Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mtazamo wa Kiafrika

>> Tuesday, October 17, 2006

Kuna kipindi hapo nyuma niliongelea kuhusu jinsi Watanzania tunavyoweza kutoa heshima zote kwa wageni katika nchi mambo hambayo hatupeani wenyewe. Nilisoma habari moja iliyotoka kwenye tovuti ya The Black Star News, ambayo ilinigusa pia. Hii habari ilikuwa inaongelea jambo la kuenzi wageni kuliko wazawa nchini Kenya. Inasemekana Seneta Barak Obama, alipata muda wa vyombo vya habari kuliko mwanasiasa yeyote mwingine Kenya . Lakini kilichoniua ni kwamba inasemekana hata timu ya mpira wa miguu ya Kameruni ilipofika Kenya ,maafisa wa Kenya wakaiondoa timu ya Taifa ya Kenya kwenye uwanja mzuri iliiipishe ya Kameruni. Kumbuka ni katika kipindi ambacho timu ya Kenya ilipokuwa inajiandaa kucheza mechi ya kimataifa. Soma habari hii mwenyewe:
African Inferiority Complexes. Mtazamo huu wa kimawazo nimeushuhudia sana Tanzania.

Sawa watu wengi husema sisi Watanzania ni wakarimu. Lakini mimi nahisi ukarimu wa kuufanya tu kwa kuwa tu mgeni kutoka nchi za nje anahusika hautatupeleka mbali.

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 9:19 am  

mzee Kitururu inabidi tubadilike,wewe upo nje ya Afrika,je!noa wazungu wanakupa heshima zote?
kuna kipindi uliandika yakwamba kabla mwafrika hajarudi nyumbani lazima aandae mambo kwanza yani kuweka mambo safi hapa nyumbani,je ukishindwa kuweka mambo fresh?Mara kwa mara najiuliza kwa nini waafrika wengi wanaogopa kurudi Afrika?Je!huko nje mnathaminiwa?au ndiyo yale mambo ya (SLAVE DRIVER).Swali jingine kati yenu ninani anaweza kuviva viatu vya MARTIN LUTHER KING AU MALCOM X?kama hilo swala ni gumu kidogo,basi naomba unijibu ni nani kati yenu atafufua THE BLACK STAR LINER?JAH LIVE.

Anonymous 5:21 pm  

The best swahili blogg I have been !
Keep up th egood works

Simon Kitururu 9:25 pm  

@Luihamu, nimekujibu hapo juu!
@anonymous, thanx for the compliment. Karibu tena!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP