Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Chakula cha mawazo!

>> Wednesday, October 25, 2006

Hivi tutawalalamikia Wazungu na Waasia kwa kutunyonya na kuendelea kutufanya watumwa mpaka lini?Mwanzo tulisema kuwa hatukuwajua hawa watu na hila zao.Sasa asilimia kubwa ya wasomi wetu ambao wamewasoma hawa watu wanajua hila zao.Sasa tunafanya nini na ugunduzi huu wa hila zao? Tunafanya nini kukabiliana na mifumo yao ambayo sasa hivi tunao wasomi wengi tu Afrika waliobobea katika taaluma za mifumo yao?Hivi wasomi wetu wa Afrika walio wengi siku hizi si wamesoma shule hizi hizi za hawa wamagharibi waongozao nchi hizi?Hata akina Sumaye , Malima nk si baadhi tu ya hawa ambao vikorido vya vyuo vikuu kama Harvard, nk, wanavijua kama nyuma ya viganja vya mikono yao?

Sasa swali ni kwamba, kama tunajua wanafanya nini hawa wamagharibi kwanini tunashindwa kujikwamua au hata kuwa na laghai zitakazotufaidisha sisi?Wachina walivyostuka wakaamua kubadili mtazamo na kutumia mpaka laghai ilikujifaidisha.Wajapani, Wakorea nk walifanya laghai kulingana na mazingira yao.Sasa sisi je?


500 YEARS LATER: AFRICA AND SLAVERY Dr Kimani Nehusi akilalamika.Nakubaliana naye lakini najiuliza hivi tutafanya hivi mpaka lini?

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 7:38 am  

Kwa mtazamo wangu Mzee Simon,mimi ni mtanzania naipenda sana inchi yangu na Afrika kwa jumla.Najua inakuwa vigumu kila mtu kuamini ya kwamba KILIMO ndiyo njia pekee inayaweza kutukomboa katika utumwa huu.Nakumbuka kinakipindi Mwalimu Julius alisisitiza sana vijana kushika JEMBE.Hatuwezi kusubiri serikali ifanye kila kitu bali ni jukumu langu na wewe kusaidia Afrika.Tukitaka kujikomboa kutoka utumwa huu ni vizuri vijana wote kurudi vijijini na kujiwekea mikakati,angalia inchi kama Japan,China,Korea,Libya ni mikakati Mzee wangu.Tukiamua kusitisha kupokea PIPI kutoka kwa inchi za kitajiri itakuwa jambo la maana kabisa.Narudia tena kujikomboa kwa mwafrika ni kilimo tu,kilimo ndicho uti wa mgongo.

luihamu 9:06 am  

Mzee simon hatuna viwanda unategemea serikali itoze kodi kutoka wapi?serikali inatozo wananchi kodi,mwananchi anapata hela kutoka na kazi yake.serikali kama haina hela itazidi kuwakata wananchi kodi zaidi,sasa Mzee bila kilimo hiyo kodi tutatoa wapi?

naona baadhi ya wanabloggu hawakubaliani nami kabisa kuhusu vijana kurudi vijijini na kukamata jembe.

naomba mjadala huu uendele.JE VIJANA WABAKI MJINI AU WARUDI VIJIJINI KUKAMATA JEMBE?

Kwawale wenye ajira mjini wabaki mjini na wakipata likizo waendekuwekeza vijijini.Naomba tusaidiane hapa.

Anonymous 1:46 am  

Nimeitazama video hiyo. Ngoja nitafute habari zake zaidi mtandaoni. Asante kwa kutuelekeza.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP