The revolution will no be televised-Gill Scott Heron
>> Thursday, October 05, 2006
Mzee Gill enzi hizo
Ukitaka kufanya mapinduzi jishughulishe kw vitendo.Ndivyo alivyokuwa akisema Mzee Gill-Scott Heron.
Kwa kweli Luninga inadaka baadhi ya mambo katika mapinduzi, lakini mapinduzi halisi yako mtaani kwa Bi kidude na kwa Mzee Hamdala pale kijiweni.
Leo nimemkumbuka Mzee Gill-Scott Heron baada ya kupitia baadhi ya mashairi yake.
Nasikitika Kuwa huyu Mzee ana ukimwi .Lakini ninamshukuru kwa kunifikirisha mambo kibao. Unakumbuka shairi lake lisemalo, Weupe wako mwezini wakati siye tunahaha?
Duh! Inanikumbisha tu kuwa Tanzania mpaka sasa hivi upande mmoja unaweza kukumbwa na njaa wakati mwingine vyakula vinaoza!
Ingawa Mzee Gill anamambo sikukubaliani nayo lakini bado hata katika hilo anaendelea kunifikirisha. Asante Mzee Gill-Scott Heron kwa hilo.
Mzee kwenye Hardtalk
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Hawa ndio vichwa ngumu wenye vipaji. hakuna kitu kama compromise na hawa.
Kulikoni kichwa ngumu mwingine Fela naye pia alikamata umeme.
Ahsante kwa kutukumbusha.
Post a Comment