Hivi akina Ndesanjo hawako Nyumbani?
>> Sunday, October 08, 2006
Ndani ya wiki mbili hivi sasa nimeulizwa sana kuwa kwanini akina Ndesanjo hawako nyumbani+ Mawazoni nikaanza kujiuliza kwanini hili swali hapelekewi Ndesanjo mwenyewe? Lakini baada ya muda kidogo nikagundua kumbe wote Watanzania ambao hatuko Tanzania ndio akina Ndesanjo. Nikaanza kufikiria sana kuhusu hili swala. Kwanza nikaanza kujiuliza Mzee Ndesanjo anafikiria nini kuhusu sisi wote tunavyojumuishwa kwa kutumia jina lake. Pili nikaanza kufikiria kwanini sipo Tanzania hivi sasa ingawa ni mpango wangu kurudi nyumbani. Nikaanza kufikiria jinsi ilivyokuwa ngumu kwa familia yangu kutoka Kilimanjaro ,Musoma, Mbeya kwenda Songea halafu Morogoro.
Swali hili lilinikumbusha sana Kwame Nkurumah. Huyu Muafrika ambaye aliamini sana katika kuiunganisha Afrika. Na mpaka sasa hivi hakuna kiongozi wowote wa Afrika ambaye amejaribu kwa nguvu zote kufanya Afrika iungane kama yeye. Nakumbuka alivyorudi nyumbani na imani yake na juhudi zake lakini bila ya kuwa na ukweli wa hali alisi ya mtaani Afrika na majibu ya kukabili shaghala baghala zake. Sijaribu kusema kuwa kila mtu ana ndoto kama zake ambaye yuko ughaibuni. Lakini jibu la swali naloulizwa ni kwamba, maisha si rahisi kienyeji enyeji namana hiyo.
Watu wengi naokutana nao Ughaibuni wako shule. Pili wako ambao wana elimu ambayo hata kazi za kukizi ujuzi wao haziko bado Tanzania. Wako watu ambao wamekwama Ughaibuni kwa sababu kihali alisi hawawezi kuishi bongo. Kumbuka watu huiita tanzania Bongo. Sababu moja ni kwamba si sehemu unaweza kuitokea tokea tu kienyeji halafu ukategemea mambo yakawa shwari.
Nawakumbuka sana leo Nkuruma ,akina Sekou Toure mpaka Patrice Lumumba. Ingawa pia siwezi kumsahau Mwalimu Nyerere katika kundi hili. Nyerere na Nkurumah walirudi na kufanya mambo. Ingawa nafikiri Nkurumah aifanya maswala yake kabla ya muda wake. Maana jambo lake la kutaka Afrika yote iungane wakati sisi kama Watanzania bado hatujapata suluhisho kamili kati ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar , unaweza kuona ugumu uliopoa ukitaka Tanzania na Somalia ziungane.
Lakini hivi Ndesanjo hayuko Nyumbani?. Si ndio huyu huyu Ndesanjo aliyekuwa kwa nguvu zote akitetea Watanzania na Raisi wetu tulivyoitwa kuwa sisi Watanzania ni maimuna na Kikwete ni kiwete?Si ndio huyu huyu Ndesanjo apendaye kutukumbusha tutumie kiswahili katika mtandao kwa kuwa sisi ni Watanzania?Cha ajabu baadhi ya watu waliokuwa wananiuliza kwa nini akina Ndesanjo hawarudi nyumbanni waliniuliza hivyo wakitumia lugha ya kizungu.
Sasa kwanini bado sijarudi Tanzania. Jibu kubwa kuliko yote ni majukumu ambayo yana nibana ki jiografia sasa hivi. Je nitarudi Tanzania hivi karibuni? Jibu ni ndiyo. Je ninamshauri Mtanzania arudi nyumbani? Jibu ni ndio. Je We Mtanzania ulioko nje ya nchi urudi tu pale ki holela. Jibu ni hapana. Kumbuka ukirudi kiholela hata mchango wako katika jamii unaweza ukawa mdogo kuliko mchango wako ukiwa nje ya nchi.
Hivi tokea Wayahudi waanzishe mradi wao wa Israel ni asilimia ngapi bado hawajarudi? Hivi mchango wao nje ya nci si ndio uendelezao Nchi? Hivi wachezaji wa mpira kama akina Samuel Eto'o, mchango wao nje ya nchi hauifaidishi Kameruni?
Ntaendelea kujibu swala hili siku nyingine.
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ngoja nicheke kwanza! Kisha nimalizie kumwelimisha yule ndugu yetu wa nchi jirani, kisha tuje kwenye swali hili uliloulizwa kwa ile lugha bora kuliko zote duniani na ahera, kiingereza.
ni lazima mtajitetea kwa hali na mali,kumbukeni fimbo ya mbali haiuwi nyoka.mnaogopa kurudi nyumbani.
Usemacho Rasta kinaukweli wake.SI kila mtu ananguvu ya kutoogopa.
Simon!
Vipi ndugu yangu? Nimefurahia kusoma mawazo yako humu ndani. Nakukumbuka sana tangu mara ile ya mwisho pale Viitakivi, Finland.
Mzee Maggid asante kwa kunitembelea.Nakumbuka sana safari ile Viitakivi.Na nimeipenda blogu yako sana tu.
Post a Comment