Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Vilevi vya akili

>> Sunday, October 08, 2006

Kilevi kikubwa kisicho cha kawaida ni dini.
Pombe kwa Wabongo, na karibu kila kabila lina vyake.
Bangi Wahindi. Wajamaika nk....
Pombe kali, Warusi, Wafini nk.........
Bia, Wajerumani. Wana viwanda zaidi ya 1200 vya kutengenezea kifyonzo hiki.nk..........
Sigara, Wahindi wekundu, dunia, nk.........
Ngono, Dunia.nk......
Elimu, dunia. nk.........
Je umelewa?
Kilevi chako ni nini?
Je ni ngono?

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 12:42 pm  

MIMI KILEVI CHANGU SANA NI KILIMO.HIVI MZEE SIMON WEWE NI RASTAFARIAN AU NI RASTA BUSINESS.SAMAHANI KWA KUULIZA.

Simon Kitururu 1:11 pm  

Mimi sio Rasta kiimani. Mimi Muafrika tu.Nilizaliwa Mkristo mitaa ya wakati wa sekondari nikaokoka , halafu nikageuka kuwa rasta kiimani. Nikarudia ukristo halafu mwishoni nimekuwa naamini Mungu lakini bila kujihusisha na institution yoyote.Nafuata zaidi uafrika na na machale yangu mwenyewe.

Anonymous 1:52 pm  

Hapo Simon nimekupata. Sijui kwanini ukimwambia mtu kuwa wewe mwafrika anabaki kuuliza, wewe ni dini gani? Uafrika wangu unanipa mitazamo kuhusu masuala makubwa duniani ikijumuisha masuala ya kiimani. Utamaduni wetu umebeba sio tu masuala ya ngoma (kama wengine wanavyodhani) bali pia falsafa za masuala ya dini, imani, n.k.

Halafu sijui kwanini watu wakiona mtu ana nywele msokoto mara moja wanakimbilia kukuita rasta. Mbona kuna marasta wengi sana wasio na nywele kama zako?

Ndio blogu zetu basi tuzitumie kupanua maarifa ya masuala haya.

luihamu 1:14 pm  

Samahini nadhani hatujaelewana,katika picha yake mbele kuna lilevi,nikaamuwa kuuliza.kwahiyo kama wewe sio mmoja wa wana wa Yosefu sawa endelea kupata kilevi.

luihamu 1:15 pm  

samahani sio lilevi ni KILEVI.

luihamu 1:18 pm  

Msiogope kujiunga na rastafarian,sio wavuta bangi,ni watoto wa Yosefu mwana wa Israeli.

Simon Kitururu 9:29 pm  

@Msemoooo!Nimekubali:-)
@ndesanjo, nahisi unajua nimefikiria nini baada ya kusoma ulicho andika.
@Luhiamu, nimekujibu kwenye atiko ya juu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP