Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Unakumbuka ulipocheka baada ya kuona mtu kaanguka?

>> Friday, October 06, 2006

Nilipopita katika blogu ya Mzee wa Mshitu niliona picha hii hapa chini ambayo ilinifikirisha kidogo.




Picha imepigwa na Edwin Mjwahuzi





Picha hii imenikumbusha jinsi jambo limsikitishalo mtu mmoja lavyoweza kuwa ni la kumfurahisha mwingine. Likanikumbusha jinsi ma- stock broker wenye madili ya mafuta na dhahabu ambavyo walifurahia vita vilipoanza Iraki. Unaambiwa kila siku walikuwa wakisubiria kwa hamu vita ianze kwa sababu walijua ikianza tu bei ya mafuta na dhahabu zitapanda, hivyo faida itakuwa bwelele.Kumbuka hiki ndio kipindi hicho hicho ambacho wengine wakiombea vita isitokee.

Duh! Baada ya kunyoshea wengine vidole nimekumbuka kuwa mimi mwenyewe ishawahi tokea nikacheka wakati nashuhudia mtu kakanyaga ganda landizi halafu anaanguka. Ukweli kicheko kiliisha baada ya kugundua aliyeanguka kavunjika mkono. Lakini kwanini kitu kimuumizacho mmoja chaweza kumkenulisha meno mwingine? Ukiangalia kwenye picha hapo juu utashangaa kuona mwenye kibanda akifa moyo wakati pembeni yake mtu anafurahia!

Hivi kwanini watu wengine hucheka mpaka vilema? Nilipopita katika blogu ya Mzee Ndesanjo, nilikuta ameongelea jinsi Mkenya moja katika kumzalilisha Raisi Kikwete wa Tanzania,akaamua kumuita Kiwete. Hivi Raisi Kikwete akiitwa kiwete amedhalilishwa? Je viwete si watu kamili?Hivi Utu ni nini?Sawa ninakubali jina lake ni Kikwete hivyo si sahihi kulibadilisha kienyejienyeji. Je? Katika kumuita kiwete wewe unafikiria ni dharau kwa kuwa jina limekosewa au kwa sababu tu kaitwa kiwete?

Usitishike najiuliza tu!

Kumbuka tu wote tunaanguka kwa zamu. Ukicheka leo usishangae utakapochekwa kesho.

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

NDABULI 10:59 am  

Bwana Kitururu, nadhani kutumia neno Kiwete ni udhalilishaji ndio maana neno hilo sasa hivi halitumiki rasmi(officially) katika maandishi au matamshi rasmi, rasmi inayotumika kama sijakosea ni mlemavu wa mkono au mguu n.k. Ni kama neno taahira siku hizi ni mtindio wa ubongo na si neno kipofu linalotumika sasa hivi. Utumiaji wa maneno haya yanapigwa vita na wanaharakati wa haki za binadamu kwani yanaonyesha udhalilishaji wa binadamu

Anonymous 10:06 am  

Kitururu: unajua maneno hayana maana yoyote hadi pale tunapoyapa maana. Mwandishi Marechera wa Zimbabwe alikuwa na tabia ya kusema kuwa anapoandika anailazimisha lugha iseme anachotaka kusema na sio lugha imfanye yeye aseme anachotaka.

Kwahiyo neno linaweza lisiwe upande wowote (hasi au chanya) hadi pale mtumiaji atakapoamua kulitumia kwa mazingira fulani anayotaka yeye (iwe ni hasi au chanya). Na wakati mwingine uhasi au uchanya wa neno unaweza kueleweka sio kutokana na kuwatazama wale ambao neno au jina hili linawataja bali utamaduni na mitazamo. Kwa mfano, neno mwanamke. Unaweza kukuta mwanaume anagombana akawamwambia mwanaume mwenzake, "mwananamke wewe." Haina maana kuwa mwanamke ni kosa au ni kashfa au tusi au ni upungufu fulani. Ni utamaduni ndio umefanya ikaonekana hivyo kwahiyo mtu akatumia neno mwanamke kama njia ya kumtukana mwenzake kutokana na jinsi ambavyo neno mwanamke linachukuliwa katika mazingira hayo.

Ndio maana basi baada ya kusoma yote aliyoandika ndugu wetu huyu wa Kenya kuhusu Kikwete utagundua kuwa neno kiwete amelitumia hapo kwa mtazamo upi. Sijui kama nimejieleza vyema.

Simon Kitururu 3:52 pm  
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous 3:59 pm  
This comment has been removed by a blog administrator.
Simon Kitururu 5:14 pm  

Ndabuli nakubali kabisa na hilo. Halafu ukweli bado hili jambo kwa waliowengi halijawafikia. Watu hujisahau kuwa majina yale tuwaitayo wenzetu ,hao wenzetu hawakubaliani nayo.Ndesanjo maelezo yako, yako safi kabisa. Nilivyoandika hapa lengo lilikuwa kukumbusha watu kufikiria maneno tuyasemayo na kwanini yaweza kuwayanadhalilisha. Mara nyingi watu hatufikirii kwanini tukitukanwa -mfano:mbwa wee! tunaanza kuvurumisha magumi!Lakini katika ile habari ya Kikwete jambo lilikuwa wazi kuwa nia ilikuwa nini.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP