Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Behewa la mawazo: kwa nini Tanzania imechelewa kufanikiwa?...-N.1

>> Wednesday, October 25, 2006

#UTAIFA
Naamini Raisi Nyerere na uongozi wa kwanza ulibidi kutumia muda mwingi kujenga utaifa.Kuweka misingi ambayo ingeweza kutufanya taifa.Lugha ya kiswahili na kujenga mfumo mzima ambao ungetuwezesha kujiendesha kama taifa huru.

Swali: Je, Utaifa tunao hivi sasa?Kama tunao unatuweka katika nafasi gani nzuri ya kuendelea mbele kupita mataifa mengine ya jirani ambayo hayana Utaifa?Je kama Nyerere alikuwa anatumia baadhi ya muda kuhakikisha maswala mbalimabli ya utaifa yanaendeleaje akiwa chini ya upungufu wa viongozi wasomi, je, Raisi wa leo anatumia muda huo kufanya nini ikiwa idadi ya wasomi imeongezeka kupita ya kipindi cha Nyerere? Je , wasomi wetu wameelimika au wamekwenda shule tu na kuwa na vyeti babu kubwa?

Usistuke kama unasoma hapa maana yake uko ndani ya treni ya mawazo.
Katika behewa hili namba moja najiuliza tu kwamba kama utaifa ulikuwa lazima kujengwa hivyo lazima muda ulitumika kuujenga.Hii inaweza ikawa sababu ya kuchelewa kuendelea. Sasa kama huu utaifa umejengeka basi muda huu ni wa kuutunza Utaifa na kuutumia Utaifa wetu kama chanzo kimojawapo cha kwenda mbele.Je, mikakati ya nchi yetu inatumia faida zote ziletwazo na utaifa? Najaribu kufikiria kwanini tunajisifia sana Watanzanina kwa amani wakati sioni kama amani imetusaidia sana kupiga hatua kimaendeleo? Ukiwa unawasikiliza watu kama akina Jared Diamond, hasa katika kitabu chake cha Guns, Germs and Steel, utamsikia akikueleza ni jinsi gani Wazungu waliweza kufanikiwa . Atakupa jiografia, atakupa jinsi hata uwezo wa kugundua kilimo , kufuga wanyama mapema kulivyowezesha jamii mbalimbali duniani kuendelea mapema na kutawala nyingine.
Sasa hayo yalikuwa zamani lakini kikubwa ni kwamba jamii zote zilizo piga hatua ziliweza kutumia faida zilizoletwa na mambo ambayo wameyamasta tayari. Je sisi kama Tanzania na utaifa wetu na amani yetu , tumepungukiwa nini sasa hivi ambacho kinatufanya tusiwe Taifa lililofanikiwa kufaidika na yale tuliyoyamasta tayari? Mapungufu yapo, lakini tunajifunza nini kutokana na mapungufu hayo?Kwanini tokea enzi hizo za uhuru mpaka sasa bado tunazungukwa na magonjwa,mfumo dhaifu wa elimu,mfumo wa uongozi hata mori mbaya wa kazi?

Sasa siri ya kutatua jambo hili ni nini? Je, ni mpaka Taifa zima lielimike ili tuweze kuwa na mabadiliko?Je, hivi historia inatufundisha kitu kweli?

Naendelea kusafiri katika Treni hii ya mawazo........

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 7:59 am  

Mzee Simon mawazo yako ni mazuri,tuchukulie mfano hai,KUTOA MAONI KUHUSU MKUTANO WA WANABLOGGU WA AFRIKA 2007.Baada ya kupewa wakati wakuchangia maoni naona kimya,wengi wetu tunamsubiri Mzee Ndesanjo aendeshe mkutano huu.Kwakweli wasomi ni wengi sana Tanzania na wananchi wengi wanajituma kusoma.Kwa upande mwingine wa shilingi tumechelewa lakini mzee Simon unategemea nini ukiona vijana nguvu kazi wameketi vijiweni kuanzia alfajiri mpaka jioni?kama kusafisha mitaro tu inakuwa vigumu tunasubiri serikali.Serikali ni mimi na wewe.Katika pitapita zangu unakuta watu bar mida ya saa nne asubuhi wanakata maji na nyama choma,je tutaendelea kweli?wasomi pekee hawawezi kusaidia taifa ni mimi na wewe kukubali kushika jembe kwani Mungu atatuongoza tukijituma.Kumbuka Mussa baada ya kuitwa na Mungu kwenda Misri kuwakomboa wana wa Israeli,alisita lakini Mungu akamwambia nenda nitakuwa nawe.Afrika ikiunganishwa na kuwa UNITED STATES OF AFRIKA nakwambia mzee Simon tutakuwa mbali sana vilevile TUKAMATE JEMBE NA KURUDI VIJIJINI TUPATE MAZAO.Huu ni mtazamo wangu.Jah live.

luihamu 11:01 am  

Mzee simon,nimepata nafasi ya kusoma kazi ya mwanabloggu METTZ kwa kweli huyu bwana anatisha nimemkubali.

Simon Kitururu 8:02 pm  

Karibu Msemo!Asante kwa kunitembelea kwa mara ya kwanza. Tutawasiliana na tuwasiliane Mzee

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP