Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jifunze UFISADI- Sura ya KWANZA.

>> Friday, May 16, 2008

Mbinu moja maarufu sana ya kumshinda adui ni kumjua adui.

Si utani , ufisadi ni bomba la kitu maarufu duniani na waongeleao ufisadi mara nyingi ni wale wasiofaidika na UFISADI.

Siwezi kusema kuwa na utaalamu na somo hili ingawa nadhani kuwa, inawezekana hili somo halihitaji uende chuo chochote ili kufudhu jinsi ya KUMFISADI Mtu , Nchi au Kanisa.

Swali:

  • Ushawahi kujiuliza kwanini unaweza kuona jinsi gani MFISADI anavyofanikisha UFISADI hata bila kwenda kusomea popote wakati huoni taaluma ya PROFESA wa UCHUMI au wa KILIMO atatuavyo matatizo ya kiuchumi wa Tanzania utegemeao kilimo?
  • Unafikiri kwanini katika silabasi za shule ,hakuna kozi ya UFISADI?

Naamini UMIMI uko ndani ya binadamu tokea atokee duniani au enzi hizo binadamu walivyofikia wawili hapa duniani.

Naamini chembechembe za ufisadi zilianza kujijenga ndani ya binadamu kuanzia pale alianza kuamini uwepo wa uchache wa vitimiza mahitaji yamuwezeshayo binadamu kuishi.

Mahitaji ya binadamu na jinsi ya kuweza kuyatimiza yanaendelea kutofautiana kulingana na upeo wa akili ya binadamu ulivyo, hasa ukikumbuka enzi za KUTUMIA TREKTA na zile za KUVAA KIBWAYA , mahitaji ya RAIZONI, kunatetesi yalikuwa au bado yanatofautiana.

Kipindi cha kuishi kwa kuokota mizizi na matunda, mjanja alikuwa ni yule atakayeweza kuwa na mizizi na matunda wakati kuna uhaba wa mizizi na matunda. Lakini wakati hivi vitu(mizizi na matunda) viko vingi , ilikuwa huwezi kumtisha Mr Kidume, kwa kumnyolisha eti una mapera mengi kuliko yeye, wakati anajua kuwa hata pale apendapo kumuangushaga Binti Kitoweo jua likizama, ni chini ya mti wa mpera uliojaa matunda.

Ukiruka kutoka enzi za kupigania embeng'ong'o na mihogo mpaka kipindi hiki ambacho bado wengi hapa duniani tunaweza kupigania embeng'ong'o na mihogo ingawa wengine wanaendesha magari aina ya FERARRI na WANA VIJISENTI BILIONI kadhaa katika benki kadhaa hapa duniani, unaweza hata ukakubaliana kuwa AKILI za BINAADAMU ni UJINGA uendao na AKILI za kiBINAADAMU, hasa katika staili yake ya kusikilizia ladha ya kuridhika au MAFANIKIO.Inashangaza jinsi binadamu awezavyo kujilimbikizia wakati wengine wana njaa, kama unaweza kusahau UBINADAMU.

Unakumbuka NGAZI za MAHITAJI kwa mujibu wa Maslow (Maslow's hierarchy of needs?)

















DUH!
Naachia hapa kufundisha somo hili la UFISADI .
Unajua TENA, naweza kukudanganya bure!

Ila kumbuka kuwa chembechembe za ufisadi zipo tu hata ndani yako.

Usipoangalia , unaweza ukajikuta umeamsha chembechembe za UFISADI na ukazirutubisha pia kiaina.

Katalisti za kuamsha mshawasha wa KUFISADI ziko bwelele, zinakuzunguka hadi msalani pale ustukiapo maji hayatoki na pesa za kununulia karatasi za kujipakaza mavi sehemu zifichwazo na chupi hauna. Halafu unajua kufutia kinyesi ukutani nishai na mchanga unaweza kuwa na minyoo.

DUH!

Usitishike lakini! Labda tusipoharibu mazingira tunaweza kuwa na majani bado au mawe yafaayo kutumika kama MAKOKONEO.

LAKINI......!
Baadhi za Katalisti ziwezazo kuathiri ashki za UFISADI wako ni:
  • Utu WAKO
  • Umasikini wako au jinsi ufikiriavyo kuwa wewe ni masikini hata kama si.
  • Uelewaji wako wa staili yako ya kuridhika .
  • Udhaifu wako wa Muonekano au sehemu(status) yako katika jamii
  • Udhaifu wako ukuwezeshao kudokoa mboga ukiachwa jikoni peke yako au Ukiwekwa kwenye ofisi ishughulikiayo VITOWEO ;kwa mfano kama wewe Raisi ofisini , Mjumbe wa Nyumba kumikumi au kama VIJISENTI tu vinakatizakatiza kwenye kona yako halafu unahisi hutadakwa ukidokoa.
  • nk......kadhaaa wa kadhaaa.


JIADHARI!

DUH!
Samahani kwa simulizi chafu!

Hebu tumsikilize Ngozi Okonjo-Iweala akigusia maswala ya UFISADI au mambo ya : How to help Africa? Do business there



Au Angalia tu ujinga kama vile DUME ZIMA liwezavyo kutumia muda wake MUHIMU wa dakika kadhaa KULIA katika BIG GIRLS DONT CRY

DUH !

WIKIENDI NJEMA!

Mpate tu PAPA WEMBA au VIVA la MUSICA

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP