Kwa wapendao mpira wa vikapu, mnamkumbuka Dr. James Naismith?
>> Tuesday, November 14, 2006
Dr James Naismith akipozi na gozi la mpira wa kikapu enzi hizo
Kwa wapenda michezo naamini mnamkumbuka huyu daktari aliyebuni mchezo wa Basketi Boli. Ninachojiuliza ni kwamba katika mazingira ya kwetu tumetosheka na michezo iliyopo ambayo mingine hata kutokana na umasikini hatuwezi kushiriki? Nakubali tunamichezo mingi Tanzania. Nakubali tuna michezo kuanzia bao mpaka mieleka ya asili. Je, katika shule zetu bado kunaruhusiwa ubunifu wa michezo ili kukidhi matakwa ya mazoezi ya viungo ya Wanafunzi? Nakubali kuwa tuendelee kuipa kipaumbele michezo hii ambayo inashindaniwa kimataifa duniani. Nakubali kuwa huyu Dr J Naismith alibuni mchezo huu kuwaondoa wanafunzi kuboreka wakati wa kipindi cha baridi(winter) ambapo wanafunzi walifanya mazoezi ndani ya maholi. Lakini kwa Tanzania naamini kuboreka kwa wanafunzi katika maswala ya mazoezi kupo sana.Je hii sio changamoto ya kuchochea haja ya mchezo mpya? Na sasa hivi vijana wengi wanaacha kabisa kufanya mazoezi na kubobea mbele ya Luninga kujadili mechi za Uingereza. Sawa, inawezekana hawa ni wachache wafanyao hivyo. Lakini unaonaje muelekeo wa vijana kwa ujumla ukiweka mazoezi ya viungo kama kigezo?Labda hatuhitaji mchezo mpya!Labda ni kibano cha maisha kisababishacho kushuka kwa ushiriki kikamilifu katika michezo kwa vijana! Lakini nchi nyingi ni hasa wenye kibano ndio wanaibuka kuwa kiboko katika michezo. Ukienda Brazili akina Pele ni ushahidi.Inabidi kuangalia tena uhamasishaji wa michezo, mfumo mzima na streteji za kufanikisha michezo bongo. Naona Raisi Kikwete anapenda michezo sio kama Mwalimu Nyerere ambaye pamoja yake mazuri mengi aliyofanya, alishindwa kuona umuhimu wa michezo kama silaha moja wapo ya kujenga Utaifa. Labda hatuhitaji Dr Naismith wa kibongo!Nawaza tu usiogope!
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mzee Simon,ingawa tamaduni za rastafarian zinapendekeza sana mtu ucheze mpira wa miguu lakini mimi nasukuma sana mpira wa kikapu,ukinikuta uwanjani huto amini mambo yangu nacheze kwa kujituma na kupenda mchezo,leo umenifunguwa macho tena si kuwa na habari nani alianzisha mchezo huu lakini kutokana na kublogu nimejifunza.I salute you sir.
Samahani nyote kwani Kiswahili bado najifunza. Mimi nilizaliwa hapa U.S.A na wazazi ni kutoka Nigeria. Marafiki wangu wengine hutoka East Africa. Nawakaribisha nyote kutazama homepage yangu hapa. Asante
Post a Comment