Dini ni za amani na upendo?
>> Monday, November 13, 2006
Kila siku ukitazama au kusoma habari utasikia kasheshe za mikwaruzano duniani. Mambo mengi ya vita na majanga utayaona yakiwa kurasa za mbele za magazeti. Cha kushangaza ni kwamba baadhi ya mikwaruzo hii utaiona inaendeshwa na watu wanaosema ni wanadini zipendazo amani. Kinachoshangaza ni jinsi gani hizi dini zisemekanazo ni za amani zilivyokuwa na misingi ya utenganishi. Au hivi ni hawa wanadini tu ambao uzigeuza hizi dini kuwa chanzo cha utenganishi?
Hebu tuangalie baadhi ya chokochoko hizi:
Israeli na Wapalestina ni kawaida kabisa kuwakuta msitari wa mbele katika kupigana. Hawa pamoja na mambo mengine tofauti za dini zao ni moja ya jambo kubwa lifanyalo wabwengane. Hivyo hapa tunawakuta wale wenye dini ya kiyahudi wanabwengana na waislamu. Na wameanza zamani! Je, unawakumbuka Falashas au Beta Israel?Hawa ni wale Wahahudi Wakiethiopia. Kuna theori zinaeleza uondokaji wao baada ya ufalme wa Judah kugawanyika mara mbili na baada ya Jeroboam kumrithi Mfalme Solomon.Na baadhi ya mambo anukuliwayo ni pamoja na dini yao. Nilipenda kuwagusia kidogo Waisraeli hawa weusi hapa kwasababu mpaka leo wana mikwaruzo ya kidini Ethiopia.Na pia mzungukowao wakukimbia Israel mpaka sasa hivi warudishwapo Israel umejaa mikwaruzo ya kidini. Wako bado mafalasha kwa maelfu ndani ya Ethiopia ambao wanasubiri kuchukuliwa kwenda Uisraeli.
Waisraeli weusi ndani ya Ethiopia walikuwa na mikwaruzo na wakristo na waislamu pia. Wako ambao walilazimika kubadili dini na sasa wanarudia uyahudi ambao wanaitwa Falash Mura. Lakini wapo wanaoamini kuwa baadhi ya Falash Mura wanarudia Uyahudi ilikuweza kurudi Irael. Chaajabu ndani ya Israel wanabaguliwa kwa rangi na hata kidini na Wayahudi wa kiothodoksi.Wayahudi wakiothodoksi wanaamini Mafalashas kuwa sio wayahudi kamili.
Tukiondoka mashariki ya kati ambapo kasheshe liko wazi tunaweza kukatua mitaa ya Marekani kusini. Ukienda nchi kama Brazili , mikwaruzo ipo kati ya Wakatoliki na Maprotestanti. Hili utalikuta kwa Waairishi pia ndani ya Ulaya.
Ukienda India utakuta kasheshe iko kwenye Wahindu na Waislamu, Wahindu na Wakristo, Waislamu na wakristo bila kuwasahau Wahindu na Masikh. Ukidondoka Pakistani utakuta kasheshe kati ya Waislamu na Wakristo, Waislamu wa Sunni na Shia.
Ukienda Australia utakuta mikwaruzano kati ya Wakristo na dini za Kiaborijini na pia na waislamu pia.
Kwa haraka haraka utakuta kila kona ya dunia kuna mikwaruzo ambayo waiendeshao wanadai wako ndani ya dini zipendazo amani. Sasa ni nini kiko ndani ya dini hizi ambazo zafanya wanadini wakwaruzane bila upendo?
Sijaisahau Tanzania katika hili. Dini inayoonyesha kutulia kuliko zote ni ya kipagani ndani ya Tanzania. Sijawahikusikia wasio kwenye dini za amani zilizoletwa wakichimbiana mikwala na wenye dini. Sijawasikia wakilalamika kutoalikwa kwenye ubwabwa na Raisi Jakaya kikwete. Tanzania kuna chokochoko kati ya Waislamu na Wakristo.Kuna misingi ya chikochoko ndani ya makanisa mbalimbali. Kila thehebu hutakakuhalalisha ukweli wake kwa kujenga hoja za kukosoa jingine.Hivyo timu zipo umekosekana uwanjatu na mashabiki.
Ukirudi Israeli , Mafalasha wanabagulia na wanadini wenzao wayahudi wakiothodoksi. Ukirudi Iraq waislamu kwa waislamu wanabwengana kwa misingi ya nani ni msunni na nani Mshia. Kunakipindi ilinishangaza mitaa ya Kilimanjaro kukazuka mpaka ugomvi kati ya Waluteri na Waluteri wenzao.Kisa wanagombania dayosisi iliwaendelee kumtukuza Mungu wa amani. Sasa sababu zinasemekana kuwa ziko nyingi! Sasa sitashangaa kasheshe likizushwa kutokana na sababu hizi zisemekanazo kuwa nyingi!Chakusikitisha ni kwamba watu tunashindwa kujifunza kutokana na mikwaruzo hii ambayo mingine ni ya maelfu ya miaka. Pale Juu niligusia zaidi swala la Beta Israel kwasababu unaweza kustukia jinsi gani misingi ya amani ikawa inakuletea mikwaruzo anga zote za dunia uamiako.Nazidi kujiuliza, kwanini dini zetu za amani zinaleta utenganishi namna hii? Je Tanzania tutaponyeka kuingia katika kasheshe kubwa zaidi ya tuliyonayo sasa kutokana na dini hizi za amani?Sijui , niko bado ndani ya Treni hii ya mawazo
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mzee Simon,gazeti tando la rastafarian limeungana na gazeti tando la rundugai kijiweni kwa hivyo nitakuwa napatikana katika
www.rundugai.blogspot.com
karibu sana.
Mzee Simon,kabla ya wakoloni kutuwa afrika,babu zetu hawakuwa na dini?na kama walikuwa na dini walikuwa na mikwaruzano?la hasha babu zetu walikuwa na dini zao safi kabisa waliabudu kutokana na imani zao na Mungu aliwasikia na kuwabariki.Tatizo ni MILA NA DESTURI,tumesahau tulipotoka na kujiingiza katika dini zilizo letwa na wakoloni.Kwa nini tunakuwa na madhehebu kibao wakati Mungu ni mmoja?Kwa nini kila dhehebu lina tamaduni zake na sheria zake?Tukiweza kupata majibu haya na kurudi katika MILA NA DESTURI ZETU TUTAFANIKIWA.Kwa nini tunaamini sana huyu Mungu wa wakoloni?waliwauwa na kuwateza ndugu zetu,wakawatumikisha katika mashamba yao wakawafanya watumwa,leo hii badu tunamwabuda mungu wao,kichekesho.DINI NA IMANI SAFI NI RASTAFARIAN.
Mon Simon,
Mjomba, siyo siri unanimaliza sana na maoni yako: Unanimaliza kwa habari unazoleta, na zaidi unanimaliza kwa jinsi ninavyokufahamu na jinsi unavyoweza kufanya unayoyafanya tena kwa ufasaha sana. Ama kwa hakika wengine mliumbwa kwa udongo na mali ghafi zingine tofauti.
Keep it up, Sir Kusto,
F MtiMkubwa Tungaraza.
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa baadhi ya Watu wanatumia Dini kuwa chanzo cha ghasia wakati Dini zinapaswa kuwa za amani na upendo;
kwa sasa napatikana kwenye www.ndyemalila.blogspot.com
Asante F Mtimkubwa Kwa kunitembelea! Nasubiri blogu yako najua iko jikoni.
Asante Edson kwa kunitembelea!Karibu tena!
Post a Comment