Tanzania gizani!
>> Tuesday, October 17, 2006
Kila nikisikia juhudi za viongozi wetu kufanya ziara duniani hujiuliza hivi ni wawekezaji gani ambao ni walengwa? Karibu wawekezaji wote hawataweza kufanya mengi ikiwa hakuna umeme wakuendeshea shughuli. Labda ikiwa walengwa sasa ni wale wawekezaji ambao watasaidia kutatua matatizo ya umeme au safari hizi zenye gharama za kutafuta wawekezaji hazitakuwa na manufaa sana.
Chakujiuliza tu ni kwamba:inawezekanaje katika nchi za Afrika Mashariki ni sisi tu tunaathirika sana na swala hili la umeme mara nyingi kuliko wengine?
Je, kwanini hakuna mipango ya muda mrefu ya kujua jinsi ya kukabiliana na swala hili la umeme?
Hivi katika maswala ya kupewa kipaumbele, ndege ya raisi, radar ya jeshi au umeme uwezeshao viwanda kufanyakazi ni nini muhimu sasa hivi?
Je umeme kuwepo siku za mapumziko na kukatwa siku za kazi sio dalili kuwa wahusika wanatoa kipaumbele potofu?
Natumani siku moja taifa letu litafikia uwezo wakutabiri maswala yafaayo kupewa kipaumbele katika wakati ufaao kuandaa matatuzi.Kwa maana kama ilikuwa haijulikani kuwa taifa litaingia katika kisa hiki kabla basi sishangai Tanzania ikijikuta inakabiliana na kasheshe nyingine kama hii kienyejienyeji tu.
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment