Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NAOMBA UFUNGUO wa MOYO wako ili UJIDANGANYE kuwa sitaUMIZA roho YAKO.

>> Sunday, May 04, 2008

Unaporuhusu mtu akujue, unampa huyo mtu ufunguo wa kiboksi cha UJUZI wa wewe ni nani.

Akujuaye halafu atake kukuumiza, huwa habahatishi madoido au staili ya kukutomasa kidonda.
Akujuaye ndio anaweza akawa anajua mpaka staili yako ya kulia, kupiga mayowe au hata ya kulamba kamasi lilengalo mdomo ukilia.

Lakini...
.. ni vigumu kukiri kuwa kama ufurahiavyo kumuona achekaye, kuna wachekeshwao na muonekano wako wa sura wakati unalia.
SI unajua unaweza ukawa unakunja sura kama unanusa kimavimavi wakati unalia?

DUH!

Kama watu waogopavyo ngurumo ya radi wakati wanajua ukisikia ngurumo maana yake radi imekukosa, ndio wengine wahudhunikavyo kumuona anayelia bila kugundua kuwa tatizo ni kile kimlizacho mliaji na sio aliavyo.

Kulia humsababisha mliaji asikie ahueni.
AU?

Tatizo ni kwamba, binadamu hapendi upweke kama anaishi maisha ya kawaida ya kibinadamu.
Utajikuta umelazimika kumpa mtu fulani funguo ya moyo wako ili achokonoe roho yako.

Nakutakia kila la kheri katika kusubiria uliempa ufunguo wa kiboksi cha ujuzi wa WEWE NANI afanye ubinadamu na kukuumiza kiduchu kabla haja pulizia.
Ndio maisha!
Kwani bila maumivu tungejua utamu ni nini?

Kwa kherini kiduchu wadau wa blogu hii!
Tutaonana tena kijiweni baada ya siku kadhaa wa kadhaa!
Nakuacha na Patrice akupe EVERYDAY GOOD

Au ngojea tu aseme HOW DO U CALL IT

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP