P.W. Botha afariki
>> Wednesday, November 01, 2006
P.W Botha-The great Crocodile
Mamba mkubwa , ndivyo alivyoitwa P.W. Botha. Huyu Mzee mpaka kufa kwake hajawahi kukiri wala kuomba msamaha kwa uhalifu wa serikali yake kwa watu weusi Afrika kusini. Pia alivyo ulizwa ingekuwaje kama watu weusi wangechukua nchi mwaka 1948 wakati chama chake kilichukua hatamu akasema nchi ingeharibika. Mpaka anafariki hakuamini katika kipaji cha uongozi wa mtu mweusi. Lakini je kwa mifano ya viongozi wetu Afrika na rekodi zao za uongozi unaweza kumlaumu huyu Mzee kwa kufikia kuamini watu weusi hawawezi uongozi? Amefariki akiwa na miaka 90. Natumaini kuwa karibu Afrika itaanza kupata viongozi ambao wataturudishia heshima yetu Waafrika na wote wenye rangi nyeusi. Kabla hawajatokea changamoto aliyoacha P.W. Botha ni kwamba: je, si ni kweli mpaka sasa viongozi wetu weusi ndio wanazidi kuchangia kuporomoka kwa nchi zetu za Afrika?Kama viongozi wanabisha Botha hakuwa anasema ukweli kuhusu uongozi mbovu wa viongozi wa kiafrika basi wafanyekazi na kutukwamua katika matatizo yetu Waafrika. Haya naona hata Mo Ibrahim anataka mpaka kuwalipa pensheni ilimfanyekazi.Fanyeni kazi basi, AlaaH!Habari zaidi hapa
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mbu amefariki, ubabe wake utasahaulika. Binadamu anaishi kwa amani.
Huo ndio ukweli wenyewe, Botha katika siku zake alikuwa ni mtu wa kutoa amri mbaya mbaya sana, hakujua nani wa rika lake au nani mkubwa kwake wala nani mdogo kwake, watu weusi hakuwaweka katika tabaka la binadamu kabisa, hakutaka ubaguzi uishe pale Tshwane (Pritoria).
Hakuwa ankemea watu hivihivi bale alikuwa anawanyoshea na vidole kuonyesha ubabe wake, hakuthubutu kustahi jambo asilolipenda, alivunja maandamano kwa nguvu kubwa sana, hakuwa na busara kwenye kutuliza fujo, Jeshi la kibaguzi ndio lilikuwa ngao na tegemeo lake.
Botha akiluwa ni hatari kuliko tuambiwavyo kuhusu Saadam, hakukubali kuomba msamaha kwa madhambi yake kwenye tume ya upatanishi, alisema alichokuwa anafanya kilikuwa sahihi kwa katiba iliyomuweka madarakani! hivyo hawezi omba msamaha.
Hakika hatujaambiwa mambo ya Botha, sijui kwa nini hawamfuatilii wanahangaika na pinochet tuu.
Post a Comment