Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUKATA TAMAA ni UJANJA

>> Saturday, May 03, 2008

Kuna atakaye sema kukata TAMAA ni kitu kibaya!

Lakini...
...ukikata tamaa, utajipa nafasi kuwa HURU kujitoa katika MNASO.
Kukata tamaa ni SANAA kali, si kila MTU ni stadi katika kukata tamaa kinadhifu katika swala ambalo anahisi kukata tamaa na KUCHEKESHA ni saresare maua.

Ukikata tamaa, unaweza kujikuta umeacha kuhangaikia kitu.

Ukikata tamaa , unaweza kuacha kuchamba kwa sababu tishu, maji, mchanga, majani au jiwe utumialo kama MAKOKONEO pale msalani ,vinakosa umuhimu sana kwako kutokana na mnuko wa mvundo wa chooni na MANUKATO ya UTULI, hukosa tofauti kubwa.

Ukiweza kuishi UKIWA na MATUMAINI wakati unaweza kufanya afanyacho aliyekata TAMAA, wewe unaFURAHA maishani na jirani hakutishi.

Swali:

  • Unakumbuka kama ushawahi kutamani inawezekana huhesabu tu ni mara ngapi ulikata tamaa?
  • Unajua inawezekana kuwa kama tamaa zote si mbaya basi kukata tamaa kwingine ndio ushindi?
Naamini kuna ngazi za kukata TAMAA.
Wewe kama ni mtu wa dini lakini umefikia kwenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya MKUYATI, basi kuna maeneo unahisi kuna MATUMAINI na umekatia tamaa dini lakini bado unatafuta kuendeleza TAMAA ya KITU na sio KUIKATA.


NAAMINi....
...kila kitu kinaMPITO!
Kama unasikia UTAMU sasa hivi, USIKATE tamaa, UCHUNGU uko kwenye kona , utakudaka tu hata kama sio leo.

Kama uko kwenye MACHUNGU leo hii, kumbuka UTAMU ni kifo.Utakudaka tu, hata kama sio leo.
USIKATE TAMAA!

Swali:
  • Hivi inawezekana kuna UTAMU kwenye UCHUNGU?

Basi bwana NAACHA!
WIKIENDI NJEMA!
Nakuacha na KY-MANI MARLEY akikupa kibao COUNTRY JOURNEY

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP