Kikao cha wanablogu wa Tanzania.
>> Thursday, November 23, 2006
Kutokana na kuchelewa mkutanoni kutokana na matatizo ya kiufundi nimeona niandike tena kile ni lichokuwa nimechelewa kukipa sauti yangu kuhusu mkutano wa wanablogu.
1. Mikakati ya Kufikisha Ujumbe wa Wanablogu kwa Watu Wengi Zaidi:
Nakubaliana na yaliyo jadiliwa kikaoni. Lakini ningeshauri kuwa kuwepo ndani ya jumuia kamati yenye kufuatilia yenye 2/3 ya watu walioko Tanzania wenye kazi ya kufuatilia nukuu zizungumzwazo katika magazeti redio na Televisheni ili wote wanablogu ambao hatutakuwa tuna jua wamenukuu nini nadani ya Tanzania tuweze kujua kuwa tumenukuliwa kisahihi. Pia kama tumenukuliwa vibaya au kutokueleweka tuweze kupata nafasi ya kujitetea au hata kusawazisha vyombo vya habari kwakutu nukuu vibaya.Member waliobaki watashughulikia maswala ya Wanablogu kama wanukuliwavyo nje ya Tanzania.
2. Maadili:
Nakubalia na na mawazo yaliyotolewa kikaoni.Lakini lazima uhuru wa mwanablogu kusema apendacho lazima ubakizwe. Lugha safi ni muhimu lakini itambulike watu tofauti huchukulia kuwa wametukanwa katika vigezo tofauti. Mimi nashauri lugha ambayo ikataliwe ni ile tu ijumuishayo matusi ya nguoni. Pia mtu yeyote ndani ya jumuiya atakaye fikia kumdhalilisha mtu au nchi kwa kutumia blogu yake bila sababu maalum ambayo anaweza kuzitetea atolewe kwenye aggregator na pia hoja zake zikanwe na kamati maalum ya maadili. Nashauri atolewe ndani ya aggregator kwa muda wa mwaka na ikiwezekana wanajumuiya kumtoa katika viunganishi vyao. Kurudi kwake katika jamii kutokane na kuomba kwake msamaha kwa aliye dhalilishwa kwa kuandika hivyo kwenye blogu yake.Pia lawama za adhalilishawe ziwekwe kwenye tovuti ya jumuiya.
Picha ziwezazo kumdhalilisha mtu pia ziangaliwe.Lakini kama zina ukweli wa hoja zinazoweza kutetewa kwa mtazamo wangu zinaruhusiwa.Ila maswala ya picha za ngono na wasiwasi yanaweza kuteteleza madhumuni ya jumuiya nzima kwa kusababisha kuhusisha na kupotosha mwelekeo wa jumuiya nzima.Sipingi kuwepo kwa blogu za ngono Tanzania kwa sababu ngono ni jambo linalotakiwa kuongelewa, lakini mpaka sasa sijaona blogu ya ngono ambayo inaelimisha Mtanzania maswala ya ngono. Nashauri blogu ya ngono itakayo kubalika ni ile tu ambayo hailengi udhalilishaji wa mtu yeyote na yenye ujumbe uhitajikao katika jamii. Kwa mfano mimi naweza kuikubali blogu ya ngono iwafundishao vijana uroda na madhara yake na jisi ya kuuvinjari kiusalama na kiafya. Blogu za ngono ziwekayo picha za watu ambao hawakutoa idhini ya kutolewa picha zao na kwa madhumuni ya kuwaletea washawasha na ashki wasoma blogu na isiyofundisha mimi nadhani zisikubalike kwenye jumuiya.
Kusiruhusiwe kutukania watu dini zao.Lakini isije tu ikafikia kuwa maswala ya dini ni mwiko kuyaongelea.
Kamati ya ushauri wa maadili iwe inatoa mawazo ambayo wanajumuia watayapigia kura . Kwa mfano ili mtu kutolewa kwenye jumuia ingekuwa vyema kuwe na wiki nzima ya wanablogu kupigia kura uamuzi.Hii ingefanyika kama tulivyo pigia kura tarehe ya siku ya blogu.
3. Jumuiya:
Naunga mkono swala lakuwa na jumuiya iliyo sajiliwa. Naamini itatoa nguvu zaidi kwa wanajumuiya hasa katika maswala ya haki za wanablogu na kazi zao na pia maswala ya kuaminika.(credibility).
Katika tovuti ya jumuiya kuwepo na muhtahsari wa yaliyosemwa katika vyombo vya habari kutoka blogini.Pia kuwe na nyumba ya kuchat na forum ambayo itawezesha wanablogu kukutana mara kwa mara ikiwezekana wakitumia majina watumiayo kwenye blogu zao.Kuwepo na ukurasa wa maoni ya wanablogu na chumba cha ushauri kwa jumuiya ya wanablogu. katika chumba hiki mambo mbali mbali ambayo yanapendekezwa kufanyiwa kazi na kamati ya jumuia yatawekwa wazi.
4. Uongozi:
Nakubaliana na Uongozi wa muda ulioteuliwa .Ningependa jina uongozi lisitumike bali tutumia jina la wawakilishi.Tuwe na kamati ya wawakilishi katika kamati mbalimbali.Kwa mfano tuwe na kamati ya maadili. hii itafuatilia kuwa tunafuata miongozo tunayopanga yakutuongoza kuendelea kuwa huru lakini sio kuwa vyomo vya chuki na kashfa kwa watu. Tuwe na msemaji mkuu ambaye ndio atakuwa anahakikisha kuwa hata katika mikutano yetu hatupitilizi kupita wakati. Tuwe na kamati ya ustawi wa blogu za kitanzania. Hii itahakikisha maswala ya muonekano wetu na ni kwa jinsi gani tunawakilishwa katika vyombo vingine vya habari. Kamati zote ziwe na watu watano. Kwa sababu ni kawaida kwa wanablogu kuzidiwa na shughuli wakati mwingine hivyo kukosa muda wa kufuatilia mambo au kuandika mambo . Tuwe na kamati ishughulikiayo maswala ya elimu ya teknolojia hii ya kublogu na jinsi gani wanablogu na wananchi wataweza kujiboresha zaidi katika matumizi yake. Hapa na maana maswala ya uboreshaji wa blogu zetu na pia maswala ya ufundishaji au uelimishaji wa maswala ya blogu.Kuwena msemaji mkuu wa jumuiya ambaye yeye kwa kupitia ushauri wa jumuia nzima anaweza kuisemea jumuiya ibidipo.
Kuwe na kamati maalumu inayofuatilia jumuiya kama NGO. Hii itakuwa inafuatilia pia jinsi gani tunaweza kujenga akauti ya Jumuiya itakayo wezesha maswala yatakayo hitaji pesa . Mfano, ikiwa mwanablogu yuko matatizoni kutokana na mambo aliyo wakilisha bloguni.Mfano ikiwa tutahitaji kuwa na fund yetu kama wanablogu ya kusaidia maendeleo ya kitu tukubalianacho.Iwe ni watoto yatima au uhuru wa habari nk.
Kuhusu Jina ningependa katika kila kitu tutumie majina ya Kiswahili. Jina la jumuiya mimi na shauri liwe:
Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania(JYWT).
jina la Aggregator, mimi ningepenga jina liwe la Kiswahili au Kifupi cha jina la Kiswahili
Mfano wa majina niyafikiriayo ni:
Bloguni Wasemaje(BW)
Sauti za Watanzania Bloguni(SWB)
Kipya Katika Blogu za Watanzania(KKBW)
Kuhusu muda wa wawakilishi kuwepo katika kamati ningeshauri muda wa miaka miwili . Kila baada ya miaka miwili tungepiga kura kuchagua wanakamati wapiya au kuwabakiza wale ambao tunaona mchango wao una umuhimu wakuendelea kwa muda mwingine.Kuwepo na uwezekano wa kuitisha kikao cha dharura cha kutengua uwakilishi wa mtu katika kamati. Kwa ujumla jumuiya ibakie kuwa ya wanablogu wote hakuna kiongozi wala afuataye bali wote kwa pamoja tukienda mbele. Wawakilishi wanapewadhamana kuwakilisha wanablogu kurahisisha ufanisi wa jumuiya tu. Ila ni wajibu wa jumuiya nzima kuhakikisha kuwa tunakuwa nguvu ya kuelimisha , kuhabarisha, na ya kujikomboa.
11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Napinga kamati ya muda,tunaomba kufanya uchaguzi wa huru na haki kuwachaguwa viongozi wa jumuiya.
Kitururu, naona umetuanzishia safari yetu kwa mawazo kemkem. Nimependa mfumo uliotumia wa kuweka kila kipengele na kukichambua. Pengine tunaweza kusema kila mwanablogu anayependa kushiriki atumie mfumo kama huu.
Nitaweka kona maalum ya bunga bongo ya mambo haya, kisha nitabandika mawazo yako.
Luihamu: tutumie lugha gani kukuelewesha? Jumuiya haina viongozi. Hakuna mtu anayetuongoza hivi sasa.
Halafu badala ya kurudia sentensi hii: tufanye uchaguzi
Ingekuwa jambo la busara ungekuwa unajibu hoja zinazotolewa dhidi ya mawazo yako. Hoja zinatolewa, unaulizwa maswali, badala ya kujibu na kuitetea hoja yako kwa kina unaendelea kusema, "tufanye uchaguzi."
Rasta, vipi?
kwenye uongozi umependekeza jina 'wawakilishi"
Kwenye ukurasa wa wikipedia kabla ya mkutano nilipendekeza neno neno "wasimamizi" nikichelea kwamba neno 'kiongozi"linaweza kubeba dhana tofauti na utoaji huduma au kutumikia.
Katika maana halisi akina Damija walipewa majukumu ya kutekeleza.
Mimi sijuiui kwanini sipendi katika blogu tuwe na wasimamizi. Nahisi wasimamizi wanakua wanatuangalia chini. Wanatusimamia nini lakini?Viongozi pia naona wanatenda tendo la kuondoa majukumu ya kila mwanablogu kuchukua majukumu fulani fulani kwasababu kuna kiongozi. Hivi neno kiongozi limetokea wapi?
Sina neno la kusema likaeleweka.
Nina maana kama mtu angepewa jukumu la kusimamia shughuli ya ujenzi wa tovuti ya kikusanya habari kwa mfano, basi huyo asimamie hiyo shughuli mpaka itimilike. Sina maana ya kusimamia wanablogu wengine kwamba wanafanya nini, au awaelekeze la kufanya, la hasha - nina maana ya kusimamia kazi. Coordinator/project officer au kitu kama hicho.
Nitaondoa kwa muda neno "usimamizi" naweka neno "wenye majukumu" yaani wale watakaofanya kazi fulani.
Katiba ya jumuiya itaundwa bila wawakilishi wa kudumu?kama katiba itaundwa na wawakilishi wa muda na wao waipitishe hawa wakudumu wanaweza kuipinga,napendekeza tuwe na wawakilishi wa kudumu ili wasimamie katiba yetu na jumuiya yetu.Kabla ya kujenga nyumba lazima ununue kiwanja kisha uchimbe msingi,lakini sisi tunapendekeza tuchimbe msingi kabla hatujanunua kiwanja.napendekeza wawakilishi wakudumu kwanza ili wasimamie katiba ya jumuiya ya wanablogu wa Tanzania vile vile wawakilishi watoke Tanzania.
Mwandani nimekupata katika neno usimamizi.
Rasta Luihamu sinauhakika kama nimekuelewa. Kwa maana nachojua mimi ni kwamba sisi wote wanablogu ndio tunahusika kujenga katiba. Kuubalika kwake au kupingwa kwake ni jukumu la wanablogu wote na sio kikundi cha wakudumu au wa muda. Kwanza hata hili neno la wakudumu nahisi linatuchanganya bure kwa maana navyoelewa ni kwamba kila baada ya muda fulani tutakuwa tunapiga kura kuchagua watu wengine. Mimi nilikuwa nashauri kila baada ya miaka miwili.Kuhusu mambo ya kwamba tunachimba msingi bila kununua kiwanja sikuelewi. Kwa mtazamo wangu Rasta Luihamu wewe ni muwakilishi wa kudumu.Sioni sababu kwanini hili swala la Uongozi ni muhimu sana kwako Rasta namna hii. Ufanikiwaji wa jumuiya unataka jumuiya nzima na kila mtu ni muhimu
Jumuiya ya Wanablogu WaTanzania. Mfumo gani utumike kufikia lengo hili? Ninahisi kuwa mkutano uliofanyika hivi majuzi wa kutuleta pamoja wanablogu WaTanzania haukumaliza kujadili mambo mengi. Mojawapo ni hili analolipigia kelele Rasta Luihamu. Wanakamati walichaguliwa. Hata hivyo,muda wa kamati hiyo ya muda haukupangwa. Malengo ya kuchagua kamati hiyo yaliwekwa bayana.
Hivyo basi, ninashauri, kama ambavyo nimekuwa nikishauri, kuwa tuwe na mkutano mwingine. Mkutano huu ujadili na kupanga ratiba ya matukio yote muhimu katika mchakato wa kuanzisha Jumuiya iliyosajiliwa kisheria.
Muda ambao ninashauri ufanyike mkutano huu ni ndani ya mwezi wa December. Naamini wakati huo, wanablogu wengi watapata fursa ya kuingia ukumbuni na kutoa hoja zao humo tofauti na ilivyokuwa katika mkutano uliopita. Ninapata hisia kuwa kuna wanablogu wengi tu tulibaki nje ya ukumbi pasipo kuingia ukumbini.
Jambo jengine la kutusaidia hapa ni kupata orodha ya wale waliofanikiwa kubaki ukumbini tangu mwanzo wa mkutano mpaka mwisho. Tupate idadi yao. Hii huenda itamsaidia Rasta Luihamu kuona kuwa uchaguzi wa wanakamati ya muda ulikuwa wa sauti nyingi au la. Nahisi jambo hili linamnyima raha kabisa kabisa.
Basi kwa leo ni hayo machache.
Wasalaamu!!
Kitururu,
Kuhusu jina mimi naona hili la "Jumuiya ya wanablogu Tanzania ndiyo linaenea, ila tatizo naona liko katika kifupisho chake JYWT, naona inakuwa kama Jumuiya ya Wanawake Tanzania vile au inataka kufanana jeshi. Sasa ili tusiwachanganye watu naona herufi 'B' isiachwe iwe JYBT, au mnasemaje?
Kwa kweli namwonea huruma Rasi. Hana amani kabisa na matokeo. Nimefuatilia sana rufaa yake, sioni akijibu hoja anazoulizwa zaidi ya kusisitiza kuwa hawatambui wanakamati ambao hakuna anayewalipa wala sidhani kama kuna faida yoyote wanapata.
Mimi siamini kwamba haelewi. Anaelewa. Sasa shida ni nini, hapo ndo maji marefu.
Sikujua kwamba mambo ya akina Mrema yapo bloguni.
Nakubaliana na mawazo ya Mija, kuhusu umuhimu wa jina la jumuiya kutochanganya watumiaji wa blogu na watu wengine.
Post a Comment