Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nataka , HATAKI!Akiwa TAYARI au akitaka, MIE nimechoka!:-(

>> Tuesday, May 13, 2008

Katika maswala ya" NATAKA, HATAKI , akiwa TAYARI nimechoka", najaribu kuangalia Mahusiano ya muda, watu na tukio litokealo , hata kama tunaweza kusingizia kuwa haya maswala ni moja ya sababu zifanyazo kuwa wewe umepata na sisi wengine tumekosa.

Udhaifu wa kibinadamu, hauruhusu tuwepo sehemu zote au tuwepo katika nyumba wahitajiyo hausiboi au hausigeli mwenye sifa kama zetu wakati au siku wenye nyumba wasubiriyo mtu agonge hodi, akitafuta kazi.

Ni kweli inasemekana kuwa udhaifu wa binadamu unatofautiana ukiuchungulia katika mida tofauti au maeneo tofauti.

Kwa hiyo ,...
....inaweza kuwa ni kweli, ndani ya muda au siku fulani, kumtongoza HIDAYA ,anawezakukubali kirahisi kuliko wengi wahisivyo kutokana na wamjuavyo kwa sifa zake za kununia wanaume.

Kwa hiyo,...
.... kuna muda unaweza kujikuta umefanya dhambi kirahisi zaidi kuliko jana.

Kwa hiyo ,....
......inawezekana ndani ya muda fulani, ni rahisi kuliliza jibaba zima hata bila KULIPIGA roba ,kwa kulitukana kuwa ni ;KUBWA zima jinga!

Swali:
  • Unakumbuka kuwa labda ungecheza LOTTO sasa hivi wakati unanisoma hapa, labda ndio muda wako wa kushinda?
  • Hujawahi kushindwa kitu watu wakisifiacho kwa urahisi wake?
Inasemekana kila mtu ana nafasi yake yakuwa milionea au kupata , kama atacheza mchezo sahihi katika dakika, sekunde au muda sahihi.


Uhusiano wa kitu kiitwacho BAHATI NASIBU na ashindaye bahati nasibu, ni uhusiano wa mcheza sahihi katika muda sahihi na ndani ya mchezo sahihi.

LAKINI ...
...Kama kila mtu angeweza kugundua siri ya kucheza sahihi , muda sahihi , ndani ya mchezo sahihi, inawezekana WATU WOTE uwajuao, WANGEKUWA WANALIA sasa hivi, na hii DUNIA yetu yenye mapungufu isingeweza kuwepo tena , kutoka na mtu kufanya kitendo sahihi kama cha kulipua mabomu ya nyukilia.

Tukumbuke kuwa, kucheza kwako sahihi iliumpate Hidaya au Hamisi, kucheza kwako sahihi ili upate kazi fulani au mshahara fulani, kuna ambaye mchezo wake sahihi atakao kuucheza sahihi, ni kujaribu KUKUUA WEWE kutokana na rangi au sura yako, au kukuliza kutokana na afurahiavyo staili yako ya kulia.


Sidhani kama ni kwa bahati mbaya tu DUNIA HII tuishiyo iko kama ilivyo.
Sidhani hata binadamu wajaribu vipi ,wanaweza kuondoa mapungufu ya binadamu na dunia hii.

Kwahiyo nafikiri....
.. bado kuna ambao tutawaita kuwa wana bahati kutokana nakufikiri kila wakijaribu kitu fulani , wao hupata wakati siye tukimngoja HIDAYA uchochoroni, hapiti njia hiyo siku hiyo.

SWALI:
  • Unakumbuka umpendaye anaweza akawa anampenda yule ambaye anampenda yule akupendaye ambaye humpendi?
  • Unakumbuka kuwa hapo hapo katika barabara uivukayo, KUNA MTU atagongwa au alishagongwa muda fulani?

Katika maswala ya kukosea TIMING au kamuda, unaweza kujikuta unawaza...
....Ningependa kuonja sasa hivi , lakini dhambarau hazijaiva.
...Ningependa kuonyesha penzi, lakini mbona sina mpenzi zaidi ya hili limtu niishilonalo kwa kuogopa nini jamii itasema ndoa ikivunjika.


Lakini.....
...Mpenzi wako achekaye ukimtekenya, sikushauri umtekenye ilikujaribu kumpoza au kumuondolea maumivu ya kichwa au msiba.

Na kuna wakati kama hutaki kushindwa, ni afadhali usimpe kauli ya kutaka mkacheze MCHEZO wa BABA na MAMA au wa KUIBA yule atokaye MSIKITINI au KANISANI, wakati utaalamu wako wa kauli unashindana na wa PADRI au SHEKHE, ambaye ashamuingiza akilini umlengaye, mahusiano ya tamaa zako mbaya za kibinadamu na DHAMBI au AHERA.



LAkini.....
.....Nafikiri pamoja na udhaifu wa binadamu, ni rahisi kugundua kuwa ukirudiarudia mara nyingi kitendo kwa kutumia njia ujuayo ni sahihi, unaweza kujikuta UMEPATA kazi uitakayo, umepata MIMBA au umefanikiwa kufanya kitendo sahihi ndani ya muda sahihi na kweli jiwe ulilorusha jikoni kwa mtu , limempiga BABA mwenye nyumba aliyekwenda kuonja mboga kisiri jikoni wakati MAMAA anasukwa nywele kibarazani.

Naamini kama tunajitahidi kufukuzia kitu, sekunde ijayo inaweza ikaoanisha kitendo sahihi , mahali sahihi na muda sahihi na kutuwezesha kufanikiwa lile jambo au kufa.

AU?
DUH!
Samahani niko tu MAWAZONI kidogo!
NAACHA basi!

Mpate LUPE FIASCO katika FIGHTERS


AUtwende tu na PEPE KALLE kumtafuta kipenzi HIDAYA

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP