Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI unamkana NDUGU yako aliyedakwa UCHAWI.

>> Sunday, May 04, 2008

Kukana kitu ni jitihada za kutaka kuhakikishia wengine kuwa huhusiki kwa sababu kwa kisiri na kama wewe ni mkweli kwa wewe, ulichofanya kisha kuathiri na hata ukaneje ushaathirika nacho.

Ukishaonja ukwaju , unaweza kushindwa kuelezea tofauti ya utamu wake na embe bolibo, lakini hata ukane kwa wengine hujui utamu wa ukwaju, unajua chini ya dhamira yako kuwa ukwaju na asali vinautamu tofauti.

Nikikuudhi au kukutia aibu, unaweza kukana uhusiano wetu , undugu wetu , hata kama watu wanauhakika mimi fundi koroboi wako.

Nikisifika, unaweza kusimulia mpaka jinsi babu yako mzaa babu na shangazi ya babu yangu walivyokuwa marafiki shule ya vidudu, ilikuonyesha ukaribu wako kwangu.

DUH!

Lakini....
......Hata ukikana, UKWELI uko palepale.

Gari la zamani hata ulipake rangi bado ni baiskeli ya zamani.

Kukana inawezekana , na watu wanaweza wasijue ukweli kwa muda fulani kwa sababu binadamu ni mvivu wa kufuatilia ahisiyo ugumu na ambayo hayamsaidii kupata utamu HATA AKIJUA sasa hivi.

Unaweza ukawa unataka kujua kivipi BALOZI wa NYUMBA kumi kumi wako katajirika haraka haraka alipochukua ofisi kwa sababu zako binafsi za kuhisi KUTAJIRIKA KWAKE ni KUNYONYWA au kuibiwa kwako, la sivyo inawezekana usingejali kwanini ghafla tu, RAIS wako MTUKUFU kawa bilionea wakati nchi ina madeni.

LAkini....
.....jina lako likiwa linatajwa mara kwa mara likihusianishwa na uchawi, MCHAWI au Mama Ntilie, kuna watu kutokana na uvivu wa kufuatilia na urahisi wa kuhitimisha , watakua wanadhani wana uhakika kuwa wewe mchawi, ulilogwa au ni MAMA NTILIE.

Mchezo wakuhitimisha bila ya kuwa na vigezo vithibitishavyo nani alimpa kuku mimba lililo rutubisha yai la kwanza, ningependa libakie tu katika sentensi; kati ya yai na kuku sijui nini kilitangulia kuwepo duniani.

NAKUBALI unaweza kudai ni yai lilitangulia bila ushahidi zaidi ya kwamba katika kundi wewe ndio UNASAUTI KUBWA na wengine wameathiriwa na jamii kiasi kwamba katika mambo mengi kiduchu ya jamii, WAMEFIKIA kukubali tu kutokana na kutojiamini kama wewe ujiaminivyo katika hata mambo usiyojua.

NAKUBALI unaweza kukana!
Kana tu, hakuna noma!
Swali:

  • Ushawahi kukana wewe sio wewe?
  • Unajua unaweza kukana kile kitu lakini ukaendelea kuona aibu kutokana na kitu hicho hicho ulichokuwa shupavu kukana?

Usisahau kuwa, mara nyingi unakana kutokana na kujihami kuwa ukikubali utajiweka katika mazingira mabaya zaidi.

Usisahau kuwa, hata usiyo yaelewa lakini ukahisi ukikubali utaenda paradiso, hukawii kukiri kuwa wewe Msabato au MUNGIKI.


Naacha basi topiki hii usije ukanikana bure!
Samahani lakini kwa kukutia aibu!

LAkini....
WHO wrote the BIBLE pt1?(msikilize basi Robert Beckford)


Kuna mdau kanistua kuwa nagusia sana dini .Napenda kukiri naguswa sana na dini na ni mifumo yake tu inayonizingua....
Lakini nasikiliza ya ulimwengu tu kama ya Timbaland na Magoo wakikiri INGAWA hawamuelewi......(samahani wanatumia lugha chafu!)

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP