Jerry Rawlings , Babangida wanarudi, Mwinyi Je?
>> Tuesday, October 24, 2006
Mzee Jerry
Kama Jerry Rawlings anataka kurudi, hii inatuambia nini kuhusu imani ya Wazee wa Kiafrika kuhusu damu mpya katika ukombozi wa Afrika? Nigeria,Ibrahim Babangida anataka kurudi.Soma hapa habari za tetesi za kwamba Jerry anataka kurudi. Jambo hili kwanza likanifanya nifikirie kuwa sisi Tanzania tuna bahati, kwani sijasikia tetesi za viongozi waliopita wakitaka kurudi. Lakini nikaanza kujiuliza, hivi hawa Wazee wetu Tanzania waliondoka kweli? Tanzania ndio hivyo hata kama Raisi Mwinyi hajasema anataka kugombea tena Uraisi ili kuongeza ruksa, bado tumefanikiwa kutunza utamaduni wetu potofu wa kuwatunza viongozi ambao washaonyesha kushindwa kazi. Tabia ambayo labda wakati wa Nyerere ungeeleweka kuwa unatokana na nchi kutokuwa na wasomi wakutosha kushika uongozi, inazidi kuneemeka katika kipindi cha Muheshimiwa Raisi Kikwete. Na hii ni ya kuwaamisha viongozi walioonyesha mapungufu kutoka katika ofisi moja kwenda kwenye nyingine. Naamini kitendo hiki ndicho kimesababisha maraisi waliopita Tanzania kutosema wanataka kurudi kwa sababu kwa ujumla hakuna kilichobadilika.Natumaini jambo hili litakemewa na sisi wana jamii ya Tanzania mpaka lionekane ni la aibu kwa viongozi wetu. Au labda Raisi Mwinyi atataka kurudi tena na kuwa na waziri wake mkuu John Malecela.Tusubiri tutaona!
Kwa kuandika hivi simaanishi kuwa Wazee mchango wao hautusaidii bali ningependa wajaribu kuelewa kuwa pale ambapo mtu mwingine anaweza kutoa mchango zaidi basi apewe nafasi. Busara ya Wazee inahitajika. Hawa Wazee wangekuwa na mchango mkubwa sana katika kutambulisha ni mambo gani na njia gani walipita ambazo zimekuwa ni kikwazo cha maendeleo. Ingekuwa bora wawewakweli na makosa yafanyikayo na hii ndio busara ambayo inahitajika. Kuhusu kung'ang'ania ofisi na kushauriana jinsi ya kubaki ofisini sidhani ndio busara tuihitajio kutoka kwa Wazee wetu. Basi Wazee mlioshindwa ondokeni , mpishe damu mpya yenye mtazamo mpya. Au andikei basi hata vitabu kuelezea undani wa kiini cha kushindwa kwenu kututoa katika hali hii mbaya tuliyonayo Tanzania.Mkitoka kuweni washauri wema kwa kuwa wazi na jinsi kirahisi mzunguko wa makosa unavyoweza kujirudia.Ingefurahisha kuona heshima za shikamoo viongozi wetu mpewazo zingelingana na hekima na busara ambazo mnaziangaza kwa Taifa. Shikamooni Wazee!
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kakini Mzee unahabari ya kwamba Jerry Rawlings ni mchapa kazi kwa vitendo?ni akili tu mzee.mimi namkubali Jerry R.
Post a Comment