? Nilipopita katika blogu ya Mzee Ndesanjo, nilikuta ameongelea jinsi Mkenya moja katika kumzalilisha Raisi Kikwete wa Tanzania,akaamua kumuita Kiwete. Hivi Raisi Kikwete akiitwa kiwete amedhalilishwa? Je viwete si watu kamili?Hivi Utu ni nini?Sawa ninakubali jina lake ni Kikwete hivyo si sahihi kulibadilisha kienyejienyeji. Je? Katika kumuita kiwete wewe unafikiria ni dharau kwa kuwa jina limekosewa au kwa sababu tu kaitwa kiwete?

Usitishike najiuliza tu!

Kumbuka tu wote tunaanguka kwa zamu. Ukicheka leo usishangae utakapochekwa kesho.

Read more...

The revolution will no be televised-Gill Scott Heron

>> Thursday, October 05, 2006



Mzee Gill enzi hizo




Ukitaka kufanya mapinduzi jishughulishe kw vitendo.Ndivyo alivyokuwa akisema Mzee Gill-Scott Heron.

Kwa kweli Luninga inadaka baadhi ya mambo katika mapinduzi, lakini mapinduzi halisi yako mtaani kwa Bi kidude na kwa Mzee Hamdala pale kijiweni.

Leo nimemkumbuka Mzee Gill-Scott Heron baada ya kupitia baadhi ya mashairi yake.
Nasikitika Kuwa huyu Mzee ana ukimwi .Lakini ninamshukuru kwa kunifikirisha mambo kibao. Unakumbuka shairi lake lisemalo, Weupe wako mwezini wakati siye tunahaha?
Duh! Inanikumbisha tu kuwa Tanzania mpaka sasa hivi upande mmoja unaweza kukumbwa na njaa wakati mwingine vyakula vinaoza!
Ingawa Mzee Gill anamambo sikukubaliani nayo lakini bado hata katika hilo anaendelea kunifikirisha. Asante Mzee Gill-Scott Heron kwa hilo.



Mzee kwenye Hardtalk

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP