Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SAMAHANI, nakojoa!Si ni KITENDO tu cha Kibinadamu?

>> Friday, May 09, 2008

Si siri!

Binadamu huridhika kufanya kitendo kwa muda fulani mfupi tu.
Ukimzidishia muda katika kitendo, anaweza kukiita kitendo ADHABU.

Swali:

  • Unakumbuka kitendo binadamu ajinomacho, kama kula maparachichi, mafenesi, migagi au kukuna kipele, ukikiongezea urefu wa muda, BINADAMU anaweza kusema; utamu wake umeyeyuka au kugeuka na akaugawia jina ;UCHUNGU?
  • Unafikiri ni muda gani kitendo chako cha kujua na kufaulu mtihani kinadumu KABLA HUJAHITAJI tena kufanya kitendo cha kujisomea na KIJIFUNZA upya, iliubakie na sifa ya kuwa;WEWE UNAJUA?


Vitendo vya kibinadamu NISHAI!

Hata kama huvipendi , unawezalazimika kuvirudiarudia tu ili uishi au uendelee kuwa MJUAJI:-(

Hata kama umekula sasa hivi, lazima tu itabidi ule tena baadaye au kesho, kwa sababu ya njaa ikupendavyo na kutokukuachia uingie uvivu wa matumizi ya baadhi ya MATUNDu ya mwili yakufanikishiayo hata KUCHIMBA mzizi.

SIna uhakika!

Lakini...,
......
nahisi nataka kujaribu kuongelea vitendo binadamu afanyavyo duniani hapa,
kwa kutumia mfano wa kitendo binadamu afanyiacho mazoezi kila siku, ingawa bado siku mojamoja anaweza bado kujisaidia pembeni kidogo ya tundu la kidaka haja , KWA BAHATI mbaya.

Sasaaa....
......Kukojoa ni moja ya vitendo mamilioni , VIFUPI, binadamu afanyavyo na awezavyo kudai amemaliza au kabla hajamaliza akakujibu kutoka chumba cha kujisitiri kuwa ;ANAKUJA sasa HIVI!


NArudiA....
....Tatizo la vitendo afanyavyo binadamu, ni ulazimikaji wake wa kuvirudiarudia kabla hajafika kwenye
ZE KABURI.

Lakini......
......Tatizo au uzuri wa binadamu, .....

.....ni jinsi anavyoweza kushindwa kustukia kuwa kitendo hicho hicho cha KULA UGALI , anakifanya tofauti kila akirudiapo na kuwa, utamu wa ugali huohuo aulao ,unatofautiana ladha katika tamutamu ya TONGE la kwanza na TONGE alibwialo akishashiba.

Tatizo mojawapo la ubinadamu , .....
......ni ugumu wake kwetu sisi bin-ADAMU, kukubaliana naye MTU, kuwa amemaliza kitendo na HAWEZI kufanya ZAIDI, hasa tukikumbuka kuwa INGAWa KITENDO kimefaNYIKA, baada ya muda fulani mfupi ; nyumba itabidi kupakwa tena rangi, na labda itabidi MTU arudi tu tena jikoni, ilikujihakikishia uwezekano wa kurudi msalani.

DUH!

Lakini haishangazi,.....
.... mjanja anaweza kutamba kuwa ashafanya yote na kumaliza, kama atafumbia macho ufupi wa maisha ya kitendo kilichofanyika.

Na...
....Labda ni kweli vitendo hufanya zaidi ya maneno.
SI ndio maana kunawapatao UKIMWI au mimba kutokana na kitendo?

Swali:
  • Unamjua binadamu yoyote aliyemaliza kutenda ?
  • Hudhani kuwa kitendo binaadamu akifanyacho na kukimalizia vizuri ni kitendo cha kufa kwake mwenyewe?
Kabla sijaendelea kukunong'oneza.......

Samahani kwa kutamka neno KUKOJOA hadharani , hasa kama neno kukojoa linakukumbusha aina maradufu za KUKOJOA!

DUH!

Nakukubalia kuwa kuna vitendo ambavyo si lazima uvitamke au umwambie mtu kuwa unafanya au ulifanya KWA sauti.

Lakini.......
... uzuri au ubaya wa kitendo chochote afanyacho binadamu, ni ufupi wake katika kipimo cha muda ambacho binadamu anaweza kukiri ladha ya utamu wake.
Unaweza kubisha...
.......lakini binadamu hachukui muda mrefu kukinaishwa na kitu , kufa au kufanya kitendo kiwezacho kumjaza mimba asiyeficha maeneo.(Samahani kwa lugha chafu, namaanisha , asiyeficha sehemu nyeti au za siri)


Katika swala la vitendo sisi binadamu tufanyavyo....
...ingefurahisha kama ingewezekana kuwa ; kama umetubu leo au umeomba masamaha jana, maana yake hutamkosea tena yule kidume, kidosho, MWENYEZI Mungu, au yule binadamu,katika vitendo au mnong'ono, kesho.

....ingefurahisha; kama ingewezekana binadamu kumaliza ulichoanza kabla ya kulala , hasa kutokana na kutokuwa na uhakika na uwezo wa binadamu wa kufanya kitendo cha kuamka, baada ya kulala.

Swali:
  • Unafikiri YESU , Mtume Mohamedi, au Muheshimiwa DItopile walimaliza?
  • Kwa nini ukianza kitendo unafikiri ni lazima umalizie?
Samahani kama nakukwaza au unafikiri nakufuru!

Lakini...
...Labda kuna kitendo umeanza au ulianza , ambacho inabidi umalizie kibinadamu au inabidi ufanye tu!

Fanya tu basi hicho kitendo!
Inawezekana MARA hii kitendo chako kikalipa OOHOO!
Nakutakia kila la kheri!

Naacha HII topiki nisije nikamalizia kitendo bure halafu ukadharau ubinadamu wangu!

Kabla sijakuacha, hebu tuangalie kitendo cha binadamu ambacho wengi wangependa kukifanya KWA SIRI.Namaanisha kitendo cha KUJAMBA, ambacho unaweza kushangaa kushuhudia kuwa kinawachekesha binadamu kadhaa kiduchu, kama sio mimi na wewe!

Unajua, labda umeangalia kitendo cha kiJINGA?

Tumuachie tu BOB Marley atukumbushe hali halisi katika wimbo CONCRETE JUNGLE

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP