Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UTUuzuri WAKO , labda ni WOGA!

>> Wednesday, May 07, 2008

Hakuna uhakika akufanyiaye mazuri , anakufanyia mazuri kwa sababu anafurahia kukufanyia mazuri.

Lakini...
...yule mtu mzuri amepata umaarufu huo kwako na kwa jamii yako kutokana na tafsiri yako na ya jamii katika kutathmini aliyofanya hata zaidi ya ambayo hajafanya.

Inawezekana kabisa hata mimi na wewe tunafanya mazuri kwa sababu tunaogopa matokeo ya kumfanyia mtu mabaya.

Swali:

  • Ungekuwa una uhakika na kesho , kesho kutwa yako,mtondogoo au ....., una uhakika hakuna ambaye ungempiga konzi ?
  • Unauhakika unapima uzito wa UTU UZURi wa mtu zaidi kwa aliyokufanyia au asiyokufanyia ambayo ndio msaada?

Unaweza kubisha!

Lakini wapo wengi wanaogopa kukufanyia mabaya kwa kuogopa maswala ya wakishadedi.
Wangekuwa na uhakika na nanihii za baada ya kifo labda wangesha kubaka!:-(

DUH!
Naacha!
Siku njema!
Tulia na Sade akija na Smooth Operator (Jazz version)

12 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 10:17 am  

MKUU,NAOMBA ANUANI YA MAILA YAKO.

AMANI,RASTA HAPA.

Simon Kitururu 10:21 am  

skitururu@gmail.com

Anonymous 3:34 pm  

mzee wa kitendawili nakuaminia mkuu.
Ms Bennett

Simon Kitururu 5:41 pm  

@Ms Bennett: Asante sana!

Anonymous 12:43 am  

Bro simon, naomba nikuulize swali, ikibidi nijibu ilituingie pamoja mawazoni.

Hivi kwanini binaadamu, haoni tabu, napengine hujiskia fahari akijulikana anaenda kula au ametoka kula chakula. Lakini binaadamu huyu huyu hapendi na walahataki ajulikane anapoenda kunya au anapotoka kunya? Wakati huko kunya ni zao la kula, jee anataka wale alowaambia au walomuona anaenda kula waamini kwamba yeye hula tu, lakini hanyi?

Ni hayo tu mzee. Hem nichambulie kwa falsafa yako.

Simon Kitururu 2:00 am  

@Bablii:
Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana.Anamchezo wakujijengea mila na desturi ambazo mara kibao zinambana mwenyewe upande mmoja halafu kwa upande mwingine anadai anataka kuishi kwa uhuru na furaha.


Nafikiri chanzo cha binadamu kutotaka kuhusishwa na kitendo cha kunya ni harufu ya mavi.

Chakula huoanishwa na harufu ziloanishazo mdomo na zimtoazo udenda binadamu, halafu ni ujanja kitendo kizima cha kutafuta chakula na kula.

Binadamu hupenda kujulikana anaweza kufanya kitu na nafikiri kihistoria kutafuta chakula ilikuwa ngumu kuliko kunya.

Kwa hiyo nafikiri ni harufu na sifa zimiminikiazo binadamu kwa kuweza kunukia vizuri na kula vizuri zimfanyazo binadamu kuendekeza kuhusishwa na maswala ya kula kuliko ya kunya ambayo huja na harufu mbaya.

Anonymous 12:12 pm  

Ha ha ha thanx bro, duh umenifumbuwa macho, kwa hiyo sababu kutafuta kula kunatumia ujanja na maarifa, binaadamu anaona fahari kupambwa nayo, lakini sababu kunya hakuna ujuzi hataki hata aonekane anakunya lol! Na ile harufu mbaya ya kinyesi! Mi nilidhani labda hataki ajulikane kwamba anakinyeleo ha ha ha ha...!

Simon Kitururu 12:17 pm  

@Bablii: :-)

Anonymous 2:23 pm  

Sasa Bro Simon,umenifanya nizidi kuwa mdadisi...

Kwani huyu binaadamu anaeona fahari kujulikana anakula, lakini hapendi aonekane anakunya, anatofauti na yule binaadamu anependa ajulikane kwamba yeye kijigoo, mtaalamu wakutongoza, mtaani madada wote kashawapitia au yeye mrembo na mjuzi wa kuchuna mabuzi,ma-super star wote bongo kashatembea nao, lakini binaadamu huyu huyu akiukwaa UKIMWI hataki watu wajue? Wakati huu UKIMWI ni zao la ule ujogoo wake au ujuzi wake wakuchuna mabuzi!
'
Jee na hapa wanaogopa harufu au?

Nipe tena darasa mdogo wako mawazoni.

Simon Kitururu 3:12 pm  

@Bablii:
Naamini binadamu hujijengea tafsiri ya yeye ni nani katika jamii imfanyayo ajisikie hajapotea au ajijue sehemu yake katika jamii.Kijogoo au Mchunabuzi ni kitambulisho chake kwake na kwa jamii , hata kama ni mawazoni mwake tu mtu huyo.

Binadamu ajitambulishae kuwa mkristo au muislamu hata kama haendi kanisani wala msikitini, hasomi Biblia wala Korani , akikusikia unatukania Biblia au Korani , atakorofishika, kwasababu kinamna unakwaruza SENSE yake ya IDENTITY.

Sasa tukirudi kwenye swali lako.

Kumbuka jamii nyingi sehemu nyingi duniani,kihistoria, ilikuwa huhitaji kuwa kijogoo au kujua kutongoza ilikupata wenyeuke wengi. Mahari au misuli yako tu iliruhusu jamii kukuozesha mabiti wao.

Kwa wanawake, jamii nyingi mpaka leo, ukijisifia wewe mchuna buzi, watatafsiri kuwa wewe MALAYA.

Kinachofanya kuwa ukijisifia uchunabuzi leo , hautaathirika sana kama zamani, ni ukweli usiofichika kuwa ukaribu na mfumo wa familia na wajamii sasa hivi si ufanyao watu wawe karibu kama zamani.

Zamani , mtoto alilelewa na Kijiji kizima. Siku hizi jirani yako akimgombeza mtoto wako kwa kosa la kumfumania migombani akiwa na Abdalah, wewe na familia nzima yako, mnaweza kumtokea jirani na kumsema vibaya kwa kuingilia yasiyo mhusu.Siku hizi hata mwalimu anaogopa mwnafunzi kinamna na kwa binamu huwezi kujiendea tu ukakaa miezi sita bila ya taarifa.

Sasaa....

Hapa namaanisha kuwa umaarufu wa kijogoo ni kuwa kijogooo. Kijogoo anajitambua na kupata ufahari na kujisikia mtu katika watu kwa jinsi ahisivyo mnamuonea gele kwa matumizi yake ya kikojoleo. Akipata UKIMWI , maana yake inabidi aanze upya kutafsiri yeye ni nani katika jamii ,kitu ambacho ni kigumu. Na kama binadamu, ni vigumu kujua jamii itakupokeaje kama mwenye UKIMWI.

Nafikiri Kijogoo na Mchuna buzi wakipata UKIMWI ,wanaogopa tu kupoteza IDENTITY wajitambuayo nayo katika jamii.Unajua tena!Ukipata UKIMWI gia yako ya mtongozo uliyozoea inaweza isiingie.

Wote tutakufa, na maiti haisikii aibu,lakini bado jamii ya binadamu , kwa akili finyu za kibinadamu, inafikiri kufa kwa kipindupindu hakudhalilishi kama kufa kwa UKIMWI.

Labda kwa sababu UKIMWI bado ni ugonjwa mpya na jamii bado inauoanisha mpaka na usenge, dhambi na harufu mbaya kama hizo, ndio maana asilimia kubwa ya VIjogoo na Wachunabuzi wanaweza wakasita kukustua kuwa wameukwa MDUDU kwenye kona.

Anonymous 5:23 pm  

Ha ha ha ha Bro nimekupata ndivyo!

Ohh kumbe...! Sasa nazidi kupata mwanga lakini ndo nazidi kukishangaa hiki kiumbe kiitwacho binaadamu!Kiko "very complex"

Samahani naomba nikuchokoze tena, au kiufupi naomba nizidi kujichotea vikombe vya hekima kutoka kwenye bahari yako isiyokauka!

Hivi na hawa binaadamu waliopachikwa jina "mafisadi", inakuaje wanaona fahari watu wakijuwa kwamba wanamajumba makubwa yakifahari, wana magari mazuri ya bei mbaya, wanavaa suti kali kali, wanatibiwa hospitali za nje kwa harama kubwa, hata wakipaliwa na mate au wakinaswa na nyama kwenye jino wakati wanajilia vyuku vyao, lakini binaadamu hawa hawa (mafisadi)hawapendi wengine wajuwe mali na pesa hizo wamezipataje?
Hawa huwa wanaogopa nini? Duh nimekuchokoza, samahani!

Simon Kitururu 6:10 am  

@Bablii:Swali gumu hili. Ningejua jibu ningekuwa mstari wa mbele kuondoa matatizo ya UFISADI

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP