Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KATIKA mwendo WA MARINGO, kuna WATIKISAO matako!

>> Friday, May 09, 2008

Anayeringa MJANJA!

ANAYERINGA , amekuzidi kwa kufanikiwa KUJIDANGANYA kuwa, kuna kitu amekuzidi.

Ukitaka kujua kuwa anayeringa ni mtundu, fikiria yote uyajuayo tokea uzaliwe kuhusu binadamu, yakuhakikishiavyo kuwa, hakuna binadamu asiye na kasoro, na jinsi gani akufungaye katika mchezo wa karata, uwezavyo kumshinda katika mchezo wa kuruka kamba au kumshinda kwa ulafi.


DUH!
Sitanii!

Binadamu katika ujazo , wote ni sawasawa, kutokana na mapungufu yao na waliyobarikiwa ambayo hutofautiana kutoka mtu mmoja mpaka binadamu mwingine.
Swali:

  • Ushawahi kufananisha vitendo vya anayeringa na yule binadamu watu wamuitaye TAAHIRA?
  • Unauhakika na vigezo vyako vikuhakikishiavyo kuwa binadamu huyuhuyu aendaye msalani kama wewe , anakuringia?

Lakini....
... anayetembea kwa maringo , hukimbia kama mimi na wewe tu , kipepe kasingiziwa, ukimsakizia MBWA.

Lakini....
......Unauhakika huringi?

Nisikufiche!
Sidharau waringao ingawa siwaelewi.
Nahisi kuna kitu wanapata ndio maana wanaringa.

AU?

Lakini...

..Mringaji ndio atumiaye nguvu na achoshaye ubongo katika kujiandaa na kufanikisha kukuringia.

Anayeringiwa ana bahati!
Anaweza akaamua kutomwangalia anayeringa na kupumzisha macho na kidubwana wengine wakiitacho ROHO.

Swali:
  • Kama unanyanyasika kwa kuringiwa , unafikiri AKUringiaye alitarajia nini?

DUH!
NAACHA!
WIKIENDI NJEMA!

Twende GABON utulie na OLIVER Ng'oma akija na Muetse

Au mpate tu Yasmine JET akija na Detachement

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDWIN NDAKI (EDO) 1:16 pm  

Mstahiki meya wa HELSINKI..mzima wewe.

Naona mambo ya kuringa..sijui nisemee au nisiseme.

Mimi huko kijiji kwangu kichwa kinaniuma jinsi mafisadi wanvyotafuma nchi.

IJUMAA NJEMA

Simon Kitururu 1:24 pm  

@Edo:
Lazima Kichwa kiume kwa sababu Mafisadi maarufu sikuhizi!:-(

Nahisi ukishakuwa FISADI unapofuka macho na kuwa kiziwi.Bila hivyo, nashindwa kuwaelewa ni kwa jinsi gani wanaweza kutafuna nchi wakati wanajua hali halisi ilivyokuwa mbaya na utafunaji wao usivyo saidia.

:-(

Ijumaa Njema MKUU!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP