Chakula cha Mawazo!
>> Tuesday, October 10, 2006
Dini yako ni ipi?
Je wewe ni mkristo au muislamu?
Hivi kwanini siasa ya Taifa kama Tanzania haichezi mbali na maswala ya dini?
Kwanini dini ni muhimu Marekani na siyo Japani?
Hivi Louis Farrakhan unamkumbuka?Naona naye anasubiri kufa kwa kansa sasa hivi.
Duh hivi kweli asilimia kubwa ya Wachina, Wahindi , na Waafrika ambao hawako kwenye Ukristo au Uislamu kwao ni motoni tu? Hivi Wayahudi wasio wakristo au waislamu kwao ni motoni? Hivi Uislam wa Wamarekani weusi ni sawa na Uislamu wa Uarabuni?Hivi Ukristo wa Afrika ni sawa na wa nchi za mgharibi?
Hivi wewe ni mdini wa kweli?
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kaka nimekupata,kwa maoni yangu uislamu au ukristo wa Afrika unaweza ukawa na similarities za vitabu lakini kiuhalisia ni tofauti, kikubwa katika hii ni imani. Ni mada pana sana mzee lakini nadhani hicho ndo nachoweza kusema kwa sasa.
Kitururu, hapo umegusa jambo nyeti sana, huwa nashangaa sana nikiona watu wanaweka mbele vitu ambavyo waliingizwa kwa hila tuu! Ukimuuliza mkristo au muislam una uhakika gani kama wewe ni wa dini hiyo? atakupa majibu ambayo ni mwendelezo wa udhanifu, akiwa tayari kuulinda kwa lolote lile litakalotokea!
Huwa nashangaa sana sisi tukisemana vibaya sababu ni wa 'dini' tofauti. huku hakuna mwenye uhakika wa alivyo yeye.
Mjadala mkubwa sana huu.
Post a Comment