Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UDONGO uukanyagao Inawezekana ni MABAKI ya MAITI ya mtu au HAYATI Mjusi !

>> Wednesday, May 07, 2008

Kwa wengine ni mwiko kucheza makaburini !

Lakini...
.......binadamu wengine wanafanya pikiniki makaburini.
Swali:

  • Makaburini ni wapi?

Binadamu bingwa wa kuoanisha mboga za majani na chakula ,lakini sio mabingwa wakuoanisha kabichi au maharage na mavi ya kuku, mavi ya ng'ombe au mbolea fulani ambazo hunukia manukato ya choo.

Ukifikiria kidogo, utagundua kuwa MAJI YOyoTE utumiayo ni maji ambayo inawezekana yalishawahi kuwa mkojo wa tembo, mcheuo wa bata , kamasi la nguruwe au pia jasho la mmea kama unafualilia MZUNGUKO wa MAJI (water cycle)hapa duniani.

Kwa mtazamo mwingine, maji yoyote utumiayo, ni machafu!

Nampenda binadamu kwa uwezo wake wa kufumbia macho baadhi ya mambo na kuyatolea macho yale mengine kwa visingizio vya ajabu kama vile dini,utu au hata elimu.
Ukweli ni kwamba uyatoleayo macho ni kwasababu unaweza tu kuyatolea macho.
AU?

Kuna watu wana uhakika kuwa binadamu asipoelewa kitu atamsingizia Mungu au Miungu, lakini mimi nadhani mara nyingi binadamu asipoelewa kitu hulifungia macho na masikio hilo LIKITU.

Swali:
  • Unajua ukibanwa sana na kiu utakunywa mkojo?

Nafurahia mitazamo ya binadamu!
Maiti ya mbuzi , anaweza kuisifia kuwa ni bomba la Ndafu lakini hayati mjusi anaweza asimuite mshikaki.
Si vyakula vingine tunajifunza kuviondoa sumu au uchungu lakini tunaweza kutamka neno TAMU tukizungumzia bia na chai?

DUH!

Tafsiri za binadamu ni ngumu kuzielewa kutokana na ubinamu wake unavyocheza zigzag.

Chura, konokono, mbwa na popo , binadamu mwingine atasifia ni chakula kizuri, wakati binadamu mwingine atakushangaa ukila nyama ya ng'ombe, nguruwe au matako ya sungura.

Binadamu fulani ataamini kuwa binadamu wote ni watoto wa Adamu na Hawa ,lakini ataku-Saddam Hussein au kukuKOLIMBA ukimstua kuwa kaoa dada yake au kamchumbia kaka yake kinamna.

Swali:
  • Hivi kama binadamu wote ni ndugu, unashangaa nini ukisikia kuna vita duniani?
  • Kwani hujawahi kukorofishana na ndugu yako?

Binadamu eeh!

Najua wewe binadamu unajua kuwa tokea binadamu aanze kuwepo hapa duniani kuna kaburi fulani la Adamu na Hawa halijulikani lilipo.

Na nafikiri unajua ni virutubisho gani viko mwilini mwa mwili wa binadamu ambavyo mimea na samaki huvigida.

Usifikiri nakutukana......
....... nikijaribu kuhisi kuwa kuna uwezekano kuwa binadamu wote washakula Watu.

Usifikiri nakutukana .......
.......nikijaribu kuhisi inawezekana nyumba yako imejengwa kwa kutumia mabaki ya maiti za watu na chakula ulacho kinaweza kikawa na chembe chembe za Adamu na Hawa.


Lakini....
Hakuna noma!
Najua ni ujanja kuogopa MAITI!

Labda mimi na wewe ni binadamu tu, ndio maana mimi mwenzio nikiona mchele nafikiria maswala ya ubwabwa .

DUH!
Kwangu fikira za ubwabwa ni ubwabwa tu .
Tofauti za ubwabwa ni maswala ya ubwabwa unaulia nyumbani, msibani au ni Darling ,kishtobe au zee la nyeti limepika.

DUH!
Naacha!

Hebu tuangalie mapenzi ya BABA na MWANA kidogo....


Mpate Neneh Cherry akupe kibao WOMAN

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP