Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Yesu Mweusi

>> Wednesday, November 01, 2006

Moja ya picha imuonyeshayo yesu kama mtu mweusi.










Hivi karibuni sinema mpya ya kimarekani imetoka ikimuonyeshaYesu kama mtu mweusi. Sinema hii inaitwa The Color Of The Cross. Kuhusu swala la kwamba Yesu alifananaje ni swali ambalo limeulizwa na kuchambuliwa kwa miaka kedekede. Nachojiuliza ni kwamba , hivi kwanini watu wanahangaika sana kujua Yesu alifanana vipi? Hivi hii sio hali ileile ya watu kutaka kujifananisha na waliofanikiwa? Hivi hali ya watu kutaka kujulikana wanauhusiano na mtu maarufu, au wanafanana na mtu maarufu sio dalili ya udhaifu katika idara ya kujiamini?
Katika sinema hii kunakipengele kihusishacho rangi ya Yesu kama sababu nyingine yakumthulubu.Sijaiona hii sinema bado.Wewe je?

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mwandani 1:12 pm  

hivi Mungu ni mzungu au mwafrika?

luihamu 2:18 pm  

Ninavyoamini mimi Rastafarian,Mungu ni neno,na neno ni Mungu,kwahiyo Mungu hana rangi,hawa jamaa ni wajanja,watati wa ukoloni walileta mambo yote haya na kutupumbaza,kutufanya tuamini Yesu ni mweupe.Yesu ni Mungu kwa sababu Mungu ni Yesu.Kinachotakiwa hapa ni Imani yako na kuwa na msimamo katika imani.Jah ananiongoza kila siku.Mzee Simon asante kwa kuzungumzia hili jambo tena.Je!
Mzee Simon Yesu ni Binadamu?

Simon Kitururu 3:11 pm  

Luihamu , umesema Mungu ni neno na neno ni Mungu.Ukasema pia Yesu ni Mungu kwa sababu Mungu ni Yesu. Halafu ukasema kinachotakiwa hapa ni imani yako na kuwa na msimamo katika imani. Basi kimisimamo yangu Yesu ni binadamu.

luihamu 7:01 pm  

Hapa lazima niwe makini,la sivyo utanifunga goli la kisigino,nakubaliana na wewe kwasababu ni msimamo wako.

Anonymous 2:47 pm  

Nakubalina nanyi kuwa Yesu ni mwanadamu. Kama kuna mwenye taarifa au uthibitisho tofauti ningependa ajitokeze uwanjani.

Christian Bwaya 1:17 pm  

Nadhani swali analouliza Mwandani linahitaji utulivu. Ngoja nitue kidogo.

Anonymous 4:32 pm  

Ras Kit, FJ hapa!! Kwa kweli inavutia sana kuona vijana mko Ulaya lakini bado mnakumbuka mila za kiafrika, desturi na kwa ujumla wapi tulipotoka, tulipo ta tunapoelekea.

Lakini la msingi katika hili la rangi za manabii/yesu si jamii ya walikozaliwa/walimotoka!! Bali ni imani juu ya msikilizaji wa neno la Mungu. Kwa sababu hata maneno ya Mungu pia husema Nabii hakubaliki katika watu/jamii yake alimotoka!! Kwa hiyo Yesu kuwa mweusi hakutakuwa na maana yoyote kuonyesha mtu mweusi ni mtakatifu kuliko mweupe, au ana imani ya kimungu kuliko mtu wa njano !!! Wala kumfanya kuwa bora kuliko watu wengine!!

Nafikiri utakubaliana na mimi kuwa huku kuku wa kienyeji yumkinika kuwa mweusi, mwekudu,rangi ya udongo au madoa madoa hakufanyi kuwa bora kwa utamu wa nyama yake, akili zake, ujanja wake au nguvu zake za kike au kiume!!

Kwa hiyo badala kuangalia, au kutilia mkazo ya mambo ya rangi ya mwafrika....Nafikiri msisitizo, fikra na utashi wa sisi vijana wa leo wa Africa hiwe ni ktika kuangalia jinsi gani tulikubali kuingia utumwani, ukoloni na sasa ukoloni mambo leo ulijificha katika mifumo mipya ya kiuchumi ....GLOBALISATION, MILLENIUM GOALS NA kadhalika nyingi sana!!

Na tuweze kubali kuja na changamoto na kukutaa kukubali kila hoja/mipango ya mtu mweupe/mataifa yalioendelea, tuweze kukuza hali ya kujiamini ya watu wetu katika kufanya maamuzi, kuchagua, na kutoa vipaumbelea katika maeneo yatayotarakishia maendeleo ikiwa pamoja na kuthamini wabunifu wetu, utamaduni wetu, mila zetu, na watu wetu kwa ujumla!!!

Tujenge watu wetu waweze kuangalia mbele zaidi badala ya kuangalia wakiti wa sasa au wakati mfupi ujao(short term).

Asante,

Freddy John Liundi

Simon Kitururu 11:30 pm  

FJ asante kwa kunitembelea. Nakubali kabisa hoja yako. Naamini pia kuwa tatizo kubwa sasa hivi bado liko katika kupata jinsi ya kuweka hoja hizi katika vitendo. Kwa maana tusipo angalia kama ulivyosema basi tutaendelea kushindwa kujitoa katika mfumo ambao unatufanya mpaka sasa hivi tuwe na hali ngumu ndani ya bongo.Kama unavyoona hata matatizo ya umeme yatukumbayo, mimi naamini ni moja ya tatizo lililoletwa na kutoona mbele au kutegemea short term plans. Na hata tetesi nyingi ya kuwa ni nini jawabu la tatizo hili utakuta Viongozi wetu wanajali majibu ambayo hayajaangaliwa ni nini madhara yake katika muda mrefu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP