Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Watu maarufu wachukuapo Watoto Yatima Afrika

>> Wednesday, October 18, 2006

Hivi karibuni swala la watoto yatima Afrika limekuwa jambo kubwa katika vyombo vya habari vya magharibi. Hasa ni baada ya Madonna kwenda Malawi na kuchukua mtoto mmoja wa kiyatima hapo. Nimekuwa nafuatilia mambo mengi yaliyozuka katika mjadala kuhusu kwanini ni sahihi au sio sahihi jambo hilo alilofanya Madonna. Wengi walisema kuwa mtoto wa kiafrika anapaswa alelewe na familia ya kiafrika ili awezekukua katika maadili ya kiafrika. Wengine wakasema kuwa mtoto ambaye hana ndugu wanaoweza kumlelea ,hana kwake ni afadhali apate tu pakuishi kuliko kutokuwa na sehemu aitayo nyumbani. Wako wengi wakasema, hawa watu wanatumia hii njia ya kudhamini watoto ilikujitengenezea jina zuri.Mimi ninakubaliana na wote. LAKINI NINGEPENDA WATU WOTE WASEMAO, WASEME ZAIDI YA MANENO MATUPU WAO WANAFANYA NINI KIVITENDO KUSAIDIA WATOTO YATIMA?Isije ikawa kuwa sio hawa watu maarufu kuwa wanajitafutia umaarufu, bali ikawa ni hao wawasemao akina Madonna ndio wakawa wanatafuta umaarufu.Chakujiuliza ni kwamba tunavyodai watoto wa kiafrika wanapochukuliwa kwenda nchi za magharibi wanapoteza Uafrika wao, je ni nini kinachotunza Uafrika wamtoto wa kiafrika Afrika kitamaduni sasa hivi? Kwa maana ni ukweli asilimia kubwa za mambo yanayozidi kumzunguka mtoto wa kiafrika Afrika yanamizinguo ya kimagharibi.Yaonyeshwayo kwenye televisheni ya asilimia kubwa ni ya kimagharibi.Shule zetu zinashinikiza elimu ya kimagharibi.Dini zetu ndio hizo zakutoka nje. Sasa tunafanya nini kumtunza mtoto wa Kiafrika abakie na maadili ya kiafrika? Halafu sisi Waafrika tunafanyanini kumfanya mtoto wa Kiafrika aliye nche ya bara la Afrika kujivunia Afrika? Je tunaendeleza vita na njaa+ je tunaendelea kujidharau wenyewe?

Nachoshukuru moja ya jambo lililojitokeza katika mshawasha huu ni kuwekwa hili swala la watoto yatima kwa siku kadhaa katika kurasa za mbele za vyombo vingi vya habari duniani. Natumaini kama umaarufu basi uwe katika swala zima la tatizo hili na sio kwa watu binafsi.Kwani inajulikana kwa miaka mimi wako watu binafsi ambao wanafaidika na miradi ya watoto yatima zaidi ya watoto yatima wenyewe.Tatizo hili ni kubwa.Na ninawapapongezi wale wote wajitoleao kwa moyo kusaidia kwa lolote wawezalo kutatua swala hili.

Hivi unahisi Michael Jackson angetaka kuadapti mtoto angeadapti kutoka wapi?

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 11:30 am  

HUU NI USHEZI WA HALI YA JUU NA PIA TUNAPOTOKA KWA SABABU MWISHO WETU WA KUONA MBALI NI MWISHO WA PUA.SASA NDUGU ZANGU SERIKALI INASHIDWA KUWAHUDUMIA WATOTO YATIMA?HEBU NIAMBIE,KAMA SERIKALI INAWEZA KUNUNUA MASHANGINGI,SEMBUSE WATOTO YATIMA.HILI TUKIO NI AIBU KWETU SISI WAAFRIKA.

mloyi 4:40 pm  

Funzo kubwa sana tunapata hapa? Marcus Garvey alisema katika kutapatapa kwamba watu weusi hawatamuunga mkono muda ule lakini siku ikifika wakiwa "back against the wall" hawatakuwa na chaguo bali kujiunga naye na kuwa tayari kwa lolote kwa faida yao.
Sijui sisi tunajifunza nini hapa? tumeiga taratibu za magharibi imefika wakati mtoto wa kaka yangu tumbo moja na mimi anakosa nyumbani! Sijui kama babu yangu akifufuka leo akakuta hali hii ataniangalia vipi?
Mifumo ya kimagharibi haitusaidii tunavyopenda, inatuumiza roho zetu zaidi ya kutupatia furaha, kama unabisha, angalia unavyojifikiria ukikuta vitoto vimejikunyata kibarazani pale Posta wakitafuta usingizi usiku wa manane!, sijui kama kuna mtu huwa anipendelea hali ile iendelee.
Tatizo kubwa ni kuvunjika kile kilichokuwa kinaitwa "clan organization" miongoni mwa jamii zetu, kama tutaweza kurudisha hiki kitu basi jamii yetu itakuwa bora sana kuliko zingine zote.

luihamu 6:37 pm  

mzee mloyi kulikoni?kwanini hauandiki?pia ile email yako iligoma,send it again.respect man

luihamu 8:08 am  

Mzee Simon,naomba uchangie mada kuhusu mkutano wa wanablogu kutoka Afrika,tunahitaji sana maoni yako mzee.

NDABULI 9:55 am  

Nakubaliana na wewe Kabisa bwana Simon hao wanajiita wanaharakati watueleze waliisha saidia nini kile kituo huyu mtoto alipokuwa anaiishi,lakini Madona pamoja na kumchukua mtoto anakisaidia pia kile kituo. Mimi kwa mtazamo wangu naona hizo pesa za kuendesha kesi wangizitumia kwa shughuli zingine kwa ajili ya watoto waliobaki. Naona wao wanataka kujitangaza kwa mgongo wa watu wengine.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP